BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Nimesoma hapa JF kuhusu NHC kununua eneo la urafiki kwa njia ya Mnada kwa Shilingi Bilioni 3, nikahisi labda wamekosea au walimanisha Dola Bilioni 3, nilipoenda kwenye kurasa rasmi za NHC nikakutana na taarifa ileile.
Taarifa ya Ununuzi - NHC yanunua eneo la Urafiki lenye ekari 50 na majengo yaliyopo kwa Shilingi Bilioni Tatu
Ambacho najiuliza huu mnada ambao umeiwezesha NHC kununua ekari 50 maeneo ya Urafiki, eneo lililopo maeneo ya Ubungo kwa gharama ya Bilioni 3 ulifanyika lini? Na wapi?
Pamoja na hivyo ukichukua eneo lote la Urafiki, majengo ya viwanda na makazi na rasilimali zote za hapo, eneo la Ekari 50 lina thamani ya Bilioni 3 kweli? Tena katikati ya Mji mkubwa kama Dar es Salaam!
Hivi wangapi waliomba hiyo tenda hadi NHC wakashinda? Vipi kuhusu Wapangaji waliopo sasa, je, walijulishwa au kupewa nafasi ya wao pia kuomba kununua eneo hilo? Taasisi nyingine pia je zilijulishwa?
Sikuwahi kusikia huu mnada na hata niliouliza watu wangu wa karibu nao ambao najua ni wazee wa mjini wa kufuatilia masuala ya mnada, hawana hizo taarifa za mnada.
Hiki kinachoendelea kina tafakarisha sana, majibu ya kueleweka yanahitajika hapa.