Mnaambiwa Maneno gani hadi mnakubali kufunga kizazi hata kukitoa?

Mnaambiwa Maneno gani hadi mnakubali kufunga kizazi hata kukitoa?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
Salaam,

Kuna watu wenyewe bila kulazimishwa wanaenda Hospitali kutoa kizazi au kukifunga wasizae tena.

Mnaofanya hivyo, Mnaambiwa Maneno gani hadi mnakubali kufunga kizazi hata kukitoa?

Ni akili ya kawaida au changamoto ya akili?

Wanalishwa sumu gani ya maneno hadi wanakubali? Halafu unakuta mtu ana watoto Wawili tu au mmoja.

Na mtu kama huyo bado anaenda Msikitini na Kanisani.

Nini kipo nyuma ya watu kutoa kizazi hata kukifunga?

Nini Siri?
1685598439female-sterilization.jpg

Asilimia 99 ya wanawake nchini walioamua kufunga kizazi walipewa huduma hiyo kwa njia ya upasuaji mkubwa ambao hata hivyo kwa mujibu wa wataalamu wa afya hauruhusu mwanamke kupata tena ujauzito.
 
Mbona unahukumu? Kwa maoni yako wewe si sawa kufunga kizazi japo wizarabyanafya inaruhusu na inatoa muongozo,
Sasa kwa maoni yako wewe
- ni sawa kutumia condom?
-ninsawa kutumia njia za kupanga uzazi?
-ni sawa kupiga mahesabu kwamba "nifanye mapenzi, lakini nisipate mimba?"
-ni sawa kwa mtu mwenyw magonjwa kama Hiv na mengine ambayo yanaihaji uangalizi maalum lasivyo anaweza kumzaa mtoto mwenye shida au kifo?
-ni sawa kufanya mapenzi bila kutarajia
mtoto?
_tendo la ndoa limeletwa ili kufurahia tendo au kuzaa watoto?
Ni sawa kuendelea kuzaa hata kama umetimiza idadi ya watoto uliokusidia?
-"kama hutaki mtoto no sex ever' kwako ni kauli sahihi?
-nini bora kumzaa mtoto ambaye atakuja kuteseka au kutokumzaa kabisa?
 
Kufunga kizazi kwa matatizo au Ugonjwa ni sawa. Ila kifunga uzazi kisa hutaki kuzaa si sawa
 
kwa logic yako mtu asipofunga kizazi lkn akawa na mtoto 1 au 2 ametenda dhambi kama Mkristo au Muislamu? sijaelewa unachomaanisha …
 
Kufunga kizazi kwa matatizo au Ugonjwa ni sawa. Ila kifunga uzazi kisa hutaki kuzaa si sawa
Akizaa hao watoto utamlelea wewe? Kama kapata idadinya watoto anoona anaimudu atoe tu, pia kama haihatij watoto atoe tu kuliko kuja kuleta shida kwa jamii.
 
Akizaa hao watoto utamlelea wewe? Kama kapata idadinya watoto anoona anaimudu atoe tu, pia kama haihatij watoto atoe tu kuliko kuja kuleta shida kwa jamii.
Kwani bila kutoa huwezi kujizuia kuzaa? Naona kama kutoa inatakiwa iwe hatua ya mwisho baada ya zote kushindikana
 
Back
Top Bottom