Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?

Mohamed Mtoi huyo jamaa Mzeru ni mtu wa morogoro na inasemekana si Afisa usalama ila alikua anafanya kazi na Riz one kwa wanao mfahamu wanasema alikua anaendesha Hoteli moja iitwayo CHILAKALE hapo moro mjini na kuna Jina lake maarufu ni Mlambena Malumbi sasa kuna habari kuwa hiyo hotel ni ya Riz one na kuna tatizo lilitokea so jamaa wakamuwahi asitoe siri
 
dah,MOROGORO TUMEPATWA NA SIMANZI KUBWA BAADA YA HUYU JAMAA KUUAWA KWANI NI MTU MAARUFU SANA NA PIA NI TAJIRI MKUBWA SANA HAPA MORO NA NIMTU ASIENA MAKUU NA WATU.WENGI WATA MLILIA KWA UMUHIMU WAKE KTK JAMII.INNA LILAHI WA INNALILAHI LAJUNN.
 
Ni watu wa usalama wamemmaliza...Kuna taarifa nyeti nikiwa tayari ntaziweka hapa
kwanza Mkuu anza na kuthibitisha kuwa yule jamaa alikuwa mtu wa UWT........na yule aliyetolewa kwenye mtaro akiwa anahema kwa mbali nae ni nani.........?
 
rest in peace mzeru .ni vigumu kulinda ukweli kwa mtutu ili uwongo usambae kweli itajidhihiri mwisho wa siku
 
Inasikitisha sana polisi wao kazi yao kukamata machinga tu, pale mataa polisi wana kibanda chao lakini hawana msaada wowote.

Ndiyo polissm mkuu.!!!! tena wakati wa tukio inawezekana hawakuwepo ili kusafisha njia.
 
Mohamed Mtoi huyo jamaa Mzeru ni mtu wa morogoro na inasemekana si Afisa usalama ila alikua anafanya kazi na Riz one kwa wanao mfahamu wanasema alikua anaendesha Hoteli moja iitwayo CHILAKALE hapo moro mjini na kuna Jina lake maarufu ni Mlambena Malumbi sasa kuna habari kuwa hiyo hotel ni ya Riz one na kuna tatizo lilitokea so jamaa wakamuwahi asitoe siri

Ukweli ndiyo huu!!! Na wale wanaosimamia zile hotel mbili za bagamoyo wapate fundisho. Wakicheza iko siku nao watawamzeru. Ila kijana ni noma. Aisee bora Beno alikubali yaishe akafanya transfer ya ile nyumba ya kijitonyama iliyonunuliwa kwa jina la Benno.
 
Hivi yule mbunge wa Chalinze alikufa kwa nini vile?...........................

Walusemasema sana kuhusu dogo kuhusika kwa kuwa alikitaka kile kiti. Uzuri hakukanusha popote. Ni mafia huyu.
 
kuna bar kubwa sana Chanika, nilikuwa naijua kwa jina la kwa Mzeru, ni pazuri sana ilikuwa tukienda shamba lazima tupite kupata kuku wa kienyeji na ugali. Nahisi ni yake RIP Mzeru
 
embu tufikirie tofauti unakuta jamaa alikuwa anatoroka na nyaraka nyeti za serikali au either alikuwa anauza nyaraka nyeti za serikali au kaporwa hizo nyaraka nyeti na maofisa wa idara za upelelezi wa nchi jirani so tusibaki kushutumi pikipiki tujaribu kufikiria kiundani zaidi ya kulaumu chombo cha usafiri kilichotumika mkumbuke hii style ya mmauwaji wameshauwawa watu kibao wa usalama wa taifa kwa mtindo huu huu wa kufukuzana barabarani mfano mzuri ni bosi wao wenyewe lt general IMRAN KOMBE, afisa mwandamizi mzee Gibons Mwaikambo na wengine wengi ambao vifo vyao haviandikwi humu all in all TISS @WORK
 
kwa madhara ambayo angesababisha alistahili kufa.ninazo taarifa nyeti za za uhakika
 
kwa madhara ambayo angesababisha alistahili kufa.ninazo taarifa nyeti za za uhakika

Duh! Kaazi kweli kweli! Msione watu wanatetea status quo, their survival depends on it!
 
Mbona wengi mnapapasa mada?!
Tatizo si Pikipiki la hasha!
Kiini cha tatizo ni nini kulikuwa ndani ya briefcase ya yule mwana TISS!?
 
Band practice at the Chilakale Resort.Morogoro , Tanzania
http://geof-frica.tumblr.com/video_file/30124227768/tumblr_m876hxCJsq1rweq79


tumblr_m8745lqM8W1rplnky.jpg

The Chilakale resort in Morogoro, Tanzania
tumblr_m875t4mMoG1rplnky.jpg

The house(s) on the hill. These buildings apparently belonged to the owner of the resort Mr. Silvanus Mzeru, who was supposedly related to the President.
tumblr_m875s5uvvb1rplnky.jpg

The view of the mountain from the Chilakale resort second story in Morogoro Tanzania. As you can see with the construction, they were expanding the resort.
August 2012
 
Mkuu hizo ni baadhi ya mali za Marehemu mjini Morogoro, Tanzania.
 
Yawezekana huyo jamaa kashughulikiwa na wenzie... Hicho kitengo chake ni hatari sana hasa pale unapotishia maslahi ya watu flani. Tunaweza hisi ni majambazi yaliyomuua kumbe ni wenzie. Mungu ailaze roho ya Marehemu Peponi Amen.
 
Back
Top Bottom