Nimeona kuna movements za ku boycott / kugomea bidhaa zenye uhusiano na Israel, nimepata wazo nije kuwasapoti wadau kwenye huu mgomo kwa kuwashauri muweke mkazo zaidi kukaa mbali kwenye simu na computer kwasababu bidhaa na huduma hizi nyingi wanaozibuni ni wayahudi wa Israel.
China ndipo vilipo viwanda vingi vya kutoa nakala za bidhaa.
Marekani ndipo zilipo ofisi za usimamizi na uongozi wa makampuni haya.
Kampuni hizi unaweza kuzikuta hadi Kenya zikiwa na ofisi za ukanda, mauzo, n.k.
Lakini Israel ndipo zilipo akili zinazotegemewa kuumiza vichwa kubuni bidhaa kisha zinaenda kufyatuliwa nakala kwenye nchi kubwa kama china zenye viwanda vingi.
Makampuni makubwa kama Google, Microsoft, Intel, Qualcom, n.k. yana ofisi za Research and Development nchini Israel, Wameweka ofisi hizo kwajili ya kuwatumia wanasayansi na wahandisi wa Kiyahudi wawasaidie kubuni na kuendeleza bidhaa na huduma zao- wapo Israel kwajili ya kutumia akili za wayahudi wawabunie teknojia.
wao wanauza ubunifu, ni sawa na kwenye mgahawa, wapishi wameajiriwa kuandaa chakula lakini chakula kinajulikana ni cha mwenye mgahawa, mfano google wana ofisi Israel wameajiri wanasayansi wanaobuni teknolojia zinazoboresha matokeo ya google lakini google ndio wanaotambulika kumiliki hizo teknolojia.
Kwa ofisi za Marekani za Sillicon Valley ni kama tawi lao lingine, wamejazana mno kwenye ofisiz za Research and Development!!
Orodha chache ya Makampuni :
GOOGLE - Unaikwepaje google ukitumia internet kwamfano, Wao ndio wamiliki wa Android mfumo unaotumika kwenye simu kibao kama Samsung, Nokia, Sony, hadi huku kwenye Tecno na Itel
APPLE na SAMSUNG - Ni makampuni makubwa sana ya simu, Kwa upande wa Apple kuna laptops za Mac
INTEL - Hii ni chip inayotumika zaidi kwenye laptops, hio laptop yako unaiona imeandika Intel core i3, i5, i7, n.k. ujue hio ndio akili ya computer
HP na DELL - Brand maarufu za laptop hizi
MICROSOFT WINDOWS - System maarufu zaidi tunayotumia kwenye computer za mezani na laptops
AMAZON na EBAY - Masoko maarufu ya kuagiza bidhaa mtandaoni
IBM
ORACLE
Unaposikia Israel wapo vizuri ki intelejensia sio uchawi, ni kwamba wao wanahusika zaidi kwenye kubuni bidhaa za makampuni makubwa ya vifaa vya mawasiliano, hivyo inakuwa rahisi kwao kuingia kwenye mifumo
Kama upo kwenye kampeni ya kuipinga Israel itakuwa ni vema zaidi utumie simu za vitochi, computer za korea kaskazini, epuka kutumia google, n.k. Hadi hizo facebook, whatsapp, instagram ni za myahudi Mark Zuckbereg ongeza nguvu mpinge usitumie huduma zake.