Mnahonga mnapopenda au kuna kitu mnataka?

sasa zawadi si hadi ufanyiwe kitu cha kukufurahisha! Au unatoa tu hivi hivi?

kwako wewe Husninyo huna haja ya hayo yote, kwako ninakupa tu zawadi bila masharti!
 
we paka sidhani kama mwanaume akiwa anasaidia familia yake tutasema anahonga. Mwanamke nae akiwa anakuhonga lazima wanaume mjifikiri mara 2 mbili.



Naona kama hujanielewa mama hiyo ya familia nimeweka kama mfano tu,ila point ni kuwa mwanaume kuhonga ni wajibu na vilevile iko katika nature maana hata wanyama nao huwa wanahonga.
 
Fidel80, kumbuka hongo ni kama subset ya Rushwa!!!!!!!

Ndo maana nasema sheria iangalie hili unajua unaweza ukawa unafukuzia binti mkawa ligi moja na mtoto wa Bakharesa ukashangaa anatumia mkwanja sana ukiwa kama hongo ili imradi tu ampate huyo binti na wewe mtoto wa mkulima ndo umejipinda hapo hapo wewe unamwaga sera yule anamwaga mkwanja inabidi sheria itazame hii rushwa ya kutongoza mtu anatumia pesa kwa kumhonga mwanamke amkubalie
 
Naona kama hujanielewa mama hiyo ya familia nimeweka kama mfano tu,ila point ni kuwa mwanaume kuhonga ni wajibu na vilevile iko katika nature maana hata wanyama nao huwa wanahonga.

hapo nimekuelewa paka. Ila sikujua kama hadi wanyama nao wanahonga.
 

fidel mbona umeongea kwa msisitizo sana? Yamekukuta nini?
Mwenye kisu kikali ndio atakula nyama hata sheria ikiwepo.
 
Duh jogoo nae ama honga duh!

Mkuu tunaomba bunge lipishe mswada wa watu wanaotongoza kwa kuhonga

jogoo ni kuku na kuku ni ndege sio mnyama. Au sio wana biolojia?
Hadi paka wanahonga! Lol!
 
Mapenzi si pesa ingawa pesa ina nafasi kubwa katika mapenzi.
Hivi mnapokuwa mnahonga pesa, nyumba, simu, magari etc huwa mmependa na unaonesha kuwa unajali au unafanya hivyo ili upewe utamu?
hata mimi huwa hili linanichanganya kwakuwa kama binadamu wote wanahitaji mapenzi kwa maana ya mwanamume na mwanamke, sasa kwanini wanaume wanatumia sana materials kuwapata wanawake?

This is very challenging and disturbing

Mapenzi ni pesa au upendo?
Upendo ni pesa au amani?
Pesa bila upendo?

Na ndio maana siku hizi hakuna mapenzi ya dhati maana pesa zinapitishwa mbele kama kigezo kikubwa

Prove me wrong
 
Me nahonga kuokoa muda na kurahisisha zoezi, maana ile kwamba nakupenda kama ulivyo, na hata chini tutalala me siiamini katika majira ya sasa! nimekuwa addicted mpaka nikiwa na demu nisipomuhonga najiskia vibaya! sema inanisaidia maana nikimuhitaji anakuja bila malalamiko na kwa haraka.
 
pesa ni roho . ukichukua chapaa yangu ni umechukua roho yangu, kunikataa ni ngumu sana . lazima nikutafune
 
mimi huwa sihongi!
natoa zawadi tu!

Nilitaka kuuliza hivi ni kuhonga au kutoa zawadi? Mnaweza mkawa na tabia za kupeana zawadi mbali mbali kama Wapenzi. Hili neno la "kuhonga" naona halijakaa sawa. "Kuhonga" naona kama linafaa kutumika kwa changudoa lakini kwa mpenzi si neno sahihi. Ni maoni tu.
 
ni tamaa tu kujionyesha kuna pesa mwanamme akiwa hajui ktongoza
 
Mwanaume kamili hatoi hela kwa demu mpaka amemjua kwanza, huyo ndo wale wenye allegy na kutongoza ama domo zege, anajaribu kutumia alichonacho ili kuandaa mazingira siku ya kuomba game asitumie maneno mengi
 
Mapenzi si pesa ingawa pesa ina nafasi kubwa katika mapenzi.
Hivi mnapokuwa mnahonga pesa, nyumba, simu, magari etc huwa mmependa na unaonesha kuwa unajali au unafanya hivyo ili upewe utamu?

Kikubwa ni utamu tu hayomengine ninyinyi mna yaanzisha; Dear ona simu yangu, nimeishiwa pesa, nimechoka kupanda 5/5, ninunulie vitz. Sasa unategemea minifanye nini na hela ipo....:hungry:
 
ni tamaa tu kujionyesha kuna pesa mwanamme akiwa hajui ktongoza

Tamaa sawa. Hela ipo maneno mengi ya nii?.... Hata asiye na hela anajitahidi kuremba maneno, the same tamaa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…