Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

We ndo unaleta stori za kwenye vijiwe umemwaga povu jingi bila ushahidi wala kufanya uchunguzi zaidi ya Kuandika blahblah...ndo nyinyi. Mnachangia kudidimiza soka la bongo kwa kujifanya wajuaji kumbe hamna kitu
 
We ndo unaleta stori za kwenye vijiwe umemwaga povu jingi bila ushahidi wala kufanya uchunguzi zaidi ya Kuandika blahblah...ndo nyinyi. Mnachangia kudidimiza soka la bongo kwa kujifanya wajuaji kumbe hamna kitu
We ndo unaleta stori za kwenye vijiwe umemwaga povu jingi bila ushahidi wala kufanya uchunguzi zaidi ya Kuandika blahblah...ndo nyinyi. Mnachangia kudidimiza soka la bongo kwa kujifanya wajuaji kumbe hamna kitu
Wewe mbona unaongea saaaana!!! haya hebu eleza wewe lile tukio la goli La Ngoma mpira ulipopigwa na Juma Abdul Ngoma alikuwa ameotea au hakuwa Offside!!!!!!!??? Halafu kwanza wewe unaonekana hujui mpira bora niachane na wewe, wakija wanaojua sheria za mpira nitaongea nao.
 
Mikia kelele mingi, mnachoweza ni Taarab!

Angalieni magoli yote yalivyofungwa
 
ile faulo aliyofanya Joshua ni mbaya kuliko hata ya Kessy kwani alionesha kabisa kwamba anakwenda kulipiza na akamrukia mwenzake tumboni kitu ambacho ni gross misconduct kabisa na refa anakwenda kutoa njano
 


ninachoona hapa hata Yondani alikua Offside na alimsukuma mchezaji wa Castal ili asiucheze mpira kilichomponza ASS REF ni kutaka kunyanyua kibendera na kuficha na baadaye kuyeyusha kuonesha anayaona matukio ambayo hata mengine hayakua offside alimradi tu alishatimiza azam yake
 
hii ya kushika mpira kwa kweli niliona tu wachezaji wa coastala wakiyanyua mikono ila kiukweli Azam waboreshe maana ni kama STAR TV tu walivyokuwa wanaonesha na wao wajinasibu huku wakichomoa pesa za watz
 
Kila ligi ina uhondo wake mkuu.
 
Umeongea sahihi kbs mkuu
 
The Boss mimi sikuwepo uwanjani lakini niliangalia mpira kupitia luninga. Nakubaliana na wewe kuhusu faul ilihitaji straight red card badala ya njano. Matukio mengine ni kishabiki zaidi na kihisia kwa kuwa hayakuthibitishwa na Azam wameshindwa kabisa kuyaonyesha ili kujiridhisha. Watangazaji hawakuwa uwanjani nao walikuwa wanatangaza kupitia kwenye tv kwani mpira unaweza kusimama wasijue nini kimetokea mpaka camera ionyeshe mtu yupo chini ndo wanatangaza. Kws hiyo hata watangazaji walishindwa kuficha hisia zao na wakatangaza kiushabiki. Ukiangalia hata mipira ya EPL na kwingineko ambako unasema kuna watu wamehamia huko nayo pia malalamiko kwa waamuzi yapo kama goals za off side nk. Kwa hiyo inawezekana ni mapungufu ya kibinadamu zaidi kuliko hisia za mbeleko.
 
Mleta mada umezidisha hisia sana kuliko uhalisia.Kwa taarifa yako tu hakuna sheria complicated kama hiyo ya kuotea.Hakuna video iliyorejewa jana ili tujiridhishe,zaidi ya maneno ya kishabiki ya JAMES RANGE.Kwa upande wa Oscar Joshua alistahili red.
 
Inawezekana Ukawa unaujua mpira kwa kuutazama ila si kujua na sheria/kanuni za mpira unataka tubishane kati ya wewe ulieangalia mpira kwa TV na mimi nilikuwa uwanjani siku nyingine uwe unaangalia na body language ya mfungaji ndo utaelewa goli alilofunga ni sahihi au laah kibendera mwenyewe alikuwa anatetemeka anajua amepeta kitu ambacho ni cha wazi ndo mana toka aruhusu lile goli akakosa Umakini kabisa na refa wake hakuwa na msimamo thabiti kama umempa kadi mchezaji alienawa mpira makusudi unashindwaje kadi nyekundu aliempiga mwenzie teke kwa makusudi ambapo angeweza mjeruhi mwenzie vibaya ..muda mwingine usijivike koti la u Yanga ukasahau mpira ni fair play na kama sheria ni msumeno inabidi ukate pande zote
 
Una uhakika mimi Simba?
unafikiri wote humu wanaotaka fair play ni Simba?
Kubaini fair play kunahitaji fair observation itayopelekea kwenye fair opinion. Sijui kama ni kwa makisudi ama ni kwa bahati mbaya, wanaojenga hoja ya Yanga kubebwa kwenye uzi huu, wote wanaonekana kuwa na biased observation. Kwa hivyo hata maoni yao - bila ya kujali usahihi wake - yanaonekana kuwa ni biased.
 
Mwamuzi aliamuru timu ziingie uwanjani baada ya askari kuwatanya mashabiki wa cu Dida alirudi golini akakutana na mawe tena Mwamuzi msaidizi nae akiwa anaenda kwenye nafasi yake akala jiwe la uso, ndipo Mwamuzi akasubiri kwa dk 10 kama cu watarudi uwanjani na hali itatulia dk zikaisha Mwamuzi kapuliza kumaliza mchezo siyo kuahirisha mchezo.

Sababu za kuahirisha mchezo
1. Mvua
2. Giza
3. Au hatari yoyote isiyosababishwa na timu yoyote kati hizo mbili

Kumaliza mchezo
1. Timu ikigoma kurudi uwanjani
2. Kuleta vurugu ( kama hii ya cu)
 

Hii ni biased opinion kupita maelezo.Unawezaje kufikia hitimisho kubwa kiasi hiki dhidi ya upande mmoja huku ukisafisha upane mwingine. Unataka kuniambia wanaotetea Yanga wako objective? Unaweza kuaminika kuwa wewe pia uko objective kwenye hili?
 
Yanga Inabebwa? Huo ni uongo wa mchana ,mlianza na Azam inabebwa sasa Yanga huo ni uongo mkubwa .Yanga ina wachezaji wazuri kuliko timu yoyote TZ sasa kubebwa kunatoka wapi?
 
Hata ulaya waliwahi kusema man U inabebwa wakati wa Sir Alex F ,ila ukweli ni kuwa Man u Ilikuwa Klabu bora Uingereza the same applied to Baca wanasema ni timu ya FIfa ila sio ukweli
 
Hii ni biased opinion kupita maelezo.Unawezaje kufikia hitimisho kubwa kiasi hiki dhidi ya upande mmoja huku ukisafisha upane mwingine. Unataka kuniambia wanaotetea Yanga wako objective? Unaweza kuaminika kuwa wewe pia uko objective kwenye hili?
1. Unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union ni kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Jaalia mechi ya Coastal vs. Yanga ambayo ni lazima itoe mshindi ingeamuliwa ichezwe Dar-Es-salaam nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngesemaje? Kwa kuufumbia macho upendeleo huo wa dhahiri na wa msingi tangu mechi haijachezwa maana yake ni kwamba issue kwenu sio fairness in football lakini fairness against Yanga.
2. Unbiased oioinion yoyote juu ya maswala ya jana inejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context. Azam TV haikutoa fursa hiyo, na huenda ni kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi. Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football bali in fairness against Yanga.
3. Unbiased Opinion yoyote ingehoji tangu mwanzo Azam TV ambayo kama ni sehemu ya Bakhreesa Group of Companies yenye timu ndani ya Ligi Kuu kuwa ndiye mwenye haki pekee za kuonesha Ligi ambayo timu yake inashiriki. Unbiased opinion holders wangehoji iwapo hilo halingeleta mgongano wa kimaslahi. Jaalia Manji angekuwa na TV yake, ikapewa haki za kuonesha Ligi Kuu peke yake, nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngekosea kuhoji? Kama hiyo haitoshi, Azam haohao wenye timu inayoshiriki wakapewa udhamini wa Kombe la FA kwa sababu tu ndio waliojitolea udhamini. Halafu TV yao hiyohiyo ioneshe michezo ya mashindano hayo, fairness iko wapi hapo? Mbona hakuna aloyehoji? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
4. Kwa vyovyote iwavyo, iweje wachangiaji wote kutokemea na wengineo hata kudiriki kutetea uhuni wa watu kuvamia uwanja na waamuzi kupigwa mawe, eti kwa sababu waamuzi wamesababisha? Huo ndio umahiri tunaoutarajia kutoka kwa wana JF? Fairness iko wapi hapo? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, lakini iko kwenye fairness against Yanga.
5. Kulipizia ni kosa linalostahili onyo kwa mchezaji. Onyo linaweza kuwa ni kwa maneno, kadi ya njano ama nyekundu kwa mujibu wa uzito wa kosa lenyewe na maoni (discretion) ya mwamuzi. Fairness iko kwenye kutambua kwamba mwamuzi atapima uzito wa kosa lenyewe kabla hajatoa onyo. Wanaoshupalia kwamba Oscar alipaswa kupewa kadi nyekundu wanajikuta, out of bias, wakijitwisha madaraka ya mwamuzi. Tujaalie kosa kama hilo angafanya Shiboli na akatolewa kwa kadi nyekundu, mngekosea kudhani kwamba mwamuzi anaipendelea Yanga? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
Baada ya yote haya na mengineyo ambayo haina haja kuyakariri kwa kuokoa muda, utasemaje kwamba wachangiaji wanaoituhumu Yanga wako neutral, unbiased and absolutely fair?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…