Mimi nimesumbuliwa sana na Taifodi kwa mwaka sasa.Sasa nimeelekezwa kutumia dawa fulani na rafiki yangu kuwa naye ilimsaidia.Dawa inaitwa RIJAAL.Dawa hii imeandikwa kuwa ni ya kisuna,naomba mwenye kujua tafsiri ya maneno ni ''ya kisuna anisaidie'' ili nielewe tafadhali!!!
Tiba za kisunna maana yake ni ujuzi na utambuzi wa aina mbalimbali za miti vyakura matunda nk
ambavyo vina uwezo wa kutibu maradhi mbarimbari katika mwili wa binadamu pamoja na ujuzi wa kutambua maradhi yanayowasumbua mwanadanu na namna ya kutibu kwa kutumia madawa yaliotajwa ndani ya Qurani na hadithi za mtume MUHAMMAD (swallahu alayhi wa sallamu)
na swahaba zake(Radhiya Allaahu 'anhum).
Mfano asali imetajwa ndani ya Qurani kama chakura bora kuliko chochote na maziwa yametajwa ni kinywaji bora kuliko wakati habbat saudaa yenyewe imetajwa ndani ya hadithi.
Elimu na ujuzi wa tabibu kuhusu tiba za kisunnah ni jambo la kitaaruma kwa maana haiwezekani mtu akawa tabibu bila ya elimu au fani ya tiba ya kutabibu binadamu
Hapa inamaana sio kila muislamu ni mtaalamu wa tiba za kisunna vivo hivyo si kila imamu au ustadhi wa madrasa ni mtabibu na mjuzi wa tiba za kisunnah lah ! Ni kwa wale wachache walojaliwa karama ya utabibu au walofundishwa au kurithishwa ujuzi huo
Na kwakuwa waislamu sisi ni ndugu na tunaaminiana hasa kwa neno lililotoka katika QURAN na Sunnah(hadithi) hivyo ikiwa imetokea moja akapatwa maradhi fulani na akatibiwa na dawa fulani akapona na akatokea mmoja mwingne akapatwa na maradhi ya kufanana na hayo basi hubashiriana kuwa tumia dawa fulani ya kisunna 7bu mimi pia nilisumbuliwa kama hivyo nikapona basi hicho ndicho kilichotokea kwako
MWENYEZI MUNGU anasema katika SURAT AL ISRAA aya ya 81 "Na tunateremsha katika Qur-aan yaliyo ni matibabu na Rehma kwa Waumini"
Muhimu ni kuwa na IMANI na Uzingatiaji wa maelekezo ya tabibu ama uliponunua hiyo dawa au aliyekupa hiyo dawa ni muhimu kwa kufanikisha kupona kwako
Na la mwisho kila unapokunywa hiyo dawa tia nia ikupatie ahueni na umuombe MWENYEZIMUNGU akufanyie wepesi ikutibu maradhi yako
Namimi nina imani na ninakuombea kwa ALLAH (muweza wa yote) utakapotumia hiyo dawa atakufanyia wepesi maradhi yako na utapata SHUFAA