Mnaokwenda kushuhudia ngao ya jamii kesho, salamu zenu hizi

Mnaokwenda kushuhudia ngao ya jamii kesho, salamu zenu hizi

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Kwanza tambueni mm ni mkongwe sana wa gemu za Simba vs yanga, nimeanza kwenda uwanjan miaka ile ya Derby ya Sigara na Pilsner, Simba na Nyota Nyekundu ya Roster Ndunguru, Simba ile ya akina Itutu Kiggi, Mosses Mkandawile, Sunday Juma, Aston Pardon, Adam Seleman, Juma Limonga, Adolf Kondo, Omary Hussein Kevin Keefan.Kwahiyo naujua mpira wa bongo coz nimeuishi had Leo.

Natoa tahadhari kwa wale wenye roho nyepesi, nyepesi wakae wakijua yafuatayo hiyo kesho ambapo sare haipo, lazima mmoja alale na maumivu.

1.Mechi za Simba na Yanga hazina mwenyewe, yeyote anaweza kufungwa
2.Mechi za Simba na Yanga zimeshachezwa na watu wana matokeo.
3.Mechi za Simba na Yanga sio uwezo wa makocha wala wachezaji, ni majini tu yanatamba.
4.Shabiki yeyote akijichanganya kwenye ndumba za wanaume hao anaweza kutolewa kafara.
5.Wachezaji wengi maarufu wa timu hizo majina yao yako makaburini usiku huu yanafukiwa.
6.Viongozi wa timu hizi wanawapa matumaini ya bure ila mchezo ni dakika 90.
7.Mnaoumia ni nyie mashabiki, wenzenu hawana maumivu yoyote
8.Mechi itaisha kwa sare dakika 90
9.Kama moyo wako hauwezi kutuliza damu tulia nyumbani
 
Ahsante kwa ushauri, haya wee ni shabiki wa Team gan???
 
kwa mujibu wa jini kuu la baharini na nchi kavu muheshimiwa Makata bin Subiani kesho Simba atapewa ushindi wa kutikisa Dunia na huyu kiumbe mtata.
 
Mechi ni sare 90' simba wataibuka kidedea kwenye matuta na jezi watavaa nyeupe.

Nipo ndotoni nikiamka nitasimulia.
 
Hizi ni story za miaka ya 47 huko ambapo soka yetu ilikuwa gizani, kwa sasa hazina mashiko mpira wa sasa ni sayansi ambeye atafanya homework yake vizuri ndiye atakeahonda game ya leo.

Zamani timu ziliwekeza sana kwenye ulozi lakini hakukuwa na maendeleeo yoyote, mimi nakumbuka enzi hizo tulienda kwa mganga tukapkwa mafuta ya nguruwe timu nzima iwe waislam wote tulipakwa, matokeo tulipigwa goli 5.

Zamani timu zilikuwa zinaajiri waganga kabisa, Yanga mganga wao alikuwa Bagamoyo timu ilikuwa lazima waende Bagamoyo kukiwa na Derby , wachezaji walikuwa wanaenda Bagamoyo wanalala Kiromo hoteli, Mganga anakuja pale wanafanya mambo yao lakini hakuna maendeleo yoyote waliopata.

Mpira wa sasa mambo hayo hakuna aliye bora kwenye technical bench ndiyo anafanya vizuri.

Mimi huwa siamini msemo wa game ya simba na yanga haina mwenyewe, hiyo sio kweli, tukumbuke kipindi Yanga ilikuwa kwenye ukata ambapo walishindwa kuwa na kikosi bora, Simba waliinyanyasa sana Yanga, Msimu ulioisha pia hawakuwa na kikosi bora sana kuliko yanga, yanga waliwafunga simba.
 
Back
Top Bottom