Ligaba
JF-Expert Member
- Oct 12, 2018
- 1,063
- 2,874
Habari kwa wote.
Ni imani yangu JF ni sehemu halisi kwa kila aina maswali yanayosumbua katika jamii. Leo naomba tupeane mbinu za kudhibiti wizi hasa wa mafundi tunaowakabidhi dhamana ya kutujengea.
Kwa muda ambao nimeshughulikia mambo ya ujenzi nimegundua pamoja na ugumu halisia wa kujenga lakini kuna sehemu inachangiwa na mafundi kuanzia msingi na boma, fundi umeme, kupaua, sijui bomba, rangi, yaani kila fundi anayehusika hukugeuza fursa akuongezee cha juu.
Mathalani nimewahi kuongea na rafiki yangu yeye ni mtu wa kupaua ni mbinu gani hutumia kupata cha juu? Alichonijibu ni kuwa watu wengi huibiwa hasa kwa mabati ya vipimo vya viwandani, fundi atakupeleka kwenye kiwanda anachokijua au hata ukimpeleka kiwanda chako ukijaribu kumpa nafasi ya kuongea na mtu wa mauzo umeumia.
Anasema Mara zote huwa wanazidisha idadi za mita na vile watu wengi hawajui hesabu za bati basi zikishakatwa atapata idadi za nyumba yako, idadi aliyozidisha anatumiwa fedha zake kwa simu na hapo huwa ameshakuibia.
Mtu wa umeme nae aliniambia hivyo hivyo, atakununulisha vifaa kibao akipanda dalini anafunga vichache, baadhi ya vile vya thamani alikusudia kuiba atatia kwenye mkoba wake atauza kwa mteja mwingine wakati mwingine.
Watu wa cement nao hivyo hivyo wanakuibia mifuko itauzwa kwa muuzaji wa jumla kwa bei ya hasara.
Je wenzangu mnatumia mbinu gani wakati wa ujenzi kuhakikishia wizi hautokei ktk site yako? Kama mpo mafundi hebu mtusaidie mbinu tofauti mnazotumia kupata cha juu?