Mnaojenga kuweni makini mnaponunua mbao, kuna wizi wa kutisha!

maichrim

Member
Joined
Mar 11, 2011
Posts
76
Reaction score
40
Ndugu zangu,

Hili limenitokea napenda kuwapa tahadhari wale wote wanaofikiria kwenda kununua mbao buguruni wawe makini. Mimi nilikubaliana bei vizuri na muuzaji na kweli mzigo ulikuwa mzuri, pia bei ilikuwa nzuri tena ya kuvutia. Kazi ya kupima mbao ilipoanza ndipo nilipobaini wizi unaofanyika.

Jamaa wanatumia tape measure ambayo ni wizi mtupu.

Nilishtuka kuana mbao ya urefu wa kawaida, tape measure inasoma ft 24, hapo ndipo nilipogutuka nikaanza kuiangalia ile tape measure vzr, kumbe wameruka vipimo ili kuongeza idadi ya futi ili wapate faida zaidi...mfano ile tape measure inasomeka 1, 2, 3, 4, 5, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 17, 18, 19, 22, ......... utaona jinsi kulivyo na gap kati ya 5-10, 15-17, 19-22...

Kwa mwendo huu unakuta jamaa wanaiba futi zaidi ya saba kwa mbao moja. Huu ni wizi mkubwa ukipiga hesa ya 300 kwa kila futi kwa zile mbao ndogo kabisa 2x2, ikiwa ni mbao inayouzwa futi 700/900 utashangaa umeibiwa hela nyingi mno.

Nikaja kuwakamata tena kwenye kujumlisha idadi ya futi zote baada ya kuhesabu mbao zote. Wanatumia calculator abayo ni famba!! yenyewe ikiandika 18.7 haiweki nukta inaingiza number nzima tu, hivyo 18.7 inakuwa 187. Walipomaliza kujumlisha nikashangaa kuona idadi kubwa mno ya futi ambazo ni sawa na hela nyingi mno!! nilipoanza kujumlisha mwenyewe kwa calculater ya simu yangu, nilibaini tofauti (wizi) wa laki tatu kwa mzigo mdogo wa laki 8.

Nimeona niwape hii wadau msijeingia vibaya. Jamaa wanakula kiulaini wasijue tunataabika sana kuitafuta hela ya kujengea...
 
Asante mkuu maichrim, nimecopy na kufanya wide circulation via email na facebook.
 
Aisee si ajabu nami niliingizwa mujini damn!
 
asante kwa tahadhari.....


Asnam printi kopi nyingi zitakusaidia baadae
 
Last edited by a moderator:
Mi nilijua jamaa anatumia Lugha ya picha kupunguza makali maana kahusisha Buguruni!!! kumbe kapotea.
 
mmmh hadi nifikie hatua ya kununua mbao ntakuwa nimeshasahau hii alert ngoja niprint niibandike ukutani.

we nilie mingo tutanunua muda si mrefu, lakini tutazifuata huko huko makete/makambako/mafinga kwa kina sanga original. Siwezi nunua kwa hao wachaga wa mujini. Kupakia tutatumia usafiri wa jah people au kama humaind ungo unatosha sana.
 
Sasa hatimaye walikuuzia kwa laki 5 au walikataa?
 
Hiyo ndio biashara ya Buguruni, mara nyingi huo uwa ni mpango wa madali waliopo hayo maeneo na hapo utashangaa mwenye duka kakubali ujinga huo ufanyike dukani kwake

La pili na la muhimu kwa wanunuzi wa mbao hapo Buguruni, Unaweza kuonyeshwa mbao za bei ya chini sana lakini ukweli hizo mbao sio zile treated kutoka Iringa, hizo mbao wanachukua Cyprus ya kawaida na kuipaka hiyo dawa juujuu tu, unaona mbao inanuka kabisa ile dawa lakini dawa haijafika ndani kabisa
 
Yaliwahi kunikuta pale kibaha!!! Nilkaacha wamemaliza mbao zote na risiti juu!!! Pale pale nikaagizia FUTI KAMBA MPYA na NOTE BOOK!!!
Baada ya kubainika nikaacha mzigo wote nikaenda kwa jirani....naye the same....nikachukia nikaenda kununulia mwenge....wa mwenge akasema usilipe mpaka zifike SITE na zipimwe upya zikiwa SITE!!!
 
Pole, unauchungu kweli. Ila mbao nazo ni MMU?

Nilivyoona Buguruni sikuwa na doubt kwamba hii ni MMU kwani hizo mbao anazozisema nikajua ni wale malaya wanaojiuza(lugha ya picha)...Kazi ya kupima mbao ilipoanza ndipo...nikajua washaingia gesti na jamaa keshaanza kula mzigo,...Mambo ya tape measure nikahisi ile ndimu wanayokamulia kwenye Uuke ikaonekana ndogo kumbe ndani ni bonge la dudu...(lugha ya picha)....Lol kumbe mwishoni ndo nikagundua alichoandika ndo alichomaanisha!!

Kweli Jukwaa kina mata kwa kila sredi...!!
 

kwa kifupi ni kwamba thread imekushughulisha ubongo kinoma......maana kurelate mambo yote haya na uhali wa kufikirika si haba!
 

nami yalishanikuta si buguruni peke yake, wauza mbao wengi ndio kamchezo kao hako. na wakishajua huna uelewa juu ya biashara hiyo au ndio mara ya kwanza kununua mbao wanakufanya kitu mbaya sana.

cha msingi tuwe makini sana tunapoenda kununua mbao popote pale na tusiaminiane kirahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…