Hapo kwenye bold..utata mtupu!
Human psychology iko kwamba, mara nyingi unapoingia kwenye uhusiano ambapo tayari alikuwepo wa mwanzo hasa kwenye kesi kama hii ya mke "aliyeondoka siyo kwa kupenda bali kwa mapenzi ya mola", "wakuja" ana kazi kwelikweli.Kuna kipimo tayari cha utendaji!
Mume huyo ana kazi ya kuvuka kizingiti cha kulinganisha. Ajue kila mtu ana vionjo tofauti. Bahati mbaya sana mke wa pili hajafikia kiwango kile na hata hawezi kulingana kwa vionjo maana binadamu wako tofauti.
Mume ana bahati mbaya kuwa kilinganisho kimetokea kwenye tendo hilo.Wengine wanaweza kujikuta hawaridhishwi na mapishi, usafi, tabia njema, na mengineyo.
Cha kufanya sidhani ni kuongea na mke mpya kuhusu hili swala bali ni kwa mume kujitahidi kuzoea vionjo vipya na hata kujaribu kumwelekeza mke mpya nini akipendacho na kuepuka kuvuta hisia kwa marehemu!