Huyu mtaalamu imani kwake imeondoka, anatuhumiwa kuujua ukweli wa hichi kirusi lakini anacheza na muda pamoja na akili za watu, kilicho baki kila mtu aamue mwenyewe nini afanye kutokana na ugonjwa huu kwa kuwa wataalamu wengi wamekuwa na maoni tofauti juu ya ugonjwa, tiba pamoja na chanjo ya Corona. Tatizo kubwa watu wamesahau magonjwa mengine yanayowasumbua na kufikiria Corona huenda baada ya muda haya magonjwa yakianza kutuangamiza ndiyo tutapokuja kuamka. Nasaha ni kila mtu ajiangalie afya yake, ukijihisi chanjo itakufaa piga na ukihisi chanjo itakupotezea muda basi achana nayo. KIMFAACHO MTU CHAKE.