Mnaopenda Kubebelea Watoto Taifa Hamjifunzi Tu?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Ifikie wakati serikali kupitia wizara ya michezo kutoa kalipio na ikibidi kuzuia kabisa tabia za baadhi ya washabiki hasa zinapokutana timu hizi mbili kubwa na mikusanyiko mikubwa kuja na watoto wadogo kwenye msongamano huo mkubwa kwani ni hatari kubwa endapo litatokea swala la mtifuko wa kukimbia na kukanyagana
Bado hata mwaka kuisha taifa lilipopoteza watu pale taifa siku ya kuaga mwili wa hayati Rais magufuli,miongoni mwa wahanga ni wale watoto wadogo wa familia moja toka kimara hadi leo nikikumbuka vifo vile nasikia kuumizwa sana tukio lile na hasa kuwaona wazazi wengine kuwa ni wazembe sana,kwanini tukio lisiangaliwe nyumbani katika tv?kumbebelea mtoto na kuja kumuweka katika risk ni akili gani Hiyo?
Watanzania tuwe tunajifunza wakati mwingine.
 
simba day walijaza watu zaidi ya uwezo wa uwanja ingetokea kuna maafa kuna balaa kubwa lingetokea
 
Kwenda kuangalia msiba uwanja wa taifa ndo inashangaza ,ila kwa mpira siyo mbaya but Cha kujiuliza mechi ya derby utakaaje na mtoto mda wote mle ndani?
Kuna siku mechi ya derby jamaa aliingia na mtoto wa kama miaka 6 ,yeye kavaa Simba mtoto kamvalisha jezi ya yanga halafu akaenda kukaa uwanja wa Simba ,watu walimkamata mtoto kwa nguvu wakavua jezi ya yanga na kuchana chana,mtoto alilia sana.
 
Acha chuki yani ww kila penye ishu yenye jina la simba lazima utokeee. Kwani hukuona lile nyomii?
nyomi gani ambalo simba alikuwa nalo na yanga hakuwa nalo? Hebu leta picha kuonyesha simba ili jaza sana mashabiki kuliko yanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…