Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Mm niona hapa mnalalamika tu sijaona anayethibitisha namna wizi unavyofanyika, anayejua jinsi wizi unavyofanyika atujuze. Pia kama unajua oilcom wanaiba kwanini unarudi tena kujaza mafuta hapo? Kama ni mwizi asusiwe.

We na wewe hujielewi. Unasoma comments za watu kabla ya kuComment? Kwa mfano huoni nilivyoComment mimi hatua nilizochukua? Sidhani kama kuna hata mmoja aliyeibiwa na akaendelea kununua mafuta kwao bila kuchukua hatua za kujihami au labda umesoma comments za nani aliyelizwa mara mbili au tatu bila kuchukua hatua?
 
Shell nao walishafunga biashara zao Tanzania kabla hata kikwete hajaingia madarakani. Ila wabongo ukitaka kuongea kuhusu hivi vituo vya mafuta ili wakuelewe kwa haraka zaidi sema shell utaeleweka ila ukisema sijui petrol station utawaacha njia panda wengi sana.
Samahani lakini
Petroleum station [emoji579] =Fuel Station [emoji618]
Ivi vitu ni sawa au ndio yale yale shell au?
 
Hii inaonekana sana.kuna wizi mkubwa sana kwenye mafuta ya sheli apa mjini
Adi inafikia mda mtu unatamani uichome sheli moto
Na pia ni sheli gani hazina wizi huu na nini kifanyike

Karibuni kwa mahojiano mazurmazur
Badilish heading na content mkuu. Ukitaja Shell ni sawa na kutaja pempaers ya sleepy. Hapa namaanisha kuwa Shell ni jina la kampuni kama ilivyo Oil com au Camel oil. To a neno Shell na weka fuel station au kituo cha kujazia mafuta
 
Oil com wako juu sana kwa kupiga, kuna wale wa pale mpakani njia ya kwenda Mwenge dah waliwahi nipiga mkapa leo sijarudi tena hata kama gari linawaka taa for the whole day sipitii hapo. Engine wako poa sana na wale wa victoria
 
Mmmh hichi kituo cha mafuta kinachoitwa shell kipo maeneo gani kwa dar
Kuna products zimekamata au zilikamata soko hadi soko la products hizo linaitwa kwa jina lake.. mfano
1. Shell ikimaanisha kituo xha mafuta
2. Bukta, ikimaanisha kaptula
3. Kiwi ikimaanisha dawa ya viatu
4. Unakumbuka maswali kama una mobitel yako? Au kwenu kuna ITV?
5. Bic akimaanishwa kalamu
6. Hata colgate walifikia kiwango hicho

Etc
 
Hivi wanaibaje?

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kituo cha mafuta pale mlimanj city wanaiba mafuta usiku,hasa hichi kipindi cha sikukuuu jana limenitokea na nili waambia wakawa wanasema gari gauge yangu itasoma tuu sikuhitaji kubishana sanaa niliondoka maana najua kabisa wameiba na niliwaambia mlicho fanya sio vizurii

Uaminifu ni kitu muhimu sana sidhani kama nitaenda pale na nikienda siweki gari natoa kidumu na nita waambia kuna mfanyakazi alisha niibia mafuta hii sheli kwahiyo siwaamini tosha!
 
Kuna sheli moja jina kapuni kila Nilikuwa nikienda kununua mafuta lazima waniibie sasa hv nimeamia sheli nyingne yaaan nikinunua mafuta ya taa lita moja yanaweza pikia siku tatu.
Tunao tumia vyombo vya mafuta tuweni makin sana tunapoenda sheli
 
Dah...siku kilihappen zilipoingia Lita 120 kwenye tank lenye ujazo wa lita 100 lililokuwa robo tank kabla....wadada wa BP walinipenda ghafla...nilipewa mabusu makali...hasira zangu zikatulia[emoji13] [emoji13]
Npo napata chai apa kwa rohombaya
 
Petrol station yoyote ukikuta kuna waudumu wa jinsia ya kiume, wamenyoa mapank fahamu hapo lazima upigwe. Oil com karibu na Airport ni noma, usijaribu usiguse. Pump moja ina waudumu 3!! Na wote wamekaa kiwizi wizi.
Hahahahaha mzazi imetisha wachangamfu balaa pale sijui na madalali wapo
 
Huu wizi upo sana hasa kwenye vituo vya oilcom, kuna sheli ya oilcom nilijaza siku moja mafuta ya elfu 30 taa haikuzima wakati siku zote huwa naweka ya elfu ishirini na taa inazima, ikabidi nimuone manager wao wakaniongezea mafuta cha ajabu hakuwakaripia wale waweka mafuta, nilijafanya kama afisa wa tra kumbe mkulima wa nyanya na vitunguu.
sio kwamba namharibia biashara, ila ukweli shell za oil com huwa sijazi mafuta. vituo vyangu ni TOTAL nikibanwa sana puma. hao wengine nikiwa sina namna huwa nashuka hata kabla hajaset, namwambia asishike pump aiache iende yeneywe na ninaangalia adi mwisho ndo nalipa na kuzunguka kwenda kuingia kwenye gari.
 
Aisee
hizi BP za sheli ni noma
Na sheli za oilcom nao ni majanga
 
Back
Top Bottom