Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

Akili za vijiweni umeleta hapa
kwako wewe huwezi kuzungumza ya Yanga bila kuitaja Simba...
Hivi unajua kuna mashabiki wangapi wa Yanga na Simba wameacha kufuatilia mpira wa TZ?
wamehamia EPL na UEFA?

watu type yako ndo mnafilkiri mpira ni Simba na Yanga tu....
upeo finyu
hujui wachezaji wanaoachwa hata wakicheza faulo mbaya wataenda chezea Taifa Stars na kufanya madudu
hayo hayo?


Au wewe akili yako yoote inaishia Simba na Yanga?
Mi ni mmoja wapo nimeacha kufuatilia mpira wa bongo kwa ajili ya mambo haya
 
The Boss hivi kweli wewe unaongea haya kutoka kichwani mwako!!!! Unakumbuka game ya Yanga na Simba ile round ya kwanza Israel Nkongo alimaliza mechi ikiwa inasoka dakika ngapi!!!!!
Haya niambie wewe game ambayo waliongezewa dakika kumi!!!! Hukumbuka kama Simba ndio waliongezewa dak 10 game na Stand United!!!!Acha kujitoa ufahamu kiongozi. Hebu jipange kwanza kabla hujaandika vitu vya kusadika humu jukwaani. Sisi hatuzungumzii stor za kwenye vijiwe vya kwenye kahawa hapa.
Mbona reference inakuwa samba, kwani ww unauhakika gani kama THE BOSS ni simba ?
 
1. Unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union ni kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Jaalia mechi ya Coastal vs. Yanga ambayo ni lazima itoe mshindi ingeamuliwa ichezwe Dar-Es-salaam nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngesemaje? Kwa kuufumbia macho upendeleo huo wa dhahiri na wa msingi tangu mechi haijachezwa maana yake ni kwamba issue kwenu sio fairness in football lakini fairness against Yanga.
2. Unbiased oioinion yoyote juu ya maswala ya jana inejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context. Azam TV haikutoa fursa hiyo, na huenda ni kwa sababu ya mgongano wa kimaslahi. Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football bali in fairness against Yanga.
3. Unbiased Opinion yoyote ingehoji tangu mwanzo Azam TV ambayo kama ni sehemu ya Bakhreesa Group of Companies yenye timu ndani ya Ligi Kuu kuwa ndiye mwenye haki pekee za kuonesha Ligi ambayo timu yake inashiriki. Unbiased opinion holders wangehoji iwapo hilo halingeleta mgongano wa kimaslahi. Jaalia Manji angekuwa na TV yake, ikapewa haki za kuonesha Ligi Kuu peke yake, nyinyi wenye anti-Yanga sentiments mngekosea kuhoji? Kama hiyo haitoshi, Azam haohao wenye timu inayoshiriki wakapewa udhamini wa Kombe la FA kwa sababu tu ndio waliojitolea udhamini. Halafu TV yao hiyohiyo ioneshe michezo ya mashindano hayo, fairness iko wapi hapo? Mbona hakuna aloyehoji? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
4. Kwa vyovyote iwavyo, iweje wachangiaji wote kutokemea na wengineo hata kudiriki kutetea uhuni wa watu kuvamia uwanja na waamuzi kupigwa mawe, eti kwa sababu waamuzi wamesababisha? Huo ndio umahiri tunaoutarajia kutoka kwa wana JF? Fairness iko wapi hapo? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, lakini iko kwenye fairness against Yanga.
5. Kulipizia ni kosa linalostahili onyo kwa mchezaji. Onyo linaweza kuwa ni kwa maneno, kadi ya njano ama nyekundu kwa mujibu wa uzito wa kosa lenyewe na maoni (discretion) ya mwamuzi. Fairness iko kwenye kutambua kwamba mwamuzi atapima uzito wa kosa lenyewe kabla hajatoa onyo. Wanaoshupalia kwamba Oscar alipaswa kupewa kadi nyekundu wanajikuta, out of bias, wakijitwisha madaraka ya mwamuzi. Tujaalie kosa kama hilo angafanya Shiboli na akatolewa kwa kadi nyekundu, mngekosea kudhani kwamba mwamuzi anaipendelea Yanga? Maana yake ni kwamba issue yenu haiko kwenye fairness in football, iko kwenye fairness against Yanga.
Baada ya yote haya na mengineyo ambayo haina haja kuyakariri kwa kuokoa muda, utasemaje kwamba wachangiaji wanaoituhumu Yanga wako neutral, unbiased and absolutely fair?
very nice observation never seen
 
Hao wanaibeba yanga ili ifike fainali na simba au azam ili wao wapige hela pale taifa si wanajua watajaza uwanja wao wapige hela tu na kuua soka la tz
 
1. Hoja ya upendeleo kwa Yanga ni subjective na inaweza kuanzia kujadiliwa wakati wowote ule. Inategema na hoja anazoleta mtu. Tatizo ni wewe
unapolazimisha tuihusishe na uchaguzi wa uwanja wa kuchezea mechi ya jana pekee bila kukumbuka kuwa michezo hii ilianza zamani na Yanga ni mojawapo ya timu zilizonufaika zaidi kuchezea Uwanja wa Nyumbani isipokuwa jana.

2. Hoja ya kulazimisha watu watoe maoni baada ya kuangalia marudio ya picha TV haina mashiko. Kwani wewe unaamini wote wanaosema ile ilikuwa offside walikuwa wanatazama kupitia TV? Pili, mnaosema lilikuwa bao halali ninyi mnatumia marudio gani ya picha ya TV?Ni sahihi kulaumu wanaopinga bila kupata picha za marudion za TV huku ukiunga mkono wanaosema hapakuwa na offside bila na wao pia kutumia picha za Tv? Sitarajii reasoning ya aina hii kwa mtu objective.

3. Hoja yako ya tatu, nilishasema sina maoni kwa sababu haina uhusiano na mchezo au kilichotokea jana huko Tanga.
Na pia sio somo husika hapa.

4. Kushangaa kwako mimi kuunga mkono hoja ya uhuni wa mashabiki wa jana ndio kunazidi kuniaminisha kuwa wewe hauko objective katika hili. Unadhani mimi nitapinga kila kitu for the sake ya kupinga? Halafu hebu kagua vizuri kabla ya wewe kuandika hoja yako kama mimi nilikuwa nimeshatoa maoni. Hoja zako laini ndio zimenishangaza na kunivuta jukwaani. Na angekuwa ni mtu mwingine kaandika yawezekana nisinge comment chochote lakini sio wewe niliyetegemea hoja zenye kufikirisha zaidi

5. Hilo la mwamuzi kutumia 'akili' katika makosa makubwa na ya wazi ndio palipo na uvundo. Hii akili ya mtu mmoja akicheza rafu anapewa kadi stahili, mwinge mwamuzi anatumia kiachoitwa akili, ndipo palipo na jipu. Unadhani walioweka sheria za mchezo hawakujua kuna akili? Mwisho wa kutumia akili ni wapi? Hoja ya mwamuzi kuwepo au kutokuwepo kwenye tukio haina maana, maana mwamuzi anapaswa kufuata au kutazama mpira uliko. Na kama kwa mfano tuamini hakuona kwa nini alitoa kadi ya njano?
safi sana
 
Yanga ni team bora sana aisee. Hivi ni mechi ngapi vile kabebwa tumfutie point zake tuwaongezee mikia... Nashangaa mnatoka mapovu tu. Na mechi ya mgambo umeiona?
 
Wanasimba, hii ni awamu ya hapa kazi tu, ujanja ujanja mliyoifanya kipindi cha nyuma mzisahau, kumbukeni ujanja ujanja uliwasaidia kutokushuka daraja la siyo tungewasahau ķwenye historia ya soka kama ilivyo Pamba!
 
Kumbe yule refa anaeitwa Kambuzi ambae aliwabeba walipocheza na azam akakataa goli la shomari kapombe na pelnat ndo huyohuyo walimpanga tena awabebe kwa coastal.Mambo yameharibika wamemfungia maisha...
 
Kumbe yule refa anaeitwa Kambuzi ambae aliwabeba walipocheza na azam akakataa goli la shomari kapombe na pelnat ndo huyohuyo walimpanga tena awabebe kwa coastal.Mambo yameharibika wamemfungia maisha...
Ndie huyu huyu ambae aliwazawadia Simba penati dakika ya 95 msimu uliopita game ambayo ilifanyika pale taifa, penati ambayo iligonga mwamba huku matokeo yakisomeka Simba 1-2 Mbeya city. Ila yale hayasemwi!!!!!!!
 
Si kuiharibia Yanga tu, bali wanapandikiza Kansa wenye soka letu. Kwa namna hii hatufuki popote.

Nimeicheki hiyo game kweli uamuzi ulikuwa too weak!! na inaonekana ni kwa MAKUSUDI.
 
Ndie huyu huyu ambae aliwazawadia Simba penati dakika ya 95 msimu uliopita game ambayo ilifanyika pale taifa, penati ambayo iligonga mwamba huku matokeo yakisomeka Simba 1-2 Mbeya city. Ila yale hayasemwi!!!!!!!
Afadhali wakumbushe hao.
 
Kweli wanabebwa Sana tens na ngoma,kaseke na tambwe,uboora WA wachezaji ,uimara WA benchi la ufundi ndo vinawabeba yanga simba jipangeni
 
Back
Top Bottom