Kula unachokula usijali maneno maneno, tafiti nyingi zimefanyika kwenye vyakula vya ulaya, na america. Hivi vyetu huwa tunavipita tu hatufanyi tafiti za kutosha, wakosoaji wengi ni wale wenye uwezo mbadala. Wananchi wengi hatuna mbadala, tunakula kinachopatikana kwa urahisi.
Familia zetu tunalima mihogo kwa ajili ya unga sio kuuza, Tunalima mahindoi kwa ajili ya unga sio ya kuchoma, Tunalima mtama, uwele, na uwele kwa ajili ya unga wa kupikia ugali sio uji.
Kanda ya ziwa tulikuwa tunavua samamki kwa ajili ya kitoweo, mboga za majani tunakula za kienyeji sio chineese, cabbage au michicha.
Tukifika mijini tunaanza kusikia utakulaje ugali asubuhi, au utakulaje ugali maharage kila siku, au unakula wanga sana, asubuhi uji, mchana ugali na usiku ugali.
Sisi tulikuzwa tunakula hivyo, kama sio uji na viazi au mihogo, basi unaweza kula chochote hata kipolo cha ugali asubuhi kama kifungua kinywa.
Tumekua tumeishi vizuri na tuna afya nzuri tu, hatuna magonjwa kama visukari, wala blood pressure.
Sasa wao wanao kunywa chai na mikate, wanataka nasisi tule kama wao, au chai na mandazi,vitumbua au chapati.
Binafsi nakunywa uji na viazi vya kuchemsha ua mihogo ya kuchemsha na sioni shida yoyote.
Kwasababu sipati mboga za kienyeji ndio nakula hizi sukuma wiki, michicha na cabbage, pia samaki, dagaa, au samaki wa kuanikwa kwa jua au moshi kule kanda ya ziwa tunawaita vibambara.
Ukiwafiuata hawa kwanza budget inakuwa kubwa na unaweza ushindwe kumudu maisha yako.
Kiafya wanavyokula wao ndio hatari zaidi kuliko tulivyozoea sisi.
wao wanakula sukari kwenye chai, mikate,cake, vitumbua na mandazi. Mimi kwenye viazi sipati sukari.
Nisiandike meengi ila nilichotaka kusema.
Kula upendavyo na uwezavyo, vyakula vingi vya mijini vina matatizo kiafya kula vyetu vya kiasili, usijali maneno yao.