3-Star General
Member
- Feb 21, 2024
- 60
- 137
Utangulizi:
Kumekuwa na changamoto hasa mtu anapotaka kuuza au kununua gari moja kwa moja bila kupitia kwa madalali (middlemen) suala linalosababisha usumbufu kwa muuzaji/mnunuzi kama vile; gari kuchelewa kuuzika kutokana na dalali kuongeza bei huku muuzaji akipewa bei ndogo na/au mnunuzi kuuziwa gari kwa gharama isiyo na uhalisia, kutapeliwa, kuuziwa gari bovu, usumbufu wa kubadili umiliki n.k
Lengo:
Kuanzisha mnada wa hadhara wa magari ya watu binafsi ambao utasimamiwa na kampuni ya minada (Auctioneer). Nimewaza nikafikiri kwamba hii inaweza kuwa fursa nzuri ya kuaddress hizo changamoto na kufanya kazi yenye faida kihalali.
Utekelezaji: A. Maandalizi
Strength:
Mwisho.
Naomba kuwasilisha fursa hii. Mwenye kupata na apate.
Kumekuwa na changamoto hasa mtu anapotaka kuuza au kununua gari moja kwa moja bila kupitia kwa madalali (middlemen) suala linalosababisha usumbufu kwa muuzaji/mnunuzi kama vile; gari kuchelewa kuuzika kutokana na dalali kuongeza bei huku muuzaji akipewa bei ndogo na/au mnunuzi kuuziwa gari kwa gharama isiyo na uhalisia, kutapeliwa, kuuziwa gari bovu, usumbufu wa kubadili umiliki n.k
Lengo:
Kuanzisha mnada wa hadhara wa magari ya watu binafsi ambao utasimamiwa na kampuni ya minada (Auctioneer). Nimewaza nikafikiri kwamba hii inaweza kuwa fursa nzuri ya kuaddress hizo changamoto na kufanya kazi yenye faida kihalali.
Utekelezaji: A. Maandalizi
- Kampuni (Auction company) liyosajiliwa na kutambulika kisheria ambayo itaratibu zoezi zima la mnada.
- Mnada utakuwa wa wazi na Kampuni itaandaa masharti na taratibu zote za mnada kama ilivyo kwa minada mingine japo wanaweza kuiboresha iwe rafiki zaidi kwa muuzaji na mnunuzi.
- Eneo mahususi kama uwanja ambapo mnada utafanyika mara moja au mbili kwa mwezi (mfano siku ya jumamosi). Hivyo eneo litakodishwa kwa siku 4 (Mfano Alhamisi-Jumapili; utaona mbeleni kwa nini siku 4).
- Hapo uwanjani kutakuwa na mobile office na tents kwa ajili ya ukamilishaji wa mikataba/nyakara mbalimbali/process za kubadili umiliki (kutakuwa na wataalam wa sheria na data clerks).
- Mwenye kuhitaji kuuza gari lake atafanya yafuatayo;
- Atalisajili kwenye kampuni (online) kwa kujaza taarifa zote zinazohitajika pamoja na minimum bid value (muuzaji ataweka bei yake anzia).
- Siku mbili kabla ya mnada (mfano alhamis) ataleta gari lake eneo la mnada na atapewa lot no. kisha gari litabaki hapo (eneo litakuwa na taa za kutosha, ulinzi pamoja na cctv surveillance).
- Gari lazima liwe katika hali ya usafi (Huduma hii inaweza kutolewa hapo hapo uwanjani).
- Mnunuzi atafanya haya;
- Anaweza kufika eneo la mnada siku moja au mbili kabla ya mnada (mfano alhamis au ijumaa) kukagua gari au magari anayohitaji.
- Kama yuko mbali au nje ya mkoa anaweza kujisajili mtandaoni kwenye portal ya kampuni kama online bidder na ana option ya kutuma mkaguzi/muwakilishi wake physically (kama atapenda kufanya hivyo).
- Mnada unafunguliwa siku ya jumamosi saa4.00 asb
- Gari kutoka lot moja moja litasogezwa katikati kwenye rotating platform ambayo kila mtu ataliona kirahisi pande zote cz litakuwa linazungushwa na hiyo platform.
- Auctioneer ataanza kwa kutaja sifa na hali ya gari kisha atataja bei anzia iliyowekwa na muuzaji kisha bidders (waliopo mnadani na wa online) wataendeleza mpaka bei kikomo.
- Baada ya kuuzwa gari litarudishwa kwenye lot yake kwa ajili ya kukamilisha taratibu nyingine za malipo na documentations.
- Kampuni itasimamia zoezi zima la malipo kutoka kwa mnunuzi kwenda kwa muuzaji na malipo mengine kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa, commitment na kulinda haki za muuzaji na za mnunuzi.
- Endapo gari halijauzika muuzaji atachukua gari lake na litawekwa kwenye mnada ujao ambapo kabla ya mnada ujao muuzaji anaweza kubadili bei eleekezi kama atapenda kufanya hivyo.
- Zoezi litaendelea kwa lot inayofuata hivyo hivyo mpaka mwisho. Mnada utafungwa saa11.30 jioni Kama kuna lot zitakuwa zimebaki zitasogezwa kwenye mnada ujao na zitakuwa za kwanza kunadiwa.
- Mnada ukifungwa wamiliki wa magari yaliyopewa lot watapaswa kuyaondoa eneo la mnada mpaka kufika kesho yake (mfano Jumapili) saa7 mchana ambapo kambi itavunjwa mpaka mnada ujao.
- Hakuna ada wala kiingilio.
- Baada ya mauzo, muzaji atalipa asilimia tano (5%) ya bei kikomo kwa kampuni; pia kwa kushirikiana na mnunuzi watalipa gharama za TRA.
- Pia kampuni itakuwa na ofisi za kudumu ambapo mtu yeyote anaweza kufika na kusaidiwa hitaji lake.
Strength:
- Zoezi zima litaendeshwa kwa haki na uwazi.
- Muuzaji atauza chombo chake haraka kwa bei anayotaka (kwenye mnada mmoja au zaidi).
- Mnunuzi atanunua chombo kwa bei elekezi. Hata dalali anaweza kununua kwa bei elekezi kabisa akauze kwa bei anayotaka.
- Kampuni itasimamia na kulinda haki za muuzaji na mnunuzi.
- Gari litauzwa kama lilivyo, liwe zima au bovu as long as muuzaji amedeclare na mnunuzi amelikagua na kuridhika nalo.
- Mtu anataka gari ana milioni zake 5-6-10 anaweza pita mnadani akajiokotea kausafiri kazuri tu cha kumsaidia shughuli zake za kujenga Taifa.
- Muuzaji anaweza kutoa taarifa zisizo sahihi kwa kujua ama kutokujua.
- Mnunuzi kushindwa kukamilisha malipo kwa wakati.
- Itamlazimu mnunuzi kwa kiwango kikubwa kufika mnadani jambo ambalo kwa waliopo mbali litakuwa kikwazo kama hana access ya mitandao.
- Changamoto ya Kumfikia Online bidder kuhusu malipo, hawa itabidi wawe na utaratibu tofauti (mfano kulipa % flani ya min bid value kwa kila gari atakalotaka kubid) ambayo nayo inaweza kuwa changamoto.
- Msaada wa kisheria na umilikishaji utatolewa papo hapo hata kama mtu hana ABC za magari atasaidiwa na kampuni.
- Mnada huu ni endelevu kama ilivyo kwa minada ya mifugo na utafungua fursa ya soko la magari used ndani na nje ya nchi.
- Ajira itatengenezwa kwa vijana kabla na wakati wa mnada (mfano staff wa kampuni, vibarua wa kusaidia zoezi, watu wa bima, mafundi-mtu anaweza leta gari akahitaji fundi amuwekee sawa mambo mawili matatu kabla ya mnada, waosha magari-magari yote lazima yawe masafi, mawakala, mama lishe, wauza maji, accessories za magari nk nk).
- Hapa tumegusa maslahi ya watu flani moja kwa moja hivyo ni lazima kuwa na mikakati ya kukabiliana nao.
- Mwamko wa watu, watanzania tuna maisha flani ambayo tumezoea na kutufanya kuwa wazito kunadilika.
Mwisho.
Naomba kuwasilisha fursa hii. Mwenye kupata na apate.