Mnaojenga kuweni makini mnaponunua mbao, kuna wizi wa kutisha!

Jamani msikubali kuibiwa pale Buguruni. Mbali ya kutumia vipimo feki, hata mabao zao mara nyingi zinakuwa za kuchovya tu kwenye dawa. Wadau anayetaka mbao imara na kwa bei isiyokuwa na wizi aende pale Mabibo Kiwanda kwenye yard ya Sao Hill branch ya Dar Es Salaam. Wewe mwenyewe utapenda.

Achana na hao matapeli.

Tiba
 
Aiseee nimeshalizwa kwa kweli. Ndiyo maana hesabu niliyopiga kwa kununulia mbao na ile niliyopewa katika lile duka nililonunua zilitofautiana sana. Kwa kweli nilivyopewa hesabu sikuamini na kwa kuwa namtumia dogo kufanya hiyo shughuli as niko too far na dogo alijifanya kuchukua hizo mbao na kuanza ujenzi then kunambia, nilitamani ujenzi kwa kutumia hizo mbao ungekuwa haujaanza maana nilikuwa nafikiria kuwaruidishia wenyewe. Kiukweli nimepigwa vibaya na wamenirudisha nyuma kwenye ujenzi. Damn them
 
Barikiwa ndugu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wakatae vp tena wakati hesabu ziko wazi.....kidogo niwasweke ndani!! mi nimewapa tahadhari coz naamini watu wengi sana washapigwa
 
Nilivyoona Buguruni sikuwa na doubt kwamba hii ni MMU kwani hizo mbao anazozisema nikajua ni wale malaya wanaojiuza(lugha ya picha)...Kazi ya kupima mbao ilipoanza ndipo...nikajua washaingia gesti na jamaa keshaanza kula mzigo,...Mambo ya tape measure nikahisi ile ndimu wanayokamulia kwenye Uuke ikaonekana ndogo kumbe ndani ni bonge la dudu...(lugha ya picha)....Lol kumbe mwishoni ndo nikagundua alichoandika ndo alichomaanisha!!

Kweli Jukwaa kina mata kwa kila sredi...!!

Kwa upuuzi huu ulokujaa kichwani sidhani kama kweli utafikia hatua ya kujenga nyumba yako mwenyewe........:lying:
 
Mkuu hao watu ni hatari sana, na hawako kwenye biashara ya mbao tu bali kila biashara inayohusisha vipimo.

Dada yangu alishawahi kupigwa pale shule ya uhuru, alienda kununua carpets zile za kupima. Aliondoka nyumbani kwake na vipimo na kufika pale shule ya Uhuru kwa wauza makapeti, akatoa vipimo vyake na kukubaliana bei.

Baada ya hapo akajibebea mzigo, kufika nyumbani kapeti halijajaa sebule yote kwa karibu mita 2 hivi.

Tukamshauri achukue askari na wadada wengine wawili wajifanye wananunua carpet duka lile lile, na baada ya kulipia tu ndo yeye na askari watokee kuwakamata wauzaji na tape zao.

Zoezi lilifanikiwa, kumble ile tape pale mwanzoni haianzii na 0, imekatwa kipande cha kama futi 2 hivi.
 
Jamani msikubali kuibiwa pale Buguruni. Mbali ya kutumia vipimo feki, hata mabao zao mara nyingi zinakuwa za kuchovya tu kwenye dawa. Wadau anayetaka mbao imara na kwa bei isiyokuwa na wizi aende pale Mabibo Kiwanda kwenye yard ya Sao Hill branch ya Dar Es Salaam. Wewe mwenyewe utapenda.

Achana na hao matapeli.

Tiba

Thread hii ni very educative. sikumbuki kama na mie walinifanya hivi hivi kwani nilinunua pale pale Buguruni, lakini next time nafikiri kama nitakuwa na muda ni bora nipande basi hadi Mafinga/Sao Hill na kuchukua mzigo wa kutosha then nasubiri Malori ambayo yanarudi Dar yakiwa tupu
 
Utapeli huu unafanyika kwa karibu kila kitu kianchonunuliwa hapa mjini. Aina ya utapeli ndio hugeuka kidogo kutegemea na mazingira.

Kuhusu utapeli katika mbao nadhani buguruni imekubuhu. Ile tape measure huwa wanaiondoa kipande cha karibu futi moja halafu inaungwa, hivyo utajikuta kwa kila mbao unapunjwa futi moja. Na mara nyingi wanajitahidi kukuchanganya ili usishtukie.

Kwenye calculator vile vile huwa kuna namba ambayo iko kwenye memory hivyo wanaweza kukupigia mahesabu halafu wakajumlisha na ile namba iliyo kwenye memory na unakuwa tayari umeshaibiwa. Wana mbinu nyingi sana za kuiba.

Cha muhimu ni kuwa kabla ya kwenda kufanya manunuzi unatakiwa kufanya pre-plan. Ujue kiasi cha mbao unazohitaji, gharama ya kila futi, uwe na walau uelewa wa vipimo vya urefu (kwa mfano kukadiria futi kumi zinafika wapi) na ujue gharama ya mzigo wote utakuwa kiasi gani.

Kingine jitahidi ku-calm down...usiwe na papara, hata wao wakikuona uko makini wataogopa.
Kwa kufanya hivyo walau utakuwa umepunguza ile risk ya kuibiwa na hawa matapeli.
 
Yaliwahi kunikuta pale kibaha!!! Nilkaacha wamemaliza mbao zote na risiti juu!!! Pale pale nikaagizia FUTI KAMBA MPYA na NOTE BOOK!!!
Baada ya kubainika nikaacha mzigo wote nikaenda kwa jirani....naye the same....nikachukia nikaenda kununulia mwenge....wa mwenge akasema usilipe mpaka zifike SITE na zipimwe upya zikiwa SITE!!!

Ili la kupima tena SITE, ni muhimu kwa kweli.. 😛eace:
 
Ndugu zangu,

Hili limenitokea napenda kuwapa tahadhari wale wote wanaofikiria kwenda kununua mbao buguruni wawe makini. Mimi nilikubaliana bei vizuri na muuzaji na kweli mzigo ulikuwa mzuri, pia bei ilikuwa nzuri tena ya kuvutia. Kazi ya kupima mbao ilipoanza ndipo nilipobaini wizi unaofanyika.

Jamaa wanatumia tape measure ambayo ni wizi mtupu.

Nilishtuka kuana mbao ya urefu wa kawaida, tape measure inasoma ft 24, hapo ndipo nilipogutuka nikaanza kuiangalia ile tape measure vzr, kumbe wameruka vipimo ili kuongeza idadi ya futi ili wapate faida zaidi...mfano ile tape measure inasomeka 1, 2, 3, 4, 5, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 17, 18, 19, 22, ......... utaona jinsi kulivyo na gap kati ya 5-10, 15-17, 19-22...

Kwa mwendo huu unakuta jamaa wanaiba futi zaidi ya saba kwa mbao moja. Huu ni wizi mkubwa ukipiga hesa ya 300 kwa kila futi kwa zile mbao ndogo kabisa 2x2, ikiwa ni mbao inayouzwa futi 700/900 utashangaa umeibiwa hela nyingi mno.

Nikaja kuwakamata tena kwenye kujumlisha idadi ya futi zote baada ya kuhesabu mbao zote. Wanatumia calculator abayo ni famba!! yenyewe ikiandika 18.7 haiweki nukta inaingiza number nzima tu, hivyo 18.7 inakuwa 187. Walipomaliza kujumlisha nikashangaa kuona idadi kubwa mno ya futi ambazo ni sawa na hela nyingi mno!! nilipoanza kujumlisha mwenyewe kwa calculater ya simu yangu, nilibaini tofauti (wizi) wa laki tatu kwa mzigo mdogo wa laki 8.

Nimeona niwape hii wadau msijeingia vibaya. Jamaa wanakula kiulaini wasijue tunataabika sana kuitafuta hela ya kujengea...

KUMIMIYAO ZAO ASEE, yaani ningeingia mkenge mbaya! Thanks kwa taarifa hii muhimu, naamini ningekua muhanga wa matukio haya hivi karibuni.
 
Ushauri mzuri kwa wageni wa mambo haya!
Ila kwa sisi tuliochoka kifedha ukiuangalia tu ubao unajua una urefu gani, ubao wa ft24 si mchezo kaka, macho yangu tu ni kipimo tosha! Kikubwa unapoenda kununua mbao nenda na fundi wako, fundi hakosi futi kiunoni!!
 
Asante sana kwa taarifa. Buguruni si sehemu ya kwenda kununua. Lakini vilevile kama mtu anaamua kunua mzigo huko ni bora akaenda na vijana wa3 pamoja na tape measure. Wa2 kuangailia kazi ya upimaji na mmoja mahesabu ya mwisho.
 
hukuwapeleka Polisi?

Ndugu zangu,

Hili limenitokea napenda kuwapa tahadhari wale wote wanaofikiria kwenda kununua mbao buguruni wawe makini. Mimi nilikubaliana bei vizuri na muuzaji na kweli mzigo ulikuwa mzuri, pia bei ilikuwa nzuri tena ya kuvutia. Kazi ya kupima mbao ilipoanza ndipo nilipobaini wizi unaofanyika.

Jamaa wanatumia tape measure ambayo ni wizi mtupu.

Nilishtuka kuana mbao ya urefu wa kawaida, tape measure inasoma ft 24, hapo ndipo nilipogutuka nikaanza kuiangalia ile tape measure vzr, kumbe wameruka vipimo ili kuongeza idadi ya futi ili wapate faida zaidi...mfano ile tape measure inasomeka 1, 2, 3, 4, 5, 10, 11, 12, 13, 14, 15, 17, 18, 19, 22, ......... utaona jinsi kulivyo na gap kati ya 5-10, 15-17, 19-22...

Kwa mwendo huu unakuta jamaa wanaiba futi zaidi ya saba kwa mbao moja. Huu ni wizi mkubwa ukipiga hesa ya 300 kwa kila futi kwa zile mbao ndogo kabisa 2x2, ikiwa ni mbao inayouzwa futi 700/900 utashangaa umeibiwa hela nyingi mno.

Nikaja kuwakamata tena kwenye kujumlisha idadi ya futi zote baada ya kuhesabu mbao zote. Wanatumia calculator abayo ni famba!! yenyewe ikiandika 18.7 haiweki nukta inaingiza number nzima tu, hivyo 18.7 inakuwa 187. Walipomaliza kujumlisha nikashangaa kuona idadi kubwa mno ya futi ambazo ni sawa na hela nyingi mno!! nilipoanza kujumlisha mwenyewe kwa calculater ya simu yangu, nilibaini tofauti (wizi) wa laki tatu kwa mzigo mdogo wa laki 8.

Nimeona niwape hii wadau msijeingia vibaya. Jamaa wanakula kiulaini wasijue tunataabika sana kuitafuta hela ya kujengea...
 
Buguruni wanaloweka kwenye maji ya cement unakuta mbao imekolea dawa kisawasawa kumbe famba.vijana unakuta wanalea vitambi kama mimba za panya kwa utapeli
 
Nahisi ametoka kafura kama nini, akafika na kiupost bila hata kuangalia anapost wapi

Ila kweli mapenzi bila chumba yanakuwa ya tabu sana

Ha ha haaaaa................mapenzi si ni chumbani Da Konie nawe......chumba bila kuezeka inakuwaje!!!!!!!!!!!!!
 
Nahisi ametoka kafura kama nini, akafika na kiupost bila hata kuangalia anapost wapi

Ila kweli mapenzi bila chumba yanakuwa ya tabu sana

Dada we kwa sie akina pangu pakavu..............kujenga ni nusu ya uchizi halafu umbaini mwivi kama kwa bandugu hapo!!!!!!

Ana haki ya kukosea........!!!!!!!!!! Kama namuona akikataa hesabu :nono::nono::nono::nono:
 
maichrim, hao wote na Mafundi seremala, ndio waliochonga Msalaba wa Bwana wangu, Yesu Kristo, Laana yao si kidogo na kamwe hawatajiliki.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom