Mnaongeleaje wizi wa mafuta sheli, yaani kujaza upepo?

Leo nimejaza victoria
Asee kujaza pale adi raha
Yaan ata kwa muonekano wale wa2 hawana habar na wizi
Pili unajaza fair kabisa adi roho inafrah
Yaan hawana ata chembe ya wizi
Ndo maana gar zinajaa pale kujaza
[emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8][emoji8] to victoria
 
Mkubwa DAWA ni kujaza full tank yana mwagika unasoma mita kiasi gani unadaiwa unalipa.Na unachotakiwa kufanya ni kutafuta mtaji wa full tank first time, baada yahapo usisubirie hadi yaishe unakuwa unajaza kila unapo enda safari hutaibiwa Na Sheri yeyote
 
kuwa makini unapoingia sehemu ilipotoka bodaboda au bajaji,maranyingi hawa wanajaza mafuta hayazidi elfu tano kwahiyo wewe ukija ukitaka ya elfu ishirini wanapandishia kuanzia elfu tano mpaka elfu ishirini,unakuwa umeibiwa mafuta ya elfu tano.
 
dawa ni kujaza tank zima unakaa mwezi koz unajua kabisa gari inaingia lita ngapi,,,mengine yote mnajifariji ,,na unatakiwa kununua mafuta asubuh na mapema
 
BP sinza ni hatari. Especially ukiweka mafuta mda wa usiku.Chukueni tahadhari
pale ni balaaa.....nishawahi kuweka mafuta ya buk 20 kufika biafra kino taa nyekundu ikawaka na siku hyo hakukuwa hata folen barabaran
 
mi walinambia geji yangu ni mbovu
 
BP Chuga ni shidaaa pia msisahau mkienda kuosha magari kodoeni macho kodo wanavuta petrol kwa mirija
Mm huwa namuita muosha gari tunapiga picha gauge ya mafuta na km, afu namuachia funguo nikirudi tunalinganisha na picha ndo namlipa.
 
Huu wizi upo sana hasa kwenye vituo vya oilcom, kuna sheli ya oilcom nilijaza siku moja mafuta ya elfu 30 taa haikuzima wakati siku zote huwa naweka ya elfu ishirini na taa inazima, ikabidi nimuone manager wao wakaniongezea mafuta cha ajabu hakuwakaripia wale waweka mafuta, nilijafanya kama afisa wa tra kumbe mkulima wa nyanya na vitunguu.
 
Jana oilcom ubungo wamenidukua, hii mara ya tatu sasa. Mashine yao inasoma kiasi nilicholipia ila mpaka nafika mjini gauge bado iko chini. Leo nmeenda shekilango Total kiasi kile kile cha jana gauge fasta imefika nusu. Sidhani ka nitakuwa na biashara na hawa jamaa tena.
 
Kiukweli Oilcom sijui wana shida gani? Mi juzi kuna kituo chao cha Boko magengeni niliweka ya 10000 ktk Opa jioni lakini nashangaa taa ya empty bado inawaka mpaka kesho yake asubuhi natoka home. Ninachofanya sasa hivi ni either kwenda na kidumu au kwenda kituo kingine kilichopo msikitini. lakini Oilcom washanichosha. Victoria service station wapo vizuri wana reputation nzuri sema tu hawajasambaa sana mjini ningekuwa ninatumia huduma zao tuu bila kuwa na shaka. Engen nao sioni kama wana shida.
 
Mm niona hapa mnalalamika tu sijaona anayethibitisha namna wizi unavyofanyika, anayejua jinsi wizi unavyofanyika atujuze. Pia kama unajua oilcom wanaiba kwanini unarudi tena kujaza mafuta hapo? Kama ni mwizi asusiwe.
 
Kwani ukiwekewa mafuta ya sh kadhaa unashindwa jua geji yako itapanda vp?
 
Ukishaona kituo cha mafuta wanakataa kidumu, ujue mashine zao zimesetiwa kuiba
 
Pale mlimani city wapo vizuri sana. Sijajua kwa apa Kimara Baruti(Dar es salaam Tanzania). Wao Awapigi upepo kweli
 
Jinsi wanavyoiba....huwa hawazimi pump...na ufikapo hukuambia sogeza gari mbele ili usione kama pump inasoma zero zero.
Hakikisha pump inasoma zero zero kabla hajaanza kukuwekea mafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…