Ili ndoa iwe nzuri, yenye amani na upendo inatakiwa ijengwe kwenye misingi ya mambo mengi (inategemeana na ninyi wenyewe) lakini muhimu zaidi ni mapenzi mliyonayo kati yenu ninyi watu wawili na dini .:love:
1-Kutokana na Imani ya Dini tunafunga ndoa kwa vile tumeambiwa kuwa tendo la ndoa kabla ya ndoa ni dhambi, hivyo ni kama vile tunafunga ndoa ili kungonoana kihalali (usininukuu), hapa inawezekana kukawa na mapenzi au matamanio.
2-Kutokana na Imani hizo za Dini pia tunafunga ndoa ili kujenga familia bora inawezekana kusiwe na mapenzi.
3-Tunafunga ndoa ili kuwa na heshima mbele ya jamii (Africa zaidi) au kuondoa mkosi, hapa tutafunga ndoa bila mapenzi.
4-Tunafunga ndoa kwa vile tunalazimika kufanya hivyo kutokana umri, hapa vilevile mapenzi hakuna.
5-Tunafunga ndoa kwa vile tumeelewana kuwa kwenye uhusiano na kugundua tunapendana na kutaka kuishi maisha yetu yote pamoja (Kisasa).
6-Tunafunga ndoa kwa vile wazazi wanataka ufanye hivyo, hapa utafunga ndoa na yeyote atakaejitokeza bila mapenzi, nasikitika kusema tena kuwa hapa mapenzi hayapo.
7-Tunafunga ndoa kwa ajili ya kupata sifa, umeoa/olewa na mtu kutoka kabila/nchi fulani, mtoto wa fulani, mzuri, maarufu n.k. mapenzi hakuna.
8-Tunafunga ndoa kwa vile marafiki zetu wote wamefanya hivyo na wewe unahisi kuwa nio pekee umebaki bila mume/mke, hakuna mapenzi.
9-Tunafunga ndoa ili kupata msaidizi, iwe ni kupikiwa au kujikimu kutokana na ugumu wa maisha,