Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Nawala siri moja katika mafuta

Mafta yana tabia ya kusinyaa na kutanuka
Wakati wa joto mafta hutanuaka na wakati wa baridi mafta husinyaa
Hivyo basi kwa ww unaetaka kununua mafta nakushauri nenda sheli wakati joto limepungua yaani ucku

Kwahyo unaweza kupima mafta kwenye joto ukaona meng lakin ukienda ukanda wa baridi mafta yako yatapungua
 
Ogopa Oilcom pale kwa Aziz Ally Temeke!ukiweka ujue nusu kwa nusu!ukiwa ya elfu 20 ujue elfu 10 umewachangia
 
Naomba kwa waelewa mnisaidie ufafanuzi, hawajamaa wanajaze upepo ilhali ukiwa ndani ya gari gauge ya mafuta unaona inapanda wakati wa kuweka mafuta na ukitazama meter ya pump ya mafuta inakuwa ikisoma pia?? Naomba ufafanuzi kwa wanaoelewa namna wizi unavyofanyika ili next time nijipange sawasawa ninapoenda petrol station.
 
Pole wale ni hatari mno kuna siku minikifika nkawaambie waniwekee mafuta waset tu waiche mashine yenyewe bila kushika ooo hauifanyibkazi nikiiachia mafuta hayaingii nkamwambia basi nkasepa...
Nlifundishwa haka ka ujanja kwamba ukifika shel usikubali washike ile mashine wakisha set tu waiachie vile wakishika nakubinya binya wanaingiza upepo.
Yani Nina wiki mbili nalalamika mbona mafuta yanaisha haraka sana lohhh yani had ilibidi niwe nacheck labda tanki linavuja..yani hali mbaya..nimechange vituo kama kumi, ila nilipojaza Victoria sijapata shida
 

Hapa hata mimi waliniliza siku moja. Niliwaambia waniwekee ya elf 30, yule dada kabla hajaanza kuweka akaniambia nizime gari, nikazima. alipomaliza akanipa na risiti ya TRA nikawasha nikaondoka. kufika Kumekucha taa bado ni nyekundu nikarudi pale nikamwambia dada hujaweka mafuta. Tukabishana kweli kweli hadi kumuonesha taa bado inawaka akajiapiza kaweka. kumaliza ubishi nikamwambia weka tena ya elf 30 ila sizimi gari. Kuweka mshale ukapaa hadi robo tank na nikamwambia dada umeshuhudia? akaendelea kujiapiza aliweka. Ikabidi kumuacha na kuondoka, sijarudi tena pale!
 
Oil com wamenila juzjuz yaan niliendesha kwa hasira sana
Oil com wanaiba na hayo unayowekewa ni machafu...nilishauwa nozzles kwenye gx110. Gari ilikua fresh ila baada ya kuweka tu nusu tank..check engine light ikawaka.
 
Niko pamoja na wewe kabisa juu ya uloyosema
 
Kuna cku jini likaniishia mafuta mitaa ya mbezi,nikaomba kidumu kwa jamaa wa boda boda,nilipoenda petrol station na kidumu,nikaaambiwa meneja aruhusu kununua mafuta kwenye kidumu,ikabidi niwe mpole
Ni kweli hawaruhusu skuizi kwa kisingizio unaweza kumchoma mtu moto ikawa kesi
 
Wezi wakubwa ni Oil com hilo halina ubishi kuna ile shell yao ya manzese ndiyo hatari zaidi,
Shell ambayo huwa najaza mafuta na roho huwa safi bila wasiwasi nawashauri nendeni shell za VICTORIA popote pale jamaa wapo vizuri sana kuanzia quantity hadi quality ya mafuta.
 
Hahaha! Mazoea tu hayo ya watanzania ila hakipo.Nadhani Shell walikuwa ndio wakwaza kuanza kuuza mafuta kwenye soko la retail, so watanzania wakajikuta wanazoea hilo jina na ikawa kawaida kwa watu kuita jina la kaampuni ya Shell kwa kila kituo.
Kama ilivyo pempers, kumbe kuna hugis, Molffx, sleep, nk, ila watu wanaita zote pempers.
 
Huyo dada ndio tabia yake ila kituo kimenunuliwa na ORYX pale kwa kopa cha ajabu yule dada bado wamemuajiri tena pale pale alishawahi kunibia mafuta yangu akaniharibia siku ni mwizi hatari.
 
Victoria na ENGEN ni waaminifu sana, ila hawa wenzetu wajanjawajanja inapaswa ukiwa unawekewa mafuta ushuke nje kabisa na usiruhusu awe anaminyaminya pump.
 
The way ile mashine inavyohesabu kiwango cha fedha/fuel unaweza kupata idea pia kama wamecheza na machine ama vipi. Juzi nimejaza mafuta station ile pale kwenye roundabout ya kuingia mlimani city. Mashine ilikuwa inahesabu taratibu sana huku wese likiingia tofauti kabisa na sehemu nyingi ninazowekaga mafuta. Mafuta ya 70,000 kidogo tank la Kluger lijae kabisa.

Yaani nilichokiona nimeamini pale hawapigi sana. The higher the rotation rate the higher the possibility upo unaibiwa. Siku ukiwaambia wajaze full tank ndo utashangaa IST imebambikiziwa kesi ya kunywa lita 70
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…