ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kuzindua Ilani yake ya uchaguzi kwa mwaka 2025-2030 baada ya inayotekelezwa kwa sasa kuelekea ukingoni.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais Samia Suluhu Hassan amewaambia wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho leo Alhamisi, Mei 29, 2025 kuwa Ilani itakayozinduliwa kisha kwenda kunadiwa kwenye kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 itakuwa nzuri na inayogusa maeneo muhimu kwa Watanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amesema matarajio yake ni kuona Ilani mpya ya CCM inaweka mkazo kwenye sekta za kijamii hasa kilimo, afya na uchumi.
Kihongosi ameyasema hayo leo Alhamisi, Mei 29, 2025 nje ya ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Convertion Centre jijini Dodoma.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
"katika kuelekea kuipokea Ilani yetu ya CCM nina matumaini makubwa sababu viongozi wetu wamekuwa na weledi mkubwa kwenye kuandaa ilani za uchaguzi. Miaka yote imekuwa ikiandaa mipango bora hivyo, mwaka 2025 inakwenda kuandaa majibu ya maswali yote ya Watanzania," amesema Kihongosi.
Hata hivyo, amesema katika Ilani hii ambayo inakuja wanatarajia kuona ikigusa katika kila sekta za kijamii kuliko maeneo mengine ambayo tayari yameshatekelezwa katika ilani inayomalizika.
"Binafsi ningependa kuona nguvu inaongezwa katika sekta zote za kijamii kama vile kilimo, afya, uchumi na uzalishaji mali angalau wananchi wa chini waguswe kwa ukubwa wake ili kusukuma uchumi wa nchi kuanzia chini," amesema Kihongosi