Uchumi unahitaji usimamizi Mzuri, siyo kupiga siasa siasa. Nilitembelea Zimbabwe mwaka 1990 nikakuta maisha mazuri sana kulinganisha na Tanzania ingawa watu walikuwa wanaanza kulalamika. Nilikuwa nabadilisha USS1 kwa Zim$ 5 na wala watu walikuwa hawana papara na pesa za nje; dereva wa Taxi aliyenitoa airport alinipeleka benki kwanza Standard Charted Bank (wakati huo haijafika Tanzania) kubadilisha Traveller's Cheques zangu ili nimlipe katika Zim-Dollar ingawa nilikuwa na USD-Cash pia.
Miaka 9 baadaye mwaka 1999 nilikwenda tena Zimbabwe nikitokea Marekani nikashangaa hiyo Zimbabwe niliyokuta. Yale mabarabara mapana ya Julius Nyerere way yalikuwa ni mashimo mashimo, US$1 ulikuwa unapata zaidi Zim$5000 wakati huo na zilikuwa hazinunui chochote. Wakati huo Mugabe akiwa anahangaika na siasa dhid ya vyama vya upijnzani tu na kupora mashamba ya weupe ili apate cheap politics