Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

Niliamua kuacha kuwa shabiki wa timu zetu sio siri, kuna vitu vinatia hasira sana, hv timu ni hzo tu???Kuna cku "Julio alisema ifikie hatua basi TFF wabaki na timu tatu tu",haina maana ya kuweka timu nyingine,kma hawakutaka timu zingine zifike fainali kulikuwa na haja gani ya kuanzisha haya mashindano???Namchukia sana Malinzi uongozi wake mbovu cjawah kuona
Na kwa mtindo huu tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu miaka nenda rudi
 
Hata hivyo vile vile huwezi tumia ripoti hizo kama hitimisho pekee la maamuzi yako, lazima uangalie na vyanzo vingine ili uweze kufikia maamuzi ya haki
1.Kufanya uchunguzi lazima uwe na reference point tumeona ulaya pamoja na teknolojia walio nayo lazima kwanza wapitie ripoti ya mwamuzi

2.Halafu huwezi kuchunguza mechi bila ya kupata malalamiko rasmi kutoka kwa klabu husika na sio malalamiko ya washabiki
 
Kwenye football maamuzi ya refa ndiyo ya mwisho,kuna makosa ya kwenda CAS lakini sio la refa kukataa goli halali au kumpa mchezaji kadi kimakosa
 
Mpaka sasa hatujajua kama kuna formal complaints ambazo zimekua lodged au sio? vile vile principles za natural justice pia zinakua applicable hatakama ni huko kwenye mpira , kwamba huwezi tegemea ripoti ya mtuhumiwa pekee katika kufanya maamuzi..sijui umeielewa hoja yangu.
 
Kwenye football maamuzi ya refa ndiyo ya mwisho,kuna makosa ya kwenda CAS lakini sio la refa kukataa goli halali au kumpa mchezaji kadi kimakosa

NI sawa kwamba maamuzi ya refa ni ya mwisho uwanjani, lakini si ya mwisho nje ya uwanja kwani kuna kanuni na taratibu za kuyachallenge maamuzi yake pale inapoonekana kuna viashiria vya wazi vya upendeleo katika maamuzi yake...inafanyika hivyo dunia nzima.
 

Kwa maneno ya mashabiki (wa Coast,Simba ) wale ni watuhumiwa ,lakini kwa sasa sio watuhumiwa hadi Coastal watakavyopeleka malalamiko yao rasmi.Kuna unafiki mkubwa sana makocha,waandishi wa habari na viongozi wa soka hapa Tanzania wakiulizwa wanasema mechi nyingi timu zinapanga matokeo lakini hawatoi ushirikiano ili kuondoa huo uozo
 
Akili zako ndo zimeishia hapo
sio kosa lako
acha dharau tunakufuatilia ,unacoment ujinga ukihisi unajua na kama unahisi maendeleo au utaalamu ni kufuatilia mpira wa ulaya ,sasa kwanini unapoteza muda wako kufuatilia mechi ya yanga na c.union. You are nothing but a bogus friend.
 

Hoja zako zinaonyesha licha tu ya kuzidiwa na mahaba ya timu uipendayo lakini hata ile sifa niliyotaka kukupa kuwa mchambuzi huru haikustahili kabisa. Kwa taarifa yako wachambuzi wote dunianiwana timu wazipendazo, wana mapenzi binafsi. Hata waamuzi pia, waandishi wa habari na viongozi wa vyama vya soka pia. Kinachowatofautisha na mashabiki na wanazi ni kuwa wanapokuwa kazini au hata kama sio kazini, inapobidi wao wanatazama jambo kwa macho mawili. Lakini wewe unadhirihisha uko tayari kufumba macho pale unapoambiwa ukweli ili mradi tu timu yako inaguswa. Waungwana hukaa kimya, pale ushahidi wa mambo unavyokuwa kinyume chao. Nitafafanua.

1. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union kwa kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Seriously? Yaani tusijadili utumbo wa waamuzi wa jana kwa sababu ratiba haikuwa fair kwako? Ulianzisha mada hiyo ya ratiba watu wakakupinga? Sawa. Hata tukianza kuzingatia kujadili hilo kama tunataka kutenda HAKI unadhani itafaa kuanzia na mechi ya Coastal Union v. Yanga tu, au turudi nyuma zaidi kwa Yanga kucheza mechi zote za FA nyumbani kabla ya hii mechi ya Coastal Union, tena ambayo imepangwa hivi kutokana na pressure tu za wadau?

2. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya maswala ya jana ingejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context.

Hii ni sheria au kanuni gani au ndio unaianzisha? Refa anapoamua offside huwa anatumia picha za TV? Walioko uwanjani wanaangalia mechi laivu unataka nao wasubiri picha za tv? Mechi zinazochezwa bila kurushwa laivu hazina offside? Wanaotazama uwanjani huwa wanapiga kelele za kupinga au kuzomea kutokana na picha za TV? Wakati Yanga wanapiga mwamuzi mwaka 2012 walitumia picha? Acha kuleta hoja nyepesi kwenye vitu serious.

3. Hoja yako hii ya mgongano wa maslahi kati ya Azam FC na TV yako sina opinion kwa sasa, japo sijui inaingiliana vipi na
utumbo wa maamuzi ya mechi kati ya Coastal Union v. Yanga

4. Hoja yako hii namba nne nakubaliana nayo kwa 100%. Hizi hoja ndio zinazotakiwa kutoka kwa mtu mwenye heshima kama wewe. Walichofanya mashabiki wa Coastal Union ni uhuni usiokubalika. Adhabu kubwa iwaandane popote walipo. Lakini adhabu hii isiishie hapo tu, TFF wachunguze pia hivi vitendo vya waamuzi Ni bahati mbaya aU kuna nguvu ya mlungula?

5. Hoja yako hii ingetolewa na mtu mwingine ningeamini ni mtu asiyejua kabisa sheria za mchezo, lakini kwa kutolewa na wewe acha tu nijiaminishe kuwa kuna mtu anatumia ID yako! Retaliation yoyote ni straight red card. Wewe hili unalijua. Kulipizia ni kosa la kadi nyekundu moja kwa moja. Suala la upimaji wa uzito wa kosa linatokana na mambo mengine kama kusukuma lakini sio kumfata mchezaji mwenzako na kumkanyaga kifuani au tumboni huku ukiwa huna dhamira ya kucheza mpira. Bila blah blah na kufariajiana haziwezi kutsaidia wachezaji wetu. Kwa kweli Oscar Joshua ana bahati kuendelea kucheza mpira baada ya tukio lile.

Kwetu sisi wengine tushajizoesha kusema nyekundu nyekundu, bluu bluu sio mara bluu bahari au bluu maziwa.
 
TFF nao ni watu na wanasikia, mpaka sasa wameshasikia yanayosemwa na ili kulinda integrity ya Institution kuna ulazima kabisa wakaanzisha a formal inquiry kwa hiyo issue, sio lazima kuwe na formal complaint at times, wenyewe pia wanazewa fanya uchunguzi ili kulinda hadhi ya taasisi na ligi kwa ujumla wake, kwani malalamiko yakiachwa yaendelee watu wengi watajitoa kutazama na kudhamini mpira ukizingatia kua ile ni biashara na hakuna anayetaka kujihusisha na mambo yasiyoleta picha nzuri kwa biashara yake.
 
Uongozi uliopo wameshindwa kazi. Wao kazi yao ni gatecollection na kupanga matokeo. Yanga ipo juu ya Tff kama uamini subiri kamati yao yamagumashi ikae utasikia maamuzi watakayotoa.
 
Tukubaliane jambo moja...
Bongo hatuna waamuzi...hatuna marefa wala washika vibendera makini...huo ndio ukweli usiopingika.
Jiulize,
Je,yupo mwamuzi yeyote anayechezesha/aliyechezesha mechi za michuano ya klabu bingwa Afrika ama kombe la shirikisho kwa miaka ya hivi karibuni?
Yupo yeyote kwenye michuano ya kombe la dunia (FIFA),AFCON au hata CHAN?
 
Muda mwingine unaweza kusema mshika kibendera anapendelea kumbe maskini ya mungu hakuwa na kasi ya kutosha kuweza kuona offside kwa uhakika.
Anabaki na kigugumizi ninyanyue kibendera au nisinyanyue...anatoa uamuzi mbovu sie tunaona anapendelea kumbe ukweli ni kwamba ameshindwa kwenda na kasi ya mchezo...
 
Sio waamuzi tu
1.Hatuna wachezaji
2.Hatuna makocha (timu ngapi zinafundishwa na wageni ? Tuna makocha wangapi wanafundisha nje ya Tanzania)
3.Hatuna viongozi wa soka (TFF)
4.Hatuna viongozi wa vilabu vya soka
5.Hatuna viongozi wa vyama vya mikoa(hawa njia wanachagua viongozi wa TFF )
 
Kombe la FA Uingereza ambako ndiyo tunaazima vitu vingi, mechi za nusu fainali huchezwa kwenye neutral ground (Wembely). Labda mwakani TFF wabadili kanuni husika ili mechi za nusu fainali zichezwe neutral ground. Kuna kitu waingereza waliona wakafanya hivyo.

Pili, mechi zote za awali kila timu angalau icheze nusu ya mechi zake away na nusu nyingine nyumbani kuleta fairness.

Hivi Tanzania hatuna grading ya marefa? Wenzetu wanajua marefa wao kwa viwango kiasi cha kujua the top four ni akina nani. Nusu fainali zichezeshwe na number 2 na 3 ili yule number 1 apewe fainali.
 
Tatizo unaenda kutazama mpira ukiwa na hasira dhidi ya yanga kwa kuwa simba hafanyi vizuri.

Huu mchezo hautaki hasira boss
Sio kila anaeisema Yanga ni Simba, unakosea sana ndugu. Wengine ni wanazi wa mpira tu, hwako katika timu hizi mbili. Lakini ukweli lazima usemwe
 
Refa alistahili kupigwa risasi, roho inaniuma kwa upuuzi wa Jana, Yule match kamishna nahisi ndiye aliyepanga madudu yale,,
 
 

Attachments

Poleni wote mnaoangalia mpira wa simba na yanga kuitwa mzalendo sio kwamba upende vitu vibovu kwa mwavuli wa uzalendo
 
Tatizo si coastal wanaolalamika, bali ni simba ndio inao wauma.

Sasa kuna uchambuzi hapa, The Boss nawenzako pingeni kwa hoja



Mstari wa Zambarau->Mstari huu unaonesha kabisa goli la ngoma halikua offside mchezaji wa coastal alikua karibu kuelekea langoni kwake na ngoma yuko nyuma yake ⚫ hiyo c offside ❎


Mstari Mwekundu-> Huu mstari unaonesha mchezaj wa cost akihama position yake na kumuachia eneo ngoma kwaajili ya kutengeneza offside ⚫ Ameonekana hii si offside ❎

Mstari Mweusi-> Mstari huu unaonesha ngoma akimchomoka beki wa cost na kwenda kufunga goli⚽⚽⚽⚽ bila shaka hili ni goli sahihi kbsa ⚽✅


NB-Mchezaji ukitaka kutengeneza offside kuwa makini na aina ya mshambuliaji unaetaka kumfanyia hvo umakini wa kibendera na madhara kwa team yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…