Mnaonaje sisi twende Sudani ninyi mcheze na De Agosto?

mugah di matheo

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2018
Posts
6,307
Reaction score
12,410
Baada ya Simba kumfunga De Agosto yameibuka maneno yanayosema De Agosto ni mdhaifu kuliko Al Hilal. Sasa naomba ufanywe mpango utopolo wacheze na De Agosto nyumbani na Simba wakapambane na Al Hilal.

Unadhani utopolo atafanikiwa kuingia makundi?
 
Kwani hao Al Hilal si ndiyo waliwafunga nyinyi goli 1-0 mwezi uliopita! Subirini kaka zenu wakawafutie aibu yenu.
 
Mkuu unasahau kuwa hii mechi zote mbili zilipigwa pale chamazi kutokana Na uviko 19 ??? Utalinganisha Na Sasa hivi
Lakini pia zaidi ya wachezaji 10 wa kuaminiwa waligundulika kuwa na corona hivyo kuzuiwa kucheza!! Hivi wachezaji watano tu tegemeo wa yanga wakizuiwa kucheza jibu unalo mwen yewe!! Jiandaeni kubeba kapu la magoli huko ugenini!
 
Hao ndiyo wanao wafaa nyinyi. Wacha sisi tukacheze na wababe wenu walio wafunga wiki chache tu zilizopita kule Sudan.
Mtakapopigwa khamsa msiseme hatukuwapa msaada. Nendeni mkijua ni kuanzia goli 3 had 5 mnabugizwa. Hapa waliwakosakosa mnajiona mna timu.
 
Mtakapopigwa khamsa msiseme hatukuwapa msaada. Nendeni mkijua ni kuanzia goli 3 had 5 mnabugizwa. Hapa waliwakosakosa mnajiona mna timu.
Labda Profesa avurunde tena kwenye upangaji wa timu kama alivyofanya kwenye mechi iliyopita. Kinyume na hapo, Yanga ina kikosi imara sana tu msimu huu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…