Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Jicho la Tai

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2012
Posts
1,450
Reaction score
600
Watu waliokuwa wanatumia pikipiki wamempiga risasi mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari na kumpora begi na kisha kutokomea na pikipiki yao.

Mtu huyo amepigwa risasi na kufariki papo hapo. Inauma sana.

Natamani pikipiki zitolewe kabisa mjini.

=========
UPDATE: May 01, 2014

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.

Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Dah aliacha vioo wazi? Tatizo sio piki piki mbona nchi zote kuna hizo mtrbikes? Just police hawafanyi kazi yao

kwenye shida ndio mnawakumbuka polisi?? Lakn hao ndio tunawau,tunawaita njaa kali,tunawaita mbwa tunawadharau kama hatujui wapo kwa ajili ya nn..... Mm naomba polis walegeze kamba ili ijujlikane mwanaume ni nani na mwanamke ni nan?? Viva majambaz pigen kaz mjin hakuna kizuiz polis wamekata tamaa na mambo wanayofanyiwa na serikali na wananchi. Wapo kwenye mgomo wa kimya
 
Kuna haja ya jeshi la polisi kuweka sheria watu hawaruhusiwi kutembea na kiasi kikubwa cha fedha bila ulinzi.

Hivi mtu unajibebea mamilion tena huna hata hofu.

Kwa jins matukio yanavyozidi huu ni mchezo wa majambaz na wahusika wa karibu na alieibiwa.
Tusubiri uchunguzi
 
Kuna haja ya jeshi la polisi kuweka sheria watu hawaruhusiwi kutembea na kiasi kikubwa cha fedha bila ulinzi.

Hivi mtu unajibebea mamilion tena huna hata hofu.

Kwa jins matukio yanavyozidi huu ni mchezo wa majambaz na wahusika wa karibu na alieibiwa.
Tusubiri uchunguzi
 
Piki piki na kubeba lundo la fedha kwenye gari binafsi ni vitu viwili tofauti. Ukiona wamempiga risasi ujue walimjua sana huyo mtu na walijua naye si mchezo. Wakamuwahi. Inaonekana na yeye alikuwa komandoo ndo maana akajiamini kuchukua hilo fuko peke yake.
Jamani, mkisema pikipiki ziondolewe ni ujinga tu huo. Kwani kulipokuwa hakuna hizo boda boda, kulikuwa hakuna wezi? Polisi nao wajifunze mbinu mpaya. Kwani kama ni boda boda mbona tunawaona polisi wakivinjari nazo huku mitaani wakisaka machangu??
Semeni kuwa, labda hawajui matumizi ya piki piki au wanapata sehem yao. Kamanda Kova atapata intelijensia mpya sasa hivi.
R.I.P.
 
Hao wauaji ndo unakuta wanakula bata hapa mjini na kufadhili CCM
 
Back
Top Bottom