Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Ni ngumu kuchangia hapa kwani uwezekano wa hata kuuana wao kwa wao pia upo! Au alikula dili la watu akataka kuwaingiza mkenge! yote yawezekana. Tusubiri Intelijensia itasemaje.
 
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?

Kazi zao ni hatarishi sana, usifikiri kazi ya kuiweka nchi ya watu zaidi ya millioni 40 kwenye usalama ni kazi ndogo, ni kazi kubwa na ya hatari, wanakumbana na kila aina ya matatizo kwa kuhakikisha kuwa wengi wanabaki salama.

Hao vijana wetu wanakumbana na mengi sana na inabidi tusikitike kwa kuondokewa na mtu anaejitolea maisha yake kutulinda sisi.

Ingawa siwezi kukataa kuwa kuna wengine si waadilifu na hutumia fursa ya kazi zao kujineemesha wao wenyewe au kunyanyasa wengine kwa faida yao (Hii si kwa watu wa usalama tu, wengi sana wako hivyo hata baadhi ya wanasiasa) lakini, kama ijulikanavyo, "kwenye msafara wa mamba, kenge hakosekani".

Hilo swali lako kuhusu nani yuko salama? kumbuka, wewe kwa jina lako nahisi ni Muislaam (ingawa majina si kigezo kamili cha kujuwa dini (njia) ya mtu), kama ni Muislaam (nadhani hata Wakristo) tunaamini kuwa tunaishi kwa amri ya Mwenyeezi Mungu na hakuna mlinzi aliye bora kwetu zaidi ya Mwenyeezi Mungu. Tuzidishe imani.

Inna li Llahi wa Inna ILlahi Rajiun.

Naomba kujua kati ya silvanus mzeru na mbena malumbi nani aliyeuwawa hapo karibu na uwanja wa ndege.huyu mzeru ndio anahusika na majengo na mradi mkubwa wa chilakale resort huko moro wakihusiana na familia ya mkuu wa kaya wamejimilikisha hadi mlima wa uluguru kote ni majengo tuuu km uyoga. Kwa wale waliofika chilakale resort hata mabango ya hiyo miradi client ameandikwa ni mzeru.tokea kifo chake kuvuma tokea jana maskari wametanda huko bigwa kwenye hiyo miradi.je kwann hayaaa kuna nn hapa.nahisi kuna mengi nyuma ya pazia na vile familia ya mkuu wa kaya ilionekana ikija kutembelea hiyo miradi.....
 
nitarudi tena ngoja niperuzi data zangu.
Fanya urudi mkuu ukishapitia hizo data,jamaa ilikuwa namrespect sana,taarifa za kifo chake zimenishitua kupita kiasi,hadi sasa akili haichanganyi,nina shauku ya kujua,..ni tukio la kawaida ama? Kwa mtu wa hadhi yake kukumbwa na tukio lile inaonesha ni jinsi gani sisi raia wa kawaida hatuko salama.
 
"Spies may die during their activities (Killed
in Action ). This happens when they try to
steal a Technology and encounter an enemy
Spy doing counter-intelligence, or when
they organize an unsuccessful coup in a
City-State. Killed spies are replaced after a
few turns by new recruits".source: google.
 
Ukitaka ukweli juu ya hili kamuulize inghlonduu wa magogoni atakupa kisa kizima.
R.i.p mzeru.
 
Kazi zao ni hatarishi sana, usifikiri kazi ya kuiweka nchi ya watu zaidi ya millioni 40 kwenye usalama ni kazi ndogo, ni kazi kubwa na ya hatari, wanakumbana na kila aina ya matatizo kwa kuhakikisha kuwa wengi wanabaki salama.

Hao vijana wetu wanakumbana na mengi sana na inabidi tusikitike kwa kuondokewa na mtu anaejitolea maisha yake kutulinda sisi.

Ingawa siwezi kukataa kuwa kuna wengine si waadilifu na hutumia fursa ya kazi zao kujineemesha wao wenyewe au kunyanyasa wengine kwa faida yao (Hii si kwa watu wa usalama tu, wengi sana wako hivyo hata baadhi ya wanasiasa) lakini, kama ijulikanavyo, "kwenye msafara wa mamba, kenge hakosekani".

Hilo swali lako kuhusu nani yuko salama? kumbuka, wewe kwa jina lako nahisi ni Muislaam (ingawa majina si kigezo kamili cha kujuwa dini (njia) ya mtu), kama ni Muislaam (nadhani hata Wakristo) tunaamini kuwa tunaishi kwa amri ya Mwenyeezi Mungu na hakuna mlinzi aliye bora kwetu zaidi ya Mwenyeezi Mungu. Tuzidishe imani.

Inna li Llahi wa Inna ILlahi Rajiun.

"hata wakristo tunaamini"
inamaana umeshasilimu
!??
kadoda11 hebu msome vizuri huyu mfiadini
 
Last edited by a moderator:
He was a mentor to one of the former big brother housemate Hilda Reiffenstein

Mkuu.

Nimeingia kupekuwa kwenye hiyo link nimekutana na haya maneno "...Outside of Africa, her favourite places are Sweden – where she studied – and Denmark, where her father is from. Her mentor, Silvanus Mzeru, is her role model as he told her to be herself and to go for what she wants in life...".

Na kwenye picha nimemuona huyu

hilda.jpg

Ulimaanisha nini na ulitaka kumaanisha nini mkuu?! Kina husiana vipi na kilichotokea kwa afisa husika?!
 
Si ndiyo yule mwenye Chilakale Resort pale mkoani Morogoro?Na Mbena Malumbi ni nani?Hizi habari zinanichanganya sana.So Mzeru Silvanus na Mbena Malumbi ni mtu mmoja.
kuna mmbena malumbi,mmbena malundi na silvanus mzeru hapa tunazungushwa tu lazima kuna mambo nyuma ya pazia majina 3 tofauti lakini tukio ni moja la mauaji.hiyo chilakale ma miradi yote ya majengo pale bigwa moro ni yake kwa niaba ya mkuu wa kaya.tutajua mengi hapa
 
Usalama wa taifa au usalama wa wakubwa wa kisiasa kwenye chama tawala!
 
Mkuu.

Hii nayo kali! Sasa hao usalama wa Taifa kama ndio wenyewe, hawana namna nyingine ya kulinda usalama wa Taifa mpaka wamuue mwana usalama wa Taifa mwenzao?!

Hiyo ipo sana mkuu! TISS agents wengi wameuawa kwa usalama wa taifa
 
Back
Top Bottom