Shem...kweli kukutana na mtu hakuna fomyula. Mnaweza mkakutana popote pale iwe kanisani, sokoni, shule ya vidudu, kilabuni, mtandaoni nk. Mwisho wa siku ni uamuzi binafsi wa mtu. Mimi binafsi niko open minded na mwangalifu sana kwa wakati huo huo.
Lakini kukutana na mtu mtandaoni kwangu mimi ni no-no kabisa. Mtu unayekutania naye mtandaoni una uhakika gani kuwa ni wewe unayewasiliana naye tu na hakuna wengine? Hii haimaanishi kuwa haiwezi kutokea katika settings zingine lakini mtandaoni nadhani risk level inaongezeka zaidi. Ndio maana mimi kamwe sitakuja kumwambia mtu yeyote information zangu kamili mtandaoni let alone kujisumbua kuwa na uhusiano serious na huyo mtu. Sana sana tukiwa na communication yoyote basi kwangu mimi nitaichukulia kama burudani flani hivi.
Ila natambua kuwa kila mtu ana maisha yake na kila mtu ana haki ya kujipangia hayo maisha kwa jinsi anavyotaka yeye. Kwa hiyo kama wapo wanaopenda kusaka wapenzi mtandaoni pouwa tu. Mimi hainisumbui na wala hainihusu kabisa.