Mnaokosoa kolabo ya Diamond & Koffi msome HAPA

Mnaokosoa kolabo ya Diamond & Koffi msome HAPA

Masisiemu Sasa ndio yamejua kiasi ambacho magufuli hawaamini.

Yaani kawapa Watoto wake, Na mbuzi za chadema alizonunua mnadani na zile ng'ombe za jalalani udsm pale bila kusahau lakezonelization, watu wa Kanda ya ziwa.

Masisiemu yamepigwa na butwaa
Sio mahala pake hapa
 
Kwa taarifa zisizo rasmi sana ni kwamba ukitaka utajwe kwenye wimbo na Fally Ipupa itabidi ulipie hadi US$1000.
Unamaanisha US$ 10,000 au? Sidhani kama Fally anaweza kumtaja mtu kwa $1000.
 
Katika ngoma za rumba hakuna ngoma mondi atatoa ikawa kali kama ile aliimba na marehemu papa wemba apo ndo ninapojua mziki mzuri una wenyewe ila hii ya koffi na mondi hamna kitu ni kelele tu
 
Katika ngoma za rumba hakuna ngoma mondi atatoa ikawa kali kama ile aliimba na marehemu papa wemba apo ndo ninapojua mziki mzuri una wenyewe ila hii ya koffi na mondi hamna kitu ni kelele tu
Kweli. Ile hata tuzo ilipata. Papa Wemba kolabo zake karibu zote ni hitsong, kuna Wakeup ft Koffi, cavalier solitaire ft mpiana ,, zilisumbua sana.
 
Koffi kuimba vile n kawaida yake,ila mashairi au namna alivyoimba diamond hata Mimi naweza imba
 
Unamaanisha US$ 10,000 au? Sidhani kama Fally anaweza kumtaja mtu kwa $1000.
Nani atoe $10,000 kutajwa na Fally kwenye wimbo!? Kwani amekuwa na hadhi ya marehemu Michael Jackson huyo!? $500 mpaka $1000 anakula vizuri tu.
 
Nani atoe $10,000 kutajwa na Fally kwenye wimbo!? Kwani amekuwa na hadhi ya marehemu Michael Jackson huyo!? $500 mpaka $1000 anakula vizuri tu.
$500 labda kwenye live show akiwa ameshalewa ila sio akiwa anakwenda kurecord wimbo wake ambao unaweza kuhit na kuwa juu kwa miaka zaidi ya 20 huku wewe ukitajwa tu

Hao akina papa Moise Katumbi Chapwe anaowataja kwenye nyimbo ni mabilionea hasa na sio watu wa kutoa $500
 
$500 labda kwenye live show akiwa ameshalewa ila sio akiwa anakwenda kurecord wimbo wake ambao unaweza kuhit na kuwa juu kwa miaka zaidi ya 20 huku wewe ukitajwa tu

Hao akina papa Moise Katumbi Chapwe anaowataja kwenye nyimbo ni mabilionea hasa na sio watu wa kutoa $500
Ukishasema Moise Katumbi huyo ni mtu ambaye hategemei kulipa kwa ajili ya kutajwa na Fally huyo automatically fally ataona fahari kumtaja kwa kuwa alishakuwa mkubwa na mwenye influence kabla hata Fally hajatoka kumtumikia Koffi, ni hulka ya wacongo kuwataja ma_role model kwenye nyimbo zao. George Weah Waka Waka mfano mmoja wao. Wanaolilia fame ndio watalipa kwa kuwa hawafamiki ,
 
Natumaini mko wazima. Kwanza nimshukuru Mungu kwa neema zake. Pia nitoe pole kwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kwa kuingia mgogoro na wanachama wake nguli waliokipigania kwa muda mrefu. Siwezi kuongelea hilo hapa ila tambueni msimamo wangu ni kama wa Mh Ndugai na Mh Polepole. Leo nitaongelea suala la huu wimbo wa Komredi Diamond Platinumz akishirikiana na Koffi Olomide (Mopao Mokonzi). Kiukweli wimbo ni mzuri wenye viwango vyote vya kimataifa. Binafsi niseme kada Diamond kakiletea chama heshima na taifa kwa ujumla. Bendera ya chama na taifa kazipeperusha vyema.

Lakini wakati wengi tunasifia kuna baadhi wameibuka na ukosoaji ambao leo nimeamua kutolea ufafanuzi. Mambo yafuatayo yameibuka;

1. Koffi kazingua kutoimba.
2. Alichofanya ni kutaja majina tu kitu ambacho hakina maana.
3. Diamond kaimba mashairi dhaifu.

Mambo mawili ya mwanzo nitautolea ufafanuzi kwa pamoja, Koffi kutoimba na kutajataja majina. Ikumbukwe taratibu za muziki wa kikongo zina utofauti kidogo na Bongo Fleva. Kule wanamuziki huimba LIVE na band. Na kwa taratibu zao huwa ndani ya bendi kuna watu wanaitwa marapa/Animators/Atalaku ambao kazi yao ni kuimba kwa sauti kama za kupayuka pale sebene la kwenye wimbo linapoanza. Wasiojua muziki wa congo ni kwamba nyimbo zao zote huanza kwa kuimba na baadae kufuatiwa na sebene ambapo hao marapa huanza kuimba. Na karibu hit songs zote za Congo huanza na sebene mwanzo mpaka mwisho. Hivyo basi huwezi sikia mwanamuziki mwingine zaidi ya rapa wa bendi akiimba kuanzia mwanzo hadi mwisho wa wimbo. Koffi Olomide kama ilivyo kwa wamiliki wengine wa bendi congo kina JB Mpiana, Werrason, Fally Ipupa na wengine huwa sio rapa. Sio rahisi kuwasikia wakifanya kazi hiyo. Zamani kwenye albamu zake za mwanzo kama V12, Koffi alijitahidi kufanya Animations hata Fally Ipupa kwenye Bakandja alipambana. Tukirudi kwenye point ni kwamba wimbo wa Diamond ni kama ulikuwa sebene mwanzo mwisho hivyo kwa Mopao ilikuwa sawa kabisa kubaki kwenye utaratibu wake ili kuleta ladha kamili ya Mopao.

Sasa kutokana na Koffi kutoimba kwenye hizo hitsongs huishia kuwa back vocalist ambapo huimba kwenye viitikio ambavyo Animator atawaimbisha. Na jambo lingine ambalo hulifanya ni kutaja majina ya watu au makampuni. Hapo kwenye kutaja majina tuangalie kitu kiitwacho MABANGA.

MABANGA ni nini? Huu ni utaratibu wa kutaja majina ya watu kwenye nyimbo kwa malipo ya kiasi fulani cha pesa. Kwa taarifa zisizo rasmi sana ni kwamba ukitaka utajwe kwenye wimbo na Fally Ipupa itabidi ulipie hadi US$1000. Lakini ukiachana na Mabanga ni kwamba kutaja majina huleta ladha fulani nzuri kwenye nyimbo zao. Pia majina mengine hutajwa tu bila kulipiwa. Kwenye wimbo wa Diamond Koffi kataja majina ya familia yake. Ni ngumu kwa wimbo wenye mahadhi ya kikongo kutokuwa na hivyo vionjo vya kutaja majina. Diamond kafanya vyema kwenda sawa na nini wananchi hasa wacongo wanataka. Kibiashara iko sahihi.

Kuhusu Diamond kuimba mashairi mepesi ni hoja ya kupuuzwa na wapenda maendeleo wote. Muziki ni hisia zako tu. Kama wimbo haukupi hisia za kuufurahia achana nao haukuhusu. Kwa mfano hitsong FIESTA ya R Kelly una maana gani? Thong song ya Sisqo una maana gani? Fagilia ya Mr Nice je? Lakini zote zilitikisa ulimwengu. Cha muhimu ni kwenda sawa na BASATA huku ukigusa hisia za wateja. Nihitimishe kwa kuwataka kama taifa tumpongeze Diamond kwa kazi kubwa anayofanya.
Kuna wimbo mmoja nikiwa mdogo na sijui Kiingereza nilikuwa naupenda sana. Kabla movie kuanza kwenye kibanda umiza tulikuwa tunaomba upigwe kwanza. Siukumbuki jina wala aliyeuimba, ila nakumbuka mashairi yalikuwa yanaanza na,

"Who let's the dogs out...!"
Wooh! Wooh! Woooh! Wooooh!
Utakuta aliyekuwa anaupenda wimbo huu kama mimi ndiye anayeuponda wimbo wa Diamond na Koffi! Ahahahahahhahahah!
 
Diamond nampa hongera sababu anajituma na Ana uthubutu. Ila kwenye huu wimbo pamoja na kofi hajaimba, lakini amemfunika diamond Sana Sana. Ila kwenye kucheza dangote wetu yupo vizuri.
Hivi diamond analipwaga na Aliko dangote kumtajataja kwenye mawimbo??
 
Nitaitwa hater ila huo wimbo wamepiga boko connection kati ya Koffi na Diamond haipo kabisa utaikiri nyimbo mbili tofauti
 
Back
Top Bottom