Mnaombeza Prof. Ndalichako, amesoma PhD University of Alberta Canada

Prof. Ndalichako, kwa aliotufundisha Statistics Udsm, tunaujua umuhimu wake na Madini kichwani aliyonayo.
 
hata angeenda uni of
hata angeenda Univ of mbinguni tungembeza tu kwamba hajui kiingereza, tena kwa huu uzi wako ndio umemuharibia kabisa maana mtu unakaa marekani alafu unashindwa kuunda sentesi za kingereza
mimi naona Deo kisandu yupo vizuri kwenye kimalkia kuliko ndalichako, yani mtu tumempa dhamana ya wizara yenye jukumu la kuhakikisha wtoto wanajua English lakini yeye mwenyewe hajui !!
 
Mama kasoma Hesabu hizo English mtamuonea tu, namba unaongea kinambanamba huwa haja ya kutembea ngeli
 
Professor ndalichako awaambie watanzania kile kitabu cha historia ya Tanzania kiliishia wapi, maana aliahidi kwamba kitaanza kutumika jul. 2021.
 
Jambo kwangu kwakwe sio Kiingereza chake, bali uwezo wake wa uongozi, SIjawahi kuamini kuwa Elimu kubwa ndio uongozi bora na kila siku zinavyokwenda hili jambo linaendelea kujiprove
 
Tatizo pale ni "Accent"ila English yake inaeleweka.

Kwa mfano badala ya good yeye anasema gudi.
 
Labda Canada ya kasuru
 
Kule Kenya machokoraa yanabonga kingereza safi kabisa
 
Labda walimuhurumia tu.

Hamjui kitu. Andiko unaandika na lugha inarekebishwa kwa kuwa Ni scientific work. Defence inategemea na somo. Unaandaa Pia na kupresent. So still lugha yako inarekebishwa. Kwenye maswali Sasa ndo inabidi uteseke Lakini kwa uzoefu Wangu magiiiiniiiaaas wengi lugha hasa wa science lugha haijawahi kuwapenda. Maprofessor huangalia na kusikiliza content. Maneno mengi huwachukiza na kuona huna points.

Kumbukeni Kiswahili ndo lugha yetu. Hao wanaijeria na wengine wanatoka kwenye makabila to English.
 
kiingereza Cha nn bana,tunachotaka umeme usikatkekatke hii tabu tuliisahau enz na jiwe,tunachotaka bwawa la mwl. likamilike,SGR ikamilike,vituo vya afya vikamilike.hayo ndo muhimu kwetu ss, kwanza ikiwezekana aongee hata lugha yake ya kjjn kwao !!,tunataka maisha Bora,sio wakae kwenye mavi 8,halafu wananchi wanalalamika usumbufu wa umeme ,n.k.
 
Mode of communication na jamii ya chuo ilikuwa mathematics? Do you have to school to know a language? Chuoni aliishije na wanafunzi wenzake hakushiriki majadiliano ya roundtable na wenzake? Wamishonari walisoma vyuo gani wakajua kisukuma na kihaya?
 
Ficha upumbavu wako... post graduate kupata nasafi popote duniani hata Havard hakuna cha ukipanga ni mshiko wako tuu....


Angesoma hapo bachelor ingekua habari nyingine.
 
Vipi kuhusu maprof wa Kihindi wanavyo ongea
Vipi wa Kinaijeria
Kweli Bongo nyoso tembea muone
Hao wanajua lugha ila matamshi yameharibiwa na lugha za asili. Ndalichako hajui sio kwamba ana matamshi ya Kiswahili kwenye English. Unaanzaje kumtetea Prof. anayesema "aah, we, we political will by ensuring that we we we....."
 
Nchi hii haijawahi Kuwa na waziri wa Elimu bora na mbunifu zaidi ya marehemu Jackson Makwetta nae hakuwa na Ph.D!!!! What is important therefore is the performance and vision of an individual.
Makweta commission naikumbuka

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Kichwa cha mtu Mimi nmesoma kata na Niko competent kizungu

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ok..kwahiyo alikuwa Canada 1993-1997...alikuwa anaongea nini na wanafunzi wenzake?..anyway, utetezi unakuwa mgumu tu ata mimi nataka kumtetea lakin nashindwa
 
OK, ni mtaalamu nguli wa mambo ya mahesabu na statistics......kitu ambacho wanawake wengi hawawezi na unaweza kukuta wanaoponda wengi humu ni wanawake. Kwa wasomi wengi wa masomo ya sayansi kufanya academic writing and presentation siyo tatizo kwao, ila kuongea kiingereza katika mazungumzo ya kawaida ndo inakuwa shida kwa sababu mazungumzo ya kawaida yanatumia maneno common ambayo yanatumika mitaani na hivyo yanahitaji exposure ya kuyatumia zaidi kwenye mawasiliano ya kila siku.
Wakati nafanya PhD yangu ulaya wale supervisor wangu walikuwa wanasema naeleweka vizuri kwao nilipokuwa najadiliana nao kuhusu progress ya masomo yangu ingawaje kwangu mimi nilikuwa nahisi kiingereza changu hakikuwa perfect sana.
Kwa hiyo ni upuuzi kutumia muda mwingi kujadili swala la kiingereza cha waziri utafikiri kwa mazingira ya Tanzania kuna mtu anaweza kujigamba kutema yai kama mtu aliyezaliwa na kukulia London......​
 
Sawa ndarichako tumekusikia..ila bado wewe ni kilaza tu kwenye lugha ya malikia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…