Mnaenda katika "nyumba za ibada" zisizo na Ukweli

Mnaenda katika "nyumba za ibada" zisizo na Ukweli

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
1,486
Reaction score
1,874
Ukweli na Uongo Ili uvitambue kwa Urahisi vipe muda tu. Uongo una Tabia ya Kuja kwa Kasi sana na Unapotea kwa Kasi pia. Ila ukweli una tabia ya Kuja Kwa Mwendo wa Taratibu ila Hauna Mwisho wake ukweli utaendelea kuwa Ukweli

Majumba mnayokimbilia ili kwenda kutatua matatizo yenu (kwa waganga, Makanisani n.k) maana kama Kungekuwa na Ukweli huko Msingeenda kila mara maana Mngekuwa mmeshapona

Ukiona Serikali inajenga Mahospitali na Mashule halafu wagonjwa hawapungui wanazidi ongezeka na Ujinga Unazidi ongezeka ujue Hapo serikali hakuna Wanachofanya.

Angalieni jinsi gani Hayo majumba Yanavyojengwa na Yanavyoongezeka halafu hakuna nafuu mnayopata zaidi ya kuzidi kuharibikiwa halafu mnashangaa misukule na Zombie za Diana(Zumaridi) Huko Mwanza. Hamjioni nyie wenyewe ni Misukule yenye Nafuu tu ila Hamjapona kikamilifu

Hivi mlishakaa chini kwa Kutumia Akili Timamu zenu mkajiuliza. Kama Kweli hizo Nyumba Mungu anaishi humo Kama Mnavyodai angeruhusu Majini na Wachawi waje waabudu humo!

Hizo nyumba Kila mkienda Zinatoaga mapepo na Wachawi. Hivi mchawi anaweza kukubali aende Sehemu ambayo ataweza Kutolewa na Kukuta Pingamizi. Hata huo mlango ataweza Usogelea kweli

Ndio mjue ukweli kwamba Mnaenda Katika Sehemu ambazo Makazi ya Hao Viumbe ni humo humo tu na Wala Hamkemei wala Kufukuza Chochote kile huo ndio ukweli ukubali ukatae huo ndio ukweli ndugu yangu hizo nyumba haziwasaidii mnazidi kuharibikiwa. Mungu mwenye Vyote hakai sehemu moja na Viumbe wake.

Eti amekaa na Malaika anawatuma huo ni Uongo mtupu. Hivi mmesahau kwamba kuna Malaika walikuwa wanatumwa Halafu mambo waliyotumwa wakifika Yanagoma. Huko Sodoma na Gomora Watu walionywa ila Wakagoma kuacha Uovu wao. Hivi kwa Akili zako timamu Mungu atume ujumbe wake halafu Wewe ukatae maagizo yake huyo atakuwa Mungu unayemwabudu na Kusema Hakuna Kinachoshindikana Kwake ila Wale watu walimgomea Kubadilika. Eti mwishoni Ndio kawachoma Moto.

Haya Hapo hapo Kawaokoa Watu wake Kutoka Misri miaka Hiyo kupitia Musa kumbuka Wewe kila Siku unaimba Mungu si Mbinafsi na Hamnyimi Yeyote na Anawapenda Binadamu wote ila Hujawahi jiuliza Kwanini Babu zako walipokuwa Utumwani hakuja Kuwaokoa Akaenda Kuwaokoa Watoto wa Hudi (Wayahudi) akawaacha Nyie mpo utumwani Kwa Wajerumani na Waingereza

Kawaokoa Wana Wa Hudi kapasua Bahari wakapita ila Mpaka leo Nchi ya Ahadi hawajawahi Fika na Kula Hizo Asali na Maziwa wamebaki kuwa Kwenye mgogoro na Vita Kila Siku. Kama kweli Mungu mwenye Vyote Angefanya Hivyo si Ndio angemaliza Uovu wote wa Misri angetekeza Ushenzi wote na Dunia Ingekuwa Salama. Ila Ushenzi uliendelea huko Misri.. Ujinga Uliendelea.. Waliabudu masanamu yao mpaka Leo na Mambo mengi tu ya Kishenzi yaliendelea.

Sasa Wewe Mwafrika kwa Sababu hutumii akili Timamu uliyojaliwa na Mungu mwenye Vyote unaletewa ma historia ya Viumbe huko vimepigana kwa Mambo yao unasahau historia Mpka za Mababu zako na Unaitukana Kwa Kuiita Mizimu. Kwanini Usiharibikiwe wewe

Chambueni kila Kinacholetwa mbele yenu si mnapkea tu. Hata Hayati Aliwahasa sana hili swala Mkamuona Kama Vile ni Mtu anayekataa misaada ila Mngekaa kwa Akili zenu timamu Mngegundua jambo Kubwa Lililojificha.


ASANTENI
 
Ujinga wenu nanyi ni mmoja yani huwa mnazichambua imani za hizi dini mnazoita za kuletewa ila linapokuja kwenye hizo imani mnazoita za asili yetu huwa mnataka tuzikubali tu kisa ni za mababu zetu hivyo ni asili yetu, mkishafika hapo tu huwa naona ni walewale tu wawamba ngoma mnavutia upande upande wenu ila hakuna jipya.
 
MKUU KWA HIYO TUENDELEE NA MIZIMU YETU
Naunga hoja mkuu.

Hawa kina St. Andrews, St. Michael, St. Valentine etc na wenyewe ni mizimu ya wazungu.

Kwanini tusiombe kwa mizimu yetu wenyewe tunang'ang'ania Mtakatifu Rita uniombee sijui mtakatifu nani huko.

Yaani unamuomba mtu ambaye hata hakujui na wala sio wa asili yako akuombeee, huo ni uduwanzi wa hali ya juu sana.
 
Afrika kwa ujumla tuna changamoto sana, haswa hili swala la dini na imani hizi tulizo nazo.

Nafsi ni kama zinatusuta hivi na kila upande kuendelea kuamini au kuendelea kutokuamini.
 
Sijaona ulichoandika!!
Ila nitakuuliza swali moja tu...
Je Unaamini kuwa Mungu Yupo?
Nijibu hilo
 
Naunga hoja mkuu.
Hawa kina St.Andrews, St. Michael, St. Valentine etc na wenyewe ni mizimu ya wazungu.
Kwanini tusiombe kwa mizimu yetu wenyewe tunang'ang'ania Mtakatifu Rita uniombee sijui mtakatifu nani huko.

Yaani unamuomba mtu ambaye hata hakujui na wala sio wa asili yako akuombeee, huo ni uduwanzi wa hali ya juu sana.
kweli kiongozi aisee
 
Kwamba kila jamii au bara ina mizimu yake kwamba waafrika tuna mizimu yetu, wazungu wana mizimu yao, wahindi yao,waarabu yao,wachina yao n.k Sasa ikiwa mtoto amezaliwa na wazazi wa jamii mbili tofauti hapo inakuaje au ndiyo anaweza kutumia mizimu yote?
 
Uliahirisha kukata tamaa mkuu ukaamua uanze kukosoa jamii na imani zao kisa mapesa yamekukataa.


Unahitaji akili ya ziada ili kuielewa jamii kwa nini iko kama ilivyo.
 
MKUU KWA HIYO TUENDELEE NA MIZIMU YETU
Kwani Huko Hakuna Mizimu mkuu. Si mnaiita Watakatifu. Mtu akifa Na Wewe ukawa bado unamtaja Taja Jua Unaiita hiyo Mizimu ije ikusikilize

Si kila Mzimu ni Mwema mpka Ujue Unachofanya
 
Back
Top Bottom