Mnaofuatilia soka la Bongo mna moyo mgumu sana. Soka halivutii kabisa

soka la tz linaonekana la hovyo kwa sababu ya udhamini mdogo bado timu nying hazina nguvu ya udhamini, ni ngumu sana sisimizi kumuangusha tembo na ni ukichaa tembo akijisifu kumuweza sisimizi wakati tembo wenzie hawawezi. Kitu kingine ni teknolojia duni yani unaangalia mechi makosa ni mengi lakin hakuna visaidizi zaid vya kuwezesha kubaini kilichotokea(wale wanaojua kuhusu VAR watakubaliana na mimi) madhambi yamefanyika lakini REPLAYni mara moja tu tena mbovu hata sisi watazamaji tunashindwa kuelewa ni kipi hasa kilichotokea. Waamuzi nao wanakuwa wepesi mno kutoa kadi utadhani ni za harusi hata kwenye foul ambazo ni za kawaida sana, soka la hapa nyumbani bado sana tunahtaji mengi sana kwenye soka letu.
 
hakika mkuu hata mimi sifuatiliagi huu upuuzi soka la bongo ukiangalia hata magoli wanayofungawanayofunga hawa magiant kwa vitimu vidogo hayana ufundi wowote na yanazuulika ila sema wachezaji wa vitimu vidogo nao mafan wa hao magiant wa kkoo ndio maana wanafanya mambo ya ovyo hata Azam haijulikani inataka nini
 
hao mikia FC wanabebwa na Ceria.
 
Mpira nchini unaharibiwa na timu ya Simba Mia kwa mia
Refa dhahiri alihongwa na simba wakishirikiana na tff
 
Soka letu ubovu wake unaanzia kwenye ubovu wa viwanja...
Kwa game ya AZAM + SIMBA kusema inaonyesha ubovu wa soka letu hapo sio kweli (una lako jambo?... huwezi kupata soka la ufundi na mbinu nchi hii tofauti na hizi timu 2.
Game kama hz mara nyingi fujo na kukamiana hakukosi hata huko ulaya ulikopanga kuna battle kama hizi nyingi tu.
Na ukilinganisha soka la ulaya na bongo utakuwa unakosea sana..
Mfano angalia world cup timu zetu za afrika na timu za ulaya au amerika, unaona kama tunajifunza kabisa.
Lakini ukweli utabaki palepale sio sisi tu tulio nyuma ila afrika ligi zetu ni chache zenye soka bora
 
Kumbuka wanaocheza wana mikataba wanalipwa na wanaendesha familia kwa soka hilo unaloona ni bovu, hata wewe kazini kwako wapo wanaosema haufanyi vizuri ila maisha yako yanaenda.
Ni kweli soka la bongo ni baya ukilinganisha na Ulaya ila sisi tunalipenda hivyo hivyo, tena umenikumbusha kulipia azam, kuna game kali ya Singida utd na Simba mtoto hatumwi dukani , hilo game Simba anakufa mapemaaaaaa.
NB : mimi sio Yanga
 
Uliangalia mpira vzr au unaongelea mhemko tu wa kinazi?
 
Komaaa kufuatilia aiseeeee mm akili ufwala huo sina
 
Kijana kua mzalendo, penda vya nyumbani,
Maendeleo hayana vyama
 
Uliangalia mpira vzr au unaongelea mhemko tu wa kinazi?
Sijaanza jana kufatilia soka la bongo... labda wewe unaeishi Watford England utuambie umeanza lini ??
Ubishoo wa kijinga punguza ndugu.
 
Swali langu ulilielewa vzr au umeendelea kutumia mhemko kujibu badala ya fikara
Sijaanza jana kufatilia soka la bongo... labda wewe unaeishi Watford England utuambie umeanza lini ??
Ubishoo wa kijinga punguza ndugu.
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kila mtu afanye anachokipenda anayeshabikia mpira wa bongo ashabikie anayeshabikia wa ulaya ashabikie.
 
Nenda ukafume vitambaa huko, mpira uache kama ulivyo
 
Mpira sio fani yako broo, umevamia! Mtu wa mpira hata ukikuta watoto wadogo mtaani wanacheza mpira waweza poteza dakika kuwaangia!
 
tatizo ni elimu ya mpira haipo,mchezaji anajua kanuni za mpira wakati yupo daraja la kwanza au ligi kuu,mchezaji kama kaseke na ali ali sio wa kucheza premier league,mohd hussein na simba..wachezaji wa daraja la nne miaka ya 90 walikua sawa au zaidi ya hawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…