GE2025 Mnaonong'ona muelewe katiba sio biolological in nature

GE2025 Mnaonong'ona muelewe katiba sio biolological in nature

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

anthopody

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2024
Posts
262
Reaction score
183
Niliwahi kuandika humu nikasema kuwa katiba haikutokana na genetic factor,bali katiba bora lazima iakisi mazingira yaliopo,povu zikawa nyingi,nikatolea mfano wa PK.

Demokrasia mnayoipigia chapuo mlio wachache ni ile tuliokaririshwa na kurithishwa miaka mingi iliyopita lkn leo kuna sehemu haiingii hata tafsiri ya demokrasia leo imebadilika kulingana na mazingira

Kwenye mfumo wa demokrasia ya leo bado tunaendelea na uwakilishi kwa niaba ya sauti ya wengi sababu kadhaa ya dhana hii zipoje lukuki japo sio lengo kuelezea,hivo tunapokuwa na uwakilishi katika maamuzi dhana hii inaathiriwa na suala la udhamini na athari zake katika jamii na imekuwa jeraha huwezi kulitenganisha na ndio mazingira ya sasa.

Mdhamini ni mtu mwenye uwezo na ndie anayesoma mazingira yaliopo na kubadilisha upepo kuweza kuendana na kasi ya mazingira yaliopo.

Dhana ya reforms katika katiba limekuwa chapuo na ndio siasa za kikanda zilizoibuka hivi punde katika mifumo ya kisiasa na mabadiliko yake tukishuhudia Trump na mabadiliko ya kisera,PK na mabadiliko ya katiba kwa kutumia sauti ya wawakilishi kuweza kuwasemea walio wengi-hii yote ni siasa na demokrasia katika mazingira ya sasa Ili kuendana na ukuaji wa uchumi.

Zamani wabunge wa makundi maalumu waliokuwa hawapigiwi chapuo sana,dhana ya kujali watu hao haikuwa inatiliwa mkazo lakini leo hii tunashuhudia hadi Mkt wa chama ni kundi maalumu,wapo wengi wamepewa fursa kama mnakumbuka visa vya Idd Amina wa Uganda kusema kuwa si wazalishaji na kwenda kuwamwaga katika mito na vyanzo vingine vya maji yote hii ilikuwa demokrasia ya wakati huo-lkn Leo hii Tanzania chini ya SSH na CCM kwa miaka yote imekuwa ikisikia kilio cha wananchi wake kupitia uwakilishi na kuzisikiliza sauti hizo kwa ufasaha na kuziwekea mikakati ya utekelezaji.

Hii ya katiba ndani ya CCM ni takwa la mazingira ya sasa amabao limechagizwa na shauku ya wengi kupitia wawakilishi wao na watu wamewekewa asali wanalamba midomo tu sasa na tunasubiria kutick October

Mabadiliko haya yanachochewa na mazingira ya sasa ambapo ukuzaji wa uchumi ni kipaumbele chini ya dira ya taifa ya 2050 kuelekea Tanzania ya maziwa na asali kwa kila mtanzania pasi kujali tofauti zozote kwani tu wamoja.

Mabadiliko haya yametiwa chachu na uhitaji wa wananchi kwa kuona sasa Tanzania walau kisiasa tupo mbele na siasa yetu safi sasa tuhamie kwenye uchumi Ili kuendelea kuwawekea wananchi fursa za kiuchumi lukuki tena lukuki zaidi Ili kupaisha Pato la taifa hadi 2050.

Hii ndio geo-politics ndani ya nchi yetu,chini ya SSH na CCM kwa mazingira ya Leo na mtazamo wa mazingira ya hadi kufikia 2050

Viva Mama SSH,viva CCM viva Tanzania
 
Back
Top Bottom