Mnaokata tiketi za mwendokasi acheni kunyanyasa wanafunzi wanaovaa nguo za nyumbani

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Wakata tiketi kwenye mwendo mnanyayasa sana watoto, nimeshuhudia karibu mara tatu mnagombana na vijana ambao ukimuona kwa umri wake kabisa ni mtoto mnataka alipe nauli ya mtu mzima hivi kisa amevaa nguo za nyumbani si sawa kabisa.

Hivi nyinyi amjui umri wa mtoto? serikali naomba iangalie hili kwa ukaribu kwanini watoto wanasumbuliwa, sio kabisa.
 
Ulivoona hayo matukio ulichukua jukumu gani mkuu..? Au ndo kuja kupost humu
 
Sisi mbona enzi zetu tulikuwa tunaonyesha vitambulisho na hakukuwa na tatizo

Hapo cha msingi wawe na vitambulisho na upuuzi wote utaisha
 
Wakata tiketi kwenye mwendo mnanyayasa sana watoto, nimeshuhudia karibu mara tatu mnagombana na vijana ambao ukimuona kwa umri wake kabisa ni mtoto mnataka alipe nauli ya mtu mzima hivi kisa amevaa nguo za nyumbani si sawa kabisa.

Hivi nyinyi amjui umri wa mtoto? serikali naomba iangalie hili kwa ukaribu kwanini watoto wanasumbuliwa, sio kabisa.
huna haja ya kuwalaumu watoa huduma ya usafiri kwani Suluhisho haliwezi kuwa kuangalia umri wa mwanafunzi kwa macho; badala yake tushauri tu kuwa;
Shule zote za Dar wanao tumia mabasi hayo waweke utaratibu wa kuwapatia wanafunzi Vitambulisho rasmi.
Naamini Halmashauri zinaweza kuweka utaratibu mzuri wa kufanikisha hilo hata kama mzazi atachangia kidogo.
 
Wanapaswa kulaumiwa Kwa Kila kitu hao watoa huduma.(UDART)

Hivi mtoto akiwa hana uniform za shule,
Au akiwa hana kitambulisho cha shule,,
Umri wake unakuwa over 30?

Mtoto anaonekana kwa macho hata kama hana kitambulisho..

Wapo wanafunzi wapo high school lakini bado ni watoto under 18.
 
Back
Top Bottom