TheForgotten Genious
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 2,087
- 3,156
Kijana amepata mke mzuri,na shape mashallah,lakini nimwendo wa makofi,mangumi na mateke,faida ni gani?.
Kilele cha udhaifu wa mwanaume yeyote Duniani ni kupiga mke,unabamiza makofi mtoto wa watu na bado anakuzalia na unapewa yote kama dozi ya hypertension,huu ni ujinga.
Nimebahatika kukutana na Na Zainabu yule dada aliyekatwa na panga Kinondoni mkwajuni na aliyekuwa mume wake,dah inasikitisha sana.
Umekuja kupata huduma ofisini kwangu,nikamuandikia vidonge akasema hawezi kumeza,nika badili sindano Za mshipa,wakati na trace mishipa nikamwambia kunja ngumi akasema siwezi na mikononi ana makovu kibao ,hawezi kukunja kiganga wala kuchezesha vidole vyake,ikabidi nimuulize kama alipata ajari ya gari,akanijibu kwamba ni historia ndefu.
Chanzo ni vipigo alivyokuwa akipewa na marehemu mume wake,alivyoona kero akaamua kuhamia kwa ndugu yake Chanika,lakini kwakuwa alikuwa na biashara iliyochangamka ya kuuza matunda pale kinondoni mkwajuni (ndipo walipokuwa wakiishi kabla),akawa anatoka chanika,naenda Mkwajuni na kurudi jioni.
Siku jamaa akamfwata na panga na kumwambia “sasa leo nakubali” huko watoto wakishuhudia,alimchapa mapanga mengi kiasi kwamba mishipa ya fahamu iliharibiwa,maeneo ya mikono maana alikuwa akijikinga kichwa.
Ninyi wenzetu mnapiga wake zenu kiasi hicho mnatabu gani kichwani ?,