Mnaishije na mabosi wenu jamani???

Assignment na maagizo yote anatoa kwa e mail au kimemo na hataki maswali au ufafanuzi wowote. Sasa hapo kazi itaenda kweli??.
Ukimfata oficn anakupa maelezo huku anaendelea kutazama computer yake as if u r rabbish. Ana maudhi kwa kweli. Dunia hii....


Ingia ofisini kwake, funga mlango kwa funguo, then mchape makofi!
 

Pole mkuu kwa masahibu, definetly hakuna komandoo wa matatizo but the prescription for your problem is (try to lie with him/her while you dress in a positive thought, jaribu kuwa na mtazamo chanya mzee!!!!!!!!)
 

Pole mkuu kwa masahibu, definetly hakuna komandoo wa matatizo but the prescription for your problem is (try to lie with him/her while you dress in a positive thought, jaribu kuwa na mtazamo chanya mzee!!!!!!!!)
 
Kuna dhana moja ambayo Prof Drucker(Marehemu) aliandika katika moja ya vitabu vyake lukuki vya management (bahati mbaya ni siku nyingi sikikumbuki) na nimeitumia kwa takriban miaka 10 +kwa mafanikio si haba; nahisi inaweza kusaidia. Anasema kuwa siku zote "jitahidi umjue bosi wako kwa undani ili ujue jinsi ya kum-manage". Kuna watu ukimwona asubuhi alivyokuja, unajua fika leo si hata wa kumsalimia, siku nyingine utaona kaamka vizuri, hiyo ndio siku ya wewe kuomba mkutano naye etc,. Hakuna bosi aliye kamili, utaondoka hapo utaenda kwingine mpaka utajuta na kumkumbuka huyo UNLESS uwe umefanya utafiti wa uhakika huko uendako.
 
Kaka Leornardo,

Hapa ni swala la Psychology tu. Unaweza ukacheza na psychology ya huyo bosi wako na hata ukashangaa akabadilika haraka sana. Ukisoma kitu kinaitwa Manageria Leadership hapa ndipo unaweza ukajua haya yote.

Ni kawaida kabisa haswa kwa sisi waafrika tunapopata vyeo kupenda kuabudiwa, kuogopwa, kuamrisha, kujionyesha mbele za watu na kuona kwamba sheria haziwagusi wao kama viongozi.

Sasa kwako wewe unachoweza kufanya ni kitu kidogo sana, kwanza jinyeyekeze kwake kwa kufanya ajione yeye yupo juu yako na yeye ndio bosi wako. Pili, jaribu kufuata yale anayoyataka yeye na hata kama yuko wrong basi jitahidi kumuelewesha kwa utaratibu (huku ukimsifia sifia).
Tatu, jaribu kuwa unampa feedback za kumsifia, kuonyesha kwamba yeye ni bora na anaweza zaidi na ikibidi kumuonyesha kwamba unamfurahia, be positive kila unapokua nae, msifie, ongea nae kwa kumsifia mara kwa mara. Mwisho jaribu kuwa nae karibu kwa kumpa feedback ya kila unachokifanya na sometimes uwe unaomba ushauri wake kwa mambo madogomadogo ili tu umuweke karibu.

Ukiweza kuyafanya hayo wewe mwenyewe utaona mabadiliko yake. Ni kawaida kwa sisi binadamu kuwapenda sana watu wanao tusifia na kuridhika na tunachokifanya (apreciation)
 

Nashukuru bro kwa ushauri, ni ngumu lakini utafanyaje? ushauri niliopewa humu JF umenisaidia kwa kweli na angalau kunipa moyo kuwa mabosi wa aina hii wapo kila mahali. Jamaa kaenda kwao likizo ya sikukuu wiki mbili so tunapumua kidogo.
 
Ingia ofisini kwake, funga mlango kwa funguo, then mchape makofi!
Mmmh! hapana ila unaweza ku-argue naye kwa kumueleza masuala ambayo hukubaliani nayo kabisa, husitake sana kutishika, lakini pia lazima kuwa makini kwa ushauri wowote utakaouchukua hapa
 

ha ha ha! We elli hayo maneno unataka mwenzio balaa liongezeke.
 

Haya yanatukuta vijana wengi makazini kwa sababu hawa wazee wanaogopa kuzidiwa na vijana na kunyang'anywa nafasi zao vivyo wanajaribu kwa kila njia kuwafrastrate ili ikiwezekana waache kazi. Vijana wakiacha kazi wao huwaambia wakubwa zao kwamba kazi ni ngumu vijana hawawezi. Uwe mvumilivu kama maslahi ni mazuri fanya kazi yako hata report ikirudishwa si unapata maelekezo wapi pa kuirekebisha fanya atakavyo yeye. Kumbuka kila lenye mwanzo huwa na mwisho. Pia kumbuka kuhifadhi vizuri pesa yako upatayo ili miaka ijayo ujiajiri na kuajiri pia. Siku njema
 
Chapa kazi kama huna akili nzuri, akikufokea chapa kazi tu, akinuna chapa kazi tu, akitukana wewe tabasamu chapa kazi tu, asipokusemesha wewe msemeshe hata kama atanyamaza wewe mwache chapa kazi tu, Asipokuja kazini usikasirike chapa kazi tu, Akikuachia ofisi kubali chapa kazi tu, Akimwachia mwingine ofisi usichukie chapa kazi tu, Akiongeza mshahara ongea naye kwa upole chapa kazi tu

NAKUAMBIA UKIFANYA HIVYO KUNA SIKU ATAKUKUBALI TU
 
Vumilia huku ukitafuta kazi ingine chukua day off ukijua una interview na usiseme kwa mtu yoyote anyehusiana na ofisi hiyo mipango yako. ukipata kwingine pesa same au zaidi then uende ukifanya interview sema muda unahitaji wa kutoa notice, na ukiwa ofisini sasa chunguza au soma contract YAKO UNAHIYAJI KUTOA NOTICE YA KUACHA MUDA GANI KABLA?

good luck,

inabidi mtu uwe na furaha asubuhi uendapo job
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…