Mmmh hivi hii ni haki

Mmmh hivi hii ni haki

Huyu bosi atakuwa genius sana, yaani ka-extrapolate tukio akaona next time kwake safi sana hiyo ndio dawa yake....:tongue: Na ndo maaana Lwambo 'Franco' alisema muongo na mlozi ni watu wa kuchoma!!
 
Si haki kwa yeye kufukuzwa kazi, the boss had ZERO basis to fire her .
Yes, amedanganya but what she lied about has got nothing to do with work.
Yes, mwenzie kapigwa na kulazwa, but she is not the one who raised her hands
and beat up the woman.

Eti "nilikua nafikiria kukufukuza kazi siku nyingi ila sikua na sababu ya msing!" , How professional is that!! Besides who in their right mind will say anything like that, when terminating someones job?
 
Huyu aliyefukuzwa kazi kwa maono yangu ni Kitunguunyanya mwenyewe.

Pole sasa, umefukuzwa kihalali kabisa maana umepewa Mshahara wa Mwezi mmoja ambayo kisheria hapa TZ ndio matakwa ya termination within 24hours. Cha muhimu jifunze kutokana na makosa kazini watu wakikaa sana ni masaa 8 kwa sheria za Tanzania, fanya kazi siyo sehemu ya kuvuruga amani, maana kazini bila amani kazi haziendi kunahitaji ushirikiano wa hali ya juu sana " Team working".

Ukienda sehemu nyinge kutafuta Kazi jitahidi wasijue huo uozo maana watakunyima kazi kwa kigezo hichohicho. Ila sijajua kwanini Mmeo akufuke Home baada ya kufukuzwa kazi? hapo ndio kuna utata?! ebu fafanua au alikuwa awala siyo mme?au ndio siku ya mkosi?

Nilitegemea swali lako liwe kama mme amekufukuza kihalali au la! Maana pia kuna haki zako ndani ya ndoa kuliko hata kazini.

Kingine pia tujuze kuhusu mafao yako ya NSSF au ndio wanakula wakina Zito bila kujali unapata shida kiasi gani? au ulikuwa ukatwi na kwanini?
 
Back
Top Bottom