Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
ACCRA, Ghana - Mtu mmoja amefariki na wengine kujeruhiwa vibaya baada ya msafara wa Rais Akufo-Addo kupata ajali, akirejea Ikulu ya Accra baada ya kushiriki mazishi ya aliyekuwa Mbunge wa Ejisu John Kumah.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Makutano ya Bunso, Mkoa wa Mashariki. Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema, chanzo cha ajali hiyo ni lori lililokatiza msafara huo.
Polisi wamesema, Gari iliyokuwa na Rais Akufo-Addo haikuathirika wakati wa tukio hilo. Maafisa wawili wa usalama wa rais wameripotiwa kuumia zaidi na wamesafirishwa hadi jijini Accra kwa matibabu zaidi.