1. Unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union ni kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Jaalia mechi ya Coastal vs. Yanga ambayo ni lazima itoe mshindi ingeamuliwa ichezwe Dar-Es-salaam nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngesemaje? Kwa kuufumbia macho upendeleo huo wa dhahiri na wa msingi tangu mechi haijachezwa maana yake ni kwamba issue kwenu sio fairness in football lakini fairness against Yanga.
2. Unbiased oioinion yoyote juu ya maswala ya jana inejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context. Azam TV haikutoa fursa hiyo, na huenda ni kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi. Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football bali in fairness against Yanga.
3. Unbiased Opinion yoyote ingehoji tangu mwanzo Azam TV ambayo kama ni sehemu ya Bakhreesa Group of Companies yenye timu ndani ya Ligi Kuu kuwa ndiye mwenye haki pekee za kuonesha Ligi ambayo timu yake inashiriki. Unbiased opinion holders wangehoji iwapo hilo halingeleta mgongano wa kimaslahi. Jaalia Manji angekuwa na TV yake, ikapewa haki za kuonesha Ligi Kuu peke yake, nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngekosea kuhoji? Kama hiyo haitoshi, Azam haohao wenye timu inayoshiriki wakapewa udhamini wa Kombe la FA kwa sababu tu ndio waliojitolea udhamini. Halafu TV yao hiyohiyo ioneshe michezo ya mashindano hayo, fairness iko wapi hapo? Mbona hakuna aloyehoji? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
4. Kwa vyovyote iwavyo, iweje wachangiaji wote kutokemea na wengineo hata kudiriki kutetea uhuni wa watu kuvamia uwanja na waamuzi kupigwa mawe, eti kwa sababu waamuzi wamesababisha? Huo ndio umahiri tunaoutarajia kutoka kwa wana JF? Fairness iko wapi hapo? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, lakini iko kwenye fairness against Yanga.
5. Kulipizia ni kosa linalostahili onyo kwa mchezaji. Onyo linaweza kuwa ni kwa maneno, kadi ya njano ama nyekundu kwa mujibu wa uzito wa kosa lenyewe na maoni (discretion) ya mwamuzi. Fairness iko kwenye kutambua kwamba mwamuzi atapima uzito wa kosa lenyewe kabla hajatoa onyo. Wanaoshupalia kwamba Oscar alipaswa kupewa kadi nyekundu wanajikuta, out of bias, wakijitwisha madaraka ya mwamuzi. Tujaalie kosa kama hilo angafanya Shiboli na akatolewa kwa kadi nyekundu, mngekosea kudhani kwamba mwamuzi anaipendelea Yanga? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
Baada ya yote haya na mengineyo ambayo haina haja kuyakariri kwa kuokoa muda, utasemaje kwamba wachangiaji wanaoituhumu Yanga wako neutral, unbiased and absolutely fair?