Mnaenda katika "nyumba za ibada" zisizo na Ukweli

Mnaenda katika "nyumba za ibada" zisizo na Ukweli

Uliahirisha kukata tamaa mkuu ukaamua uanze kukosoa jamii na imani zao kisa mapesa yamekukataa.


Unahitaji akili ya ziada ili kuielewa jamii kwa nini iko kama ilivyo.
Ingia Kwenye hoja Hali ya Uchumi wa Mtu Ambaye Humuoni Wala Humjui unaizungumziaje. Wewe si ndio utaonekana Hamnazo. Unaacha Hoja Unakimbilia Hali za Uchumi na Kukata Tamaa

Mada Hiyo hapo Juu. Si kila Anayekwenda tofauti na Wewe Ana Hali mbaya Ya Uchumi wengi wamekuzidi Sana Tu na Wanahoji Vitu vikubwa Wewe si Umekaririshwa Tu maan Huna Ukweli ndani Yako ndio maana Mnakasirika Mkiulizwa Maswali
 
Ukweli na Uongo Ili uvitambue kwa Urahisi vipe muda tu. Uongo una Tabia ya Kuja kwa Kasi sana na Unapotea kwa Kasi pia. Ila ukweli una tabia ya Kuja Kwa Mwendo wa Taratibu ila Hauna Mwisho wake ukweli utaendelea kuwa Ukweli

Majumba mnayokimbilia ili kwenda kutatua matatizo yenu (kwa waganga, Makanisani n.k) maana kama Kungekuwa na Ukweli huko Msingeenda kila mara maana Mngekuwa mmeshapona

Ukiona Serikali inajenga Mahospitali na Mashule halafu wagonjwa hawapungui wanazidi ongezeka na Ujinga Unazidi ongezeka ujue Hapo serikali hakuna Wanachofanya.

Angalieni jinsi gani Hayo majumba Yanavyojengwa na Yanavyoongezeka halafu hakuna nafuu mnayopata zaidi ya kuzidi kuharibikiwa halafu mnashangaa misukule na Zombie za Diana(Zumaridi) Huko Mwanza. Hamjioni nyie wenyewe ni Misukule yenye Nafuu tu ila Hamjapona kikamilifu

Hivi mlishakaa chini kwa Kutumia Akili Timamu zenu mkajiuliza. Kama Kweli hizo Nyumba Mungu anaishi humo Kama Mnavyodai angeruhusu Majini na Wachawi waje waabudu humo!

Hizo nyumba Kila mkienda Zinatoaga mapepo na Wachawi. Hivi mchawi anaweza kukubali aende Sehemu ambayo ataweza Kutolewa na Kukuta Pingamizi. Hata huo mlango ataweza Usogelea kweli

Ndio mjue ukweli kwamba Mnaenda Katika Sehemu ambazo Makazi ya Hao Viumbe ni humo humo tu na Wala Hamkemei wala Kufukuza Chochote kile huo ndio ukweli ukubali ukatae huo ndio ukweli ndugu yangu hizo nyumba haziwasaidii mnazidi kuharibikiwa. Mungu mwenye Vyote hakai sehemu moja na Viumbe wake.

Eti amekaa na Malaika anawatuma huo ni Uongo mtupu. Hivi mmesahau kwamba kuna Malaika walikuwa wanatumwa Halafu mambo waliyotumwa wakifika Yanagoma. Huko Sodoma na Gomora Watu walionywa ila Wakagoma kuacha Uovu wao. Hivi kwa Akili zako timamu Mungu atume ujumbe wake halafu Wewe ukatae maagizo yake huyo atakuwa Mungu unayemwabudu na Kusema Hakuna Kinachoshindikana Kwake ila Wale watu walimgomea Kubadilika. Eti mwishoni Ndio kawachoma Moto.

Haya Hapo hapo Kawaokoa Watu wake Kutoka Misri miaka Hiyo kupitia Musa kumbuka Wewe kila Siku unaimba Mungu si Mbinafsi na Hamnyimi Yeyote na Anawapenda Binadamu wote ila Hujawahi jiuliza Kwanini Babu zako walipokuwa Utumwani hakuja Kuwaokoa Akaenda Kuwaokoa Watoto wa Hudi (Wayahudi) akawaacha Nyie mpo utumwani Kwa Wajerumani na Waingereza

Kawaokoa Wana Wa Hudi kapasua Bahari wakapita ila Mpaka leo Nchi ya Ahadi hawajawahi Fika na Kula Hizo Asali na Maziwa wamebaki kuwa Kwenye mgogoro na Vita Kila Siku. Kama kweli Mungu mwenye Vyote Angefanya Hivyo si Ndio angemaliza Uovu wote wa Misri angetekeza Ushenzi wote na Dunia Ingekuwa Salama. Ila Ushenzi uliendelea huko Misri.. Ujinga Uliendelea.. Waliabudu masanamu yao mpaka Leo na Mambo mengi tu ya Kishenzi yaliendelea.

Sasa Wewe Mwafrika kwa Sababu hutumii akili Timamu uliyojaliwa na Mungu mwenye Vyote unaletewa ma historia ya Viumbe huko vimepigana kwa Mambo yao unasahau historia Mpka za Mababu zako na Unaitukana Kwa Kuiita Mizimu. Kwanini Usiharibikiwe wewe

Chambueni kila Kinacholetwa mbele yenu si mnapkea tu. Hata Hayati Aliwahasa sana hili swala Mkamuona Kama Vile ni Mtu anayekataa misaada ila Mngekaa kwa Akili zenu timamu Mngegundua jambo Kubwa Lililojificha.


ASANTENI

Wewe ni special case Kama zumaridi na nabii Tito.
 
Wewe si uko kuzimu makanisa yanakunyima usingizi
Yananinyimaje usingizi Ndugu yangu. Mie Ukweli naujua huko hakuna ukweli ndio maana mnaambiwa Sadaka ni za Mungu na nyie mnakubali wakati watu wanaenda kufanyia miradi yao na kununua Majumba ya kifahari
 
Yananinyimaje usingizi Ndugu yangu. Mie Ukweli naujua huko hakuna ukweli ndio maana mnaambiwa Sadaka ni za Mungu na nyie mnakubali wakati watu wanaenda kufanyia miradi yao na kununua Majumba ya kifahari
Yanakunyima usingizi kwa sababu matarajio yako kwa Kanisa yameshindwa unabaki kupiga kelele ambazo hazina maana.
 
Yanakunyima usingizi kwa sababu matarajio yako kwa Kanisa yameshindwa unabaki kupiga kelele ambazo hazina maana.
Kukuuambia kwamba Sadaka Zako huwa Haziendi kwa Mungu ndio Unasema Matarajio yangu hayajatimia. Huo ndio Ukweli huko Mlipo hakuna Ukweli wowote ule mnapumbazwa Sana
 
Kukuuambia kwamba Sadaka Zako huwa Haziendi kwa Mungu ndio Unasema Matarajio yangu hayajatimia. Huo ndio Ukweli huko Mlipo hakuna Ukweli wowote ule mnapumbazwa Sana
Kwani sadaka umeziona makanisani tu,je misikitini hakuna sadaka,je kwenye mahekalu hakuna sadaka je kwa mizimu hawatoi sadaka mbona unaumizwa na sadaka za makanisani?
 
Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
MTU MZIMA NA AKILI ZAKO NA MAPUPU KABISA UNAMWITA MWANAMKE MFALME ETI MUNGU.
MBWA WEWE HUFAI KUISHI , UNAMALIZA OXYGEN YA BURE
 
Kwani sadaka umeziona makanisani tu,je misikitini hakuna sadaka,je kwenye mahekalu hakuna sadaka je kwa mizimu hawatoi sadaka mbona unaumizwa na sadaka za makanisani?
Tatizo Siyo Sadaka hizo Sadaka Zinafanyiwa Nini! Sijakukataza Kutoa sadaka wewe katoe tu Ila Ushauri wangu kwako Katoe Sadaka Kwa Binadamu wenzako Maana Hao ndio wanahitaji mahitaji muhimu ya Maisha, Mungu hana Upungufu huo mpaka Eti umpe Sadaka na Shukrani

Kumpelekea Sadaka Mtu anayeenda Kujenga Kwao, Kujenga Miradi,Kujenga Mashule amabyi hata Ww kama Muumini huwezi Peleka mtoto wako na Uliijenga Kwa. MICHANGO yako huo Ni Upungufu wa Akili uliopitiliza.

Ila Kma Wewe ni Mchungaji Endelea Kuwapiga Tu mpaka akili zao zitakapofunguka
 
Back
Top Bottom