Mmoja wa polisi waliouwa afikishwa mahakamani leo

Mmoja wa polisi waliouwa afikishwa mahakamani leo

Da hii kali, ila si itabidi aje apelekwe mahakama kuu kusikilizwa? Of course za kanda? Kesi hii itapigwa dana na itapotea tu!!
 
Kapelekwa mahakamani ili kuzuia wadau mbali mbali wasijadili hi ishu kwa kina.
 
Ila Ndg Kombo, kwanini kusingekuwa na vita hata ya majaribio tu, na nchi yeyote yenye hata kamgogoro na sisi kama vile Malawi, halafu yatumike yale mabomu yaliyoko 977KJ, 303KV, 313KJ,na 39KJ au hata yale ya 971KJ halafu Polisi wawe mstari wa mbele (Front line)? Ma- RPC wote wapewe RPG kwa ajili ya kupima uwezo wao wa kulenga shabaha. IGP awe mstari wa mbele ili kutoa mwangozo aki wa ndani ya BM40,gari lenye uwezo mkubwa kivita, RCO,s wao watumie FFR tena ziwe left hand drive, wasitumie UNIMOG,kwani kiwango cha ajali kitakuwa kikubwa sana. Pia matumizi ya ZIRI na TATA yasiwepo,bali wapewe IVECO za kutosha. Mizinga ya 122 itumike pamoja na MOTOR (mizinga midogo ya kusukumwa na watu sita itumike. Wapewe pia "Flying Objects" za kutosha zinazorushwa na MG rapid response. Jeshi letu la ulinzi (TPDF au JWTZ) liingilie pale tu litakapoona Polisi wamezidiwa.

Ni mtazamo wangu.
 
IGP amepiga kambi iringa kutengeneza ugoro huu kwa maelekezo ya dhaifu ! Huyu atakuwa kashatafutiwa makaratasi na kazi ya ukorokoroni ktk moja ya balozi nje ! Itapotezewa...

RPC na wenzake hawawezi kupona kwa vile mpango huu ulipangwa.....!!

I can smell something fishy here!!!
 
Polisi wasiwe mabaradhuli, kwenye sheria kuna dhana mbiliambazo ilibidi zizingatiwe:

1. Common intention
2. To do or Ommit to do something leading to the commission of the offence

Waendesha mashtaka wangezingatia haya sidhani kama wangempeleka polisi mmoja tu mahakamani.
 
Alyaua ni mmoja tu ambaye alifyatua hilo bomu na wengine wote walikuwa mashuhuda.

Kisheria ukitumia Penal Code ni kosa hata kupiga, ina maana hawa polisi wengine wako sahihi kwa kumpiga Mwangosi?
 
Na wale walioompiga ni mashuhuda pia?


Kama utabahatika japo kidogo kusoma sharia utagundua nini nimekusudia. Kwani siku zote mahakama inatazama lile kosa lililopo mezani. Na kwa mada hii utaona kosa ni mauaji hivyo mshitakiwa atakuwa ni yule tu aliyefyatua Bomu wengine wote sio wauaji. Labda washitakiwe kwa makosa mengine.

Mfano mzuri wa huko Tanzania ni ile kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini (maarufu kama Kesi ya Zombe. Jiulize hukma ilikuwaje?

 
Kisheria ukitumia Penal Code ni kosa hata kupiga, ina maana hawa polisi wengine wako sahihi kwa kumpiga Mwangosi?

Hebu isome vizuri hiyo panel Code na kisha angalia ufafanuzi zaidi katika PGO katika kudhibiti ghasia utajua kila kitu.

Lakin all in all kesi inazungumzia muuwaji na sio mpigaji.

Pitia vizuri na punguza ushabiki pasi na shaka utaelewa

 
Do the State Attorney in charge of Iringa and the Prosecutors know 'the doctrine of common intention?' Under the doctrine all police officers present at the scene when Mwangosi was killed should have been charged for murder and conspiracy to commit an offence ie murder. Even if the 'accused' confessed, all evidences, photos and testimonies of people present show that other police officers were beating Mwangosi shortly before he was killed, in fact the RPC consented as he did not stoped the beating. To let other police officers walk free without charging them even for causing grievous bodily harm is a mockery to the family of the deceased, general public and to the legal profession.
Kaka mnheshimiwa sana msomi wa sheria mimi sio mwanasheria lkini ninaomba tuu nichangie maoni yako kwa upeo wangu finyu.inamaana kama huyo polisi aliyeua hakupewa amri yoyote na mtu yoyote na alikurupuka mwenyewe gafla na hata kumvunja miguu kiongozi wake basi na hao wengine ambao hawakuwa na malise basi na wao waunganishwe tuu kwa sababu walikuwepo eneo la tukio?au hiyo doctine of common intention inamaanisha kwamba ukiwepo tuu eneo la tukio basi umeshiriki kosa hata kama ulikuwa unafanya jitihada za kuzuia kile kilichotokea kama ilivyotokea kwa hoyo kiongozi wao wao ambaye naye alivujwa miguu na bomu hilo na askari wote wakabaki wameshikwa na bumbuwazi wasijue na lakufanya huku wkimlaumu aliyefyatua bomu hilo?.ni mapema mno kujua kilichotokea kwa askari huyo na labda hata sasa hivi ukimuuliza kwa nini alimfyatulia bomu hilo hawezi kueleza vizuri ila anachokijua kuwa alivyatua bomu,labda alipatwa kichaaa cha gafla,labda alishika trigger kwa bahati mbaya,labda alipigwa jiwe akili ikahama gafla, je kama ndivyo basi askari wote waliokuwepo basi waunganishwe kwa sababu kuna doctrine of common intention.let us not be bias to that extent
 
kapelekwa mahakamani ili kuzuia wadau mbali mbali wasijadili hi ishu kwa kina.

utajadili kitu gani kwani muajin alionekana kuanzia siku ya kwanza picha zote zinamuonyesha na amekubali yeye mwenyewe mbele ya polisi mwenzake na mbele ya mlinzi wa amani ambaye sii polisi.sasa tujadili nini wakati kesi iko wazi kabisa au nataka tutengeneze scenario na fact mpya?
 
Mkuu Okaoni, heshima na asante kwa maoni. Mkuu mimi sipo 'bias' nimeelezea kanuni ya 'common intention' inatumikaje ili kuonyesha kuwa askari wote waliokuwa eneo la tukio na kuridhia Mwangosi kupigwa walipaswa kuunganishwa katika shitaka la mauaji. Unaweza pia ukafanya utafiti kidogo tu na ukajua kanuni ya 'common intention' inatumikaje. Kifupi kanuni hii inawatia hatiani wahusika wote wa tukio au kitendo kwa matokeo yote ya uhalifu yaliyotokea wakati wapo pamoja na wakitenda kitendo pamoja. Hapa polisi walikuwa wakimpiga mwandishi wa habari na mmoja wao akalipua bomu na kumuua basi wote wanapaswa kuunganishwa katika shitaka kutokana na kanuni hii. Hii ni kwasababu askari wote hao walijua au walikuwa wazembe kujua kuwa mtuhumiwa aliyefikishwa mahakamani alikuwa na silaha ambayo angeweza kuitumia dhidi ya mwandishi wa habari hata kama wao wenyewe hawakuwa na silaha.


Baada ya kupelekwa mahakamani, askari anaweza kujitetea kuwa yeye alikuwa anazua uhalifu huo. Huyo mshitakiwa kama alipatwa na kichaa ghafla itathibitishwa mahakamani, kumbuka mahakamani inaangaliwa 'legal insanity', normal medical insanity pekee haitoshi kuondoa hatia. Sasa jiulize, Polisi hao hawakujua kuwa kumpiga Mwandishi na matumizi makubwa ya nguvu ni kosa? Je baadhi yao hawakushiriki kumpiga Mwangosi? Je hawakujua kua mmoja wao alikuwa na silaha na angeweza kuitumia wakati huo?
 
Back
Top Bottom