Mnaoacha gambe msitutangazie, mtakuja kuumbuka!

Mnaoacha gambe msitutangazie, mtakuja kuumbuka!

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Katika umri huo unaacha gambe ili iweje sasa?
Unataka kuhujumu uchumi?
Unataka kupunguza mapato ya taifa?
Unataka kupunguza ajira? Hivi unajua pombe moja unayokunywa inazalisha ajira zaidi ya 29 na kuendelea?
Umeshauriwa vibaya?
Huna haja ya kuacha bali unaweza tu kupumzika ama kupunguza kutokana na sababu mbalimbali
Majukumu kuongezeka
Afya kwa ushauri wa tabibu
Kipato kwa ushauri wa familia
Kiroho kwa ushauri wao kidini
Uamuzi binafsi na mengineyo kama uzinzi, ugomvi na madeni)
Kuacha kabisa ama moja kwa moja kuna hasara zake pia.. Labda tu kama Unataka kuwa mlozi
Vema ni
Kupunguza na kunywa kwa mpangilio ama kuzipa finyango likizo ya muda ziweze kujipanga kwa fatique nyingine😭🤣
Kunywa kwa timing
Kunywa kwa kiasi
Kunywa kwa furaha
Kunywa kwa uamuzi binafsi bila kushawishiwa na yeyote awaye yote!
Gambe lenye afya lina sheria zake! Zizingatie uishi maisha mengi
Unapokunywa zingatia haya
1. Wewe ni nani
2. Uko wapi
3. Unafanya nini
Hizi kanuni ni muhimu sana kuepuka aibu na hasara za kujitakia kama
Kutongoza hovyo
Kuanza kutoa ofa hovyo
Kuanza kakata viuno hadharani
Kugawa ajira Na kutangaza nafasi za Kazi
Kuchamba watu
Kutangaza kumwajibisha boss🤣
Kuanza kuongea ya sirini🤣 nknk
NB: usitangaze kuacha gambe kwa mapito ya muda.. Maana kuna siku tutakukuta mahali lock imetoka Kisawasawa mpaka unajikataa🤣
 
Mimi hapa ninatangaza kabisa kuacha kula gambe hadi majira ya 1800hrs siku hii.Muda huo nitautumia kutafuta hela ya kupiga gambe.Asante.
💪🏿💪🏿mimi
Foto's Kustgebied.jpeg
 
Mimi imenikodesha na kuninyong'onyeaha
😁😁 hapana mkuu pombe imeniongezea uzito wa mwili nimeona niipige chini mwaka mzima kwanza nirudi kwenye mazoezi na mlo

Next week never miss..count me in
Bro hapa kwenyewe nimewaka hatari naenda shambani veyula..tukutane msalato kwenye nyama badae
 
Katika umri huo unaacha gambe ili iweje sasa?
Unataka kuhujumu uchumi?
Unataka kupunguza mapato ya taifa?
Unataka kupunguza ajira? Hivi unajua pombe moja unayokunywa inazalisha ajira zaidi ya 29 na kuendelea?
Umeshauriwa vibaya?
Huna haja ya kuacha bali unaweza tu kupumzika ama kupunguza kutokana na sababu mbalimbali
Majukumu kuongezeka
Afya kwa ushauri wa tabibu
Kipato kwa ushauri wa familia
Kiroho kwa ushauri wao kidini
Uamuzi binafsi na mengineyo kama uzinzi, ugomvi na madeni)
Kuacha kabisa ama moja kwa moja kuna hasara zake pia.. Labda tu kama Unataka kuwa mlozi
Vema ni
Kupunguza na kunywa kwa mpangilio ama kuzipa finyango likizo ya muda ziweze kujipanga kwa fatique nyingine😭🤣
Kunywa kwa timing
Kunywa kwa kiasi
Kunywa kwa furaha
Kunywa kwa uamuzi binafsi bila kushawishiwa na yeyote awaye yote!
Gambe lenye afya lina sheria zake! Zizingatie uishi maisha mengi
Unapokunywa zingatia haya
1. Wewe ni nani
2. Uko wapi
3. Unafanya nini
Hizi kanuni ni muhimu sana kuepuka aibu na hasara za kujitakia kama
Kutongoza hovyo
Kuanza kutoa ofa hovyo
Kuanza kakata viuno hadharani
Kugawa ajira Na kutangaza nafasi za Kazi
Kuchamba watu
Kutangaza kumwajibisha boss🤣
Kuanza kuongea ya sirini🤣 nknk
NB: usitangaze kuacha gambe kwa mapito ya muda.. Maana kuna siku tutakukuta mahali lock imetoka Kisawasawa mpaka unajikataa🤣
View attachment 3192804
Nilikuwa mlevi kupindukia kwa zaidi ya miaka 15

Nilitangaza kuacha pombe na sasa naelekea mwaka, nimeichukia pombe vibaya mno
Kuacha pombe ni uamuzi wa mtu mwenyewe
 
Back
Top Bottom