Mnaokaa nyumba za kupanga (shared) fahamu hili

Jamii Forum hakuna aliyepanga.

Humu wote tunaishi kwenye nyumba zetu za ghorofa zilizopo Mbweni,Masaki,Obey na Mikocheni.

Umeme tunaweka wa laki 2 tunatumia mpaka tunasahau.

Huo umeme wa elfu 5 hatukumbuki lini mara ya mwisho kununua.
Kumbe kweli humu JF wote mnaishi dar
 
Jamii Forum hakuna aliyepanga.

Humu wote tunaishi kwenye nyumba zetu za ghorofa zilizopo Mbweni,Masaki,Obey na Mikocheni.

Umeme tunaweka wa laki 2 tunatumia mpaka tunasahau.

Huo umeme wa elfu 5 hatukumbuki lini mara ya mwisho kununua.
Labda atakuwa ni mgeni mkuu!
 
Kuna wenye nyumba ndiyo wanakusanya pesa ya umeme karne hii?

Anakuwa na yeye anaishi hapo au namna gani?
 
unakuta kijana analalamika yeye redio, tv, friji, jiko, pasi anawasha taa tu anataka awe anatoa mchango nusu wa umeme, anajibiwa na yeye akanunue vifaa vya kutumia umeme ili atumie umeme sawa na wenzake la sivyo ahame
 
Kumambuzi wakati naanza maisha sikuwa na vifaa vya kutumia umeme zaidi ya simu tu. Wapangaji wenzangu wana vifaa vingi vya kula umeme masaa 24 halafu mchango wa umeme tunatoa wote. Mjuba ilibidi nikanunue tv, sabufa, jiko, hita, friji, pasi ili nami nitumie umeme vema bila kupunjika.
 
inategemea na eneo unaloishi mkuu. anavyolipia umeme wa masaki ni tofauti na wa tandale kwa mfuga mbwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…