Simao Latino
JF-Expert Member
- Jan 11, 2025
- 477
- 608
Mimi ninakaa Wilaya ya Ilala. Jana nilikuwa Wilaya ya Temeke (mtoni kwa Aziz Ally) nilishuhudia mida ya mchana badala ya mama kuwapikia watoto (watoto walitoka kucheza wakaja kulalamika njaa inawauma) akawapa 500 wote wawili wakanunue bagia na askrimu (ice cream) na ndio imetoka hiyo mpaka Usiku, kulingana na maelezo ya mwenyeji wangu. Sema na mimi nilikuwa majalala, nilibakiwa na nauli tu 2,000, laiti kama ningekuwa na kitu chochote ningeweza kuwaongezea hata 500 nyingine aisee.
Kama hauna pesa ya kumsaidia mtoto masikini, basi mkumbuke hata wakati wa sala au swala.
Daah, uswahilini panatisha wadau, hususan kwa watoto wadogo.
UPDATE LEO JANUARY 28, 2025 SAA 15:50
======
Nimegundua watanzania wengi wanapenda sana kusaidia wenye uhitaji kisha kujitangaza.
Laiti kama ningesema niliwasaidia wale watoto, mngenirushia tena mawe "KWA HIYO NDIO UMEKUJA KIJITANGAZA JF ILI UONEKANE UNA ROHO NZURI??" Hahahahaa wabongo wengi jau sana..