Kaka Leornardo,
Hapa ni swala la Psychology tu. Unaweza ukacheza na psychology ya huyo bosi wako na hata ukashangaa akabadilika haraka sana. Ukisoma kitu kinaitwa Manageria Leadership hapa ndipo unaweza ukajua haya yote.
Ni kawaida kabisa haswa kwa sisi waafrika tunapopata vyeo kupenda kuabudiwa, kuogopwa, kuamrisha, kujionyesha mbele za watu na kuona kwamba sheria haziwagusi wao kama viongozi.
Sasa kwako wewe unachoweza kufanya ni kitu kidogo sana, kwanza jinyeyekeze kwake kwa kufanya ajione yeye yupo juu yako na yeye ndio bosi wako. Pili, jaribu kufuata yale anayoyataka yeye na hata kama yuko wrong basi jitahidi kumuelewesha kwa utaratibu (huku ukimsifia sifia).
Tatu, jaribu kuwa unampa feedback za kumsifia, kuonyesha kwamba yeye ni bora na anaweza zaidi na ikibidi kumuonyesha kwamba unamfurahia, be positive kila unapokua nae, msifie, ongea nae kwa kumsifia mara kwa mara. Mwisho jaribu kuwa nae karibu kwa kumpa feedback ya kila unachokifanya na sometimes uwe unaomba ushauri wake kwa mambo madogomadogo ili tu umuweke karibu.
Ukiweza kuyafanya hayo wewe mwenyewe utaona mabadiliko yake. Ni kawaida kwa sisi binadamu kuwapenda sana watu wanao tusifia na kuridhika na tunachokifanya (apreciation)