Wanaume tunahitaji maombi ya ziada. Namshukuru Mungu kwenye hili la Malaya nimevipiga vita na mwendo nimeumaliza. Hawa watu awe mzuri vipi, ntamnunulia chakula na akihitaji nauli ntamsaidia lakini sio kugusana nao.
Kuna siku nipo mahali akaja mmoja wa kisomali, kusema ukweli alikua mzuri nywele ndefu kazibana vizuri. Analalamika njaa, nikamwambia agiza chakula, akapiga baadae akaomba ajiliwaze na kabia, nikamwambia agiza tu. Kichwani akajua hapa tayari marketing skills zimejibu. Akachezacheza na simu akaniambia anakuja Mara Moja.
Niliendelea kupata chakula na kinywaji kama dakika 40 akarudi nywele alivyozibana zimefunguliwa hazijawekwa sawa kama awali. Nikajua tayari kazi imeanza.
Baada ya muda nikamuaga naondoka, akahamaki kwanini namuacha? Nikamwambia nawahi familia. Nikajiuliza hata kama ingekua ni mhitaji na mteja, Yani nna ushahidi wote kwamba ametoka kupeana huko namie nikapatiwe?
Tulikutana Tena siku ingine akanilaumu namtelekeza, tukapiga stori mbili tatu, tukala, nikakumuuliza straight unafanya kazi gani? Kusema ukweli aliniambia bila kuficha anajiuza na kusingizia mambo mengi kwamba hapendi ila shida tu na elimu hana kaishia form two. Nikampatia nauli tukaachana.
Leo kanitumia Salam za mwaka mpya.
View attachment 2466762