Mnamuonea sana Karia, ligi zetu ni bora kuliko za Misri na Algeria

nzagambadume

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2018
Posts
2,430
Reaction score
5,779
Kuna watu wakiongelea ligi yetu gape la mechi la kulinganisha na ligi ya uingereza unaweza ukadhani karia ni shetani aliyeandikwa kwenye vitabu vya dini..angalia ligi ya misri wana teams kama sisi wanatakiwa kila teams icheze mechi 34 angalia ndo kwanza al ahly ana mechi 19 ,pyramids ana mechi 22 bado kombe lao la FA halijaisha ukimaliza angalia ligi ya algeria wanatakiwa wacheze mechi 38 kila teams ndo kwanza teams nyingi zimecheza mechi 25.

Tusisahau kwenye msiba wa kitaifa wa JPM ligi ilisimama karibu siku 23 na wave ya kwanza ya corona waziri mkuu alisimamisha michezo sijui ilidumu weeks tatu pia?

egypt.PNG
algeria.PNG
 
Karia ni Raisi wa TFF aliyepata mafanikio kupita Maraisi wote waliomtangulia.
Tatizo la Karia ni kwamba Yanga hawajachukua ubingwa kwa miaka minne.
Kwamba baada ya kuangalia makosa yao kama yao.
Wanamdondoshea zigo la lawama Karia.
Yaani wanamsajiri Yikpe, akishindwa kufunga goli, lawama kwa Karia.
Wanataka Karia awafungie Magoli, si ndo wamemsajiri.

Timu ina NUSU ya magoli ya Simba, analaumiwa Karia.

Yanga Fikirieni,
Kaja Kocha mkamtibua, akawaita Manyani.
Kaja Morrisson, Karinyo na sasa Lamine kawakimbia.
Metacha kawasalimia juzi tu.

Lawama anapewa Karia.

Timu ya Yanga ni mojawapo ya
Seven Wonders of The Planet.
 
Achana na masuala ya Algeria lazma wadau tuipambanie ligi yetu iwe bora usijipe moyo kwamba yawezekana bakhresa na wewe mpo sawa ki pesa kisa wote mlipitisha mchana bila kula
 
Tatizo sio kalenda
tatizo nini?angalia ligi ya misri halafu njoo na utetezi wako
Achana na masuala ya Algeria lazma wadau tuipambanie ligi yetu iwe bora usijipe moyo kwamba yawezekana bakhresa na wewe mpo sawa ki pesa kisa wote mlipitisha mchana bila kula
kwa taarifa yako wanaomsema vibaya karia wanakuambia hakuna ligi ambayo haijaisha duniani ni tanzania tu tena huku wakihusisha viporo vya simba ambyo yeye na yanga wana gape la mechi 3 tena wakiongea unaweza dhani ligi zooote zimekwisha je yangekuwa kama ya misri na algeria ingekuwaje? al ahly bado mechi 15 amalize ligi
 
tatizo nini?angalia ligi ya misri halafu njoo na utetezi wako

kwa taarifa yako wanaomsema vibaya karia wanakuambia hakuna ligi ambayo haijaisha duniani ni tanzania tu tena huku wakihusisha viporo vya simba ambyo yeye na yanga wana gape la mechi 3 tena wakiongea unaweza dhani ligi zooote zimekwisha je yangekuwa kama ya misri na algeria ingekuwaje? al ahly bado mechi 15 amalize ligi
Katika kufuatilia kwako kote ligi yetu kweli ilikosa mda wa kumalizika mpk mda huu?
Na sababu gani haswa ya msingi inayopelekea ligi yetu isiishe mpk sasa?
 
nashauri viongozi wa yanga kamwe wasije wakaachia hili chaka la lawama kwa karia na tff ,shikilieni hapohapo hata hiyo mitambo ya magoli inayokuja msimu huu ikichemsha(which they will)kamwe msikubali makosa LAWAMA ZIENDE KWA KARIA NA TFF
 
Al Ahly walianza na mashindano ya vilabu ya dunia wakati lig yao inaendelea, Simba Kuna kipindi timu inakaa wiki mbili haijacheza Ligi eti unapewa nafasi ya kujiandaa na mechi za kimataifa.
 
Karia haimuhusu hili kuna bodi ya league ndio kazi yao sio TFF kupanga ratiba kitu ambacho siungi mkono kuangalia league ya Misri kama kigezo cha sisi kutokuwa bora tujifunze league bora duniani hata kama sio duniani basi Africa hapo SA tu professional league na walikuwa na wawakilishi wengi tu Africa lakini hakuna upuuzi huu tujifunze kwa waliobora sio kukimbilia Misri.
 
okay na msiba wa jpm je?kombe la dunia halikuchukua hata siku 10...vipi pyramids mbona wao wamecheza mechi 22 wakati zamaleki ana 26?au kwa sabababu alikuwa shirikisho? simba na namungo wana gap ya mechi ngapi?si 3? mmezidi bwanaa kha
 
nashauri viongozi wa yanga kamwe wasije wakaachia hili chaka la lawama kwa karia na tff ,shikilieni hapohapo hata hiyo mitambo ya magoli inayokuja msimu huu ikichemsha(which they will)kamwe msikubali makosa LAWAMA ZIENDE KWA KARIA NA TFF
Mbon unasema vitu tofauti na mada huna hoja huna majibu...haijalishi nani bingwa hakuna sababu ya ligi yetu kuwa bado haijaisha mpk sasa
 
Karia haimuhusu hili kuna bodi ya league ndio kazi yao sio TFF kupanga ratiba kitu ambacho siungi mkono kuangalia league ya Misri kama kigezo cha sisi kutokuwa bora tujifunze league bora duniani hata kama sio duniani basi Africa hapo SA tu professional league na walikuwa na wawakilishi wengi tu Africa lakini hakuna upuuzi huu tujifunze kwa waliobora sio kukimbilia Misri.
kama ni ubora wa ligi tangu karia aingie madarakani Tanzania mara mbili imeingiza teams 4 mashindano ya CAf na ipo ranked namba 12 na Caf ni ubora gani mnasemea ?kwa hiyo misri siyo ligi ya kujilinganisha nao?tumewazidi siyo kwamba siyo level yetu?
 
Mbon unasema vitu tofauti na mada huna hoja huna majibu...haijalishi nani bingwa hakuna sababu ya ligi yetu kuwa bado haijaisha mpk sasa
nawakumbusha tu hii ligi tayari bingwa ni simba sema haijulikani nani atakuwa wa pili...kuna mitambo ya yanga itaanza kushuka soon na kupokelewa airport ikishaanza kuchemsha karia anatupiwa zigo la mavi
 
Katika kufuatilia kwako kote ligi yetu kweli ilikosa mda wa kumalizika mpk mda huu?
Na sababu gani haswa ya msingi inayopelekea ligi yetu isiishe mpk sasa?
Wakati wa msiba wa rais Magufuli ligi lilisimama zaidi ya siku 23.amabazo ni zaidi ya mechi 4. Katika hizo siku.
 
kabisa unaona hata zambia msiba wa kaunda wamekataza starehe ila ligi wameruhusu iendelee kwa sharti kwamba goili likifungwa hamna kushangilia maana siku 21 ni nyingi mno mechi kama 4 zilipotea hapo
 
Basi msajirini Karia awafungie magoli.
Mlipo ongoza ligi, Karia hakutajwa.
Mlikuwa na misemo yenu tu.
Yanga Unbitten
Mabingwa wa kihistoria
Dar Yang Afrikans
Nyuma Mwiko, mbele daima.

Toka Mfungwe na Coast Union mkaanza kumtupia lawama Karia.

Simba imefungwa mechi mbili, na Ruvu shoting, na Prison.

Hii ilikuwa fulsa kwenu, mshinde mechi zenu zote, muwe mabingwa.

Mkafungwa tena na Azamu, (prince dube)
Lawama mnamuangushia Karia.

Yanga mjitafakari, ninyi ndio wenye mapungufu.

Karia kawanyima goli lipi ?
Na kawapa Simba goli lipi ?
 
Wakati wa msiba wa rais Magufuli ligi lilisimama zaidi ya siku 23.amabazo ni zaidi ya mechi 4. Katika hizo siku.
Yaani kama Karia atasema hiyo ndo sababu ya kutokuisha ligi mpk sasa basi cheo hakimfai kile mtafutieni kazi kama vp mkabeti nae huko..
 
Back
Top Bottom