Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Habari za asubuhi wanajamvi
Siandiki waraka huu kuharibu Biashara ya mtu au kwa chuki ila kwa nia njema kuepusha wanajamvi wenzangu kutokewa na yaliyonitokea.Na hata kama itatafsirika vibaya ila wameyataka wenyewe kwa kuharibu siku za watu.
Hawa vijana kwa wasiowafahamu ni wapiga picha za Video na Mnato hasa kwenye sherehe mbalimbali na Maharusi,Wanatumia Media sana kujitangaza sana kuwa ni wabunifu na wameweza kufanya lobying na kuchukua tuzo mbalimbali kitu ambacho kimewajengea kuaminika na kufuatwa na watu wengi sana.
Ila niwatahadharishe wanajamvi na Wengine wenye nia njema msije mkaingia kwenye mkumbo wa hawa wahuni na vijana wa mjini mkaharibiwa shughuli zenu msiamini kabisa kwamba kuna wanadamu wana roho za ajabu na kushindwa kuwa na utu kiasi hicho.
Ninaongea kwa yaliyonikuta mimi binafsi baada ya ukaidi,Niweke wazi nilitahadharishwa lakini nikajenga imani kwa kuangalia namna wanavyojitangaza na kupewa tuzo nikajua ndivyo walivyo,nikawapa siku yangu muhimu kabisa maishani ya kufunga ndoa yangu wanifanyie kazi ya Still picture na Video.
Aisee hawa vijana ni wahuni walichukua hela zangu wakaniharibia siku yangu walivuruga kazi zote pamoja na gharama kubwa walizochaji karibu vitu vingi wanavyoweka kwenye vipeperushi vyao ni utapeli havifanyiki na hivyo vichache wanavyoamua kuvifanya wao kwa matakwa yao huvipati utafuatilia miaka mimi nimeamua kuwaachia lakini nikiwa nimeumia sana.
Changamoto niliyoipata mimi sikuingia nao Mkataba nilikuwa nafanya malipo tu wananipa virisiti vyao vya Vitabu kwasababu ni wakwepa kodi pia nikashindwa hata kuwashtaki ila kwa jinsi walivyoniharibia shughuli yangu ningewapeleka mahakamani kama ningekuwa na Mkataba,Niwashauri wenye shughuli zenu ingieni tu Mkataba wa kisheria na Mavendors.
Kilichoniuma nilikuta watu wengi sana pale Ofisini kwao kila nikienda wanalalamika kufanyiwa vitu tofauti na makubaliano,kushindwa kupatiwa kazi zao,kuharibiwa shughuli zao nk niliumia sana kwasababu na mimi niliambiwa na dada mmoja nje wakati naenda kuwa ni wasumbufu nikakaidi baada ya kuwasikiliza manake wana sound balaa ikala kwangu.
Narudia nimeandika kwa nia njema ya kuzuia wengine wasitapeliwe au yasiwakute yaliyonikuta mimi,sherehe yangu ya harusi ambayo niliipanga kwa gharama kubwa sana na ndiyo siku yangu ya kipekee baada ya hapo ni kifo iliharibiwa na hawa wahuni,na kumbukumbu sina hadi leo kama mnavyojua picha ndiyo kumbukumbu zinazobakia.
Kwa jinsi nilivyoumia sipendi mtu mwingine aumie kama mimi au afanyiwe nilivyofanyiwa nimeona nina wajibu wa kutoka kushare na wenzangu.
Naruhusu povu kwa wenye upeo mdogo na watu wa kuchukulia mambo negative nimeshawasamehe ila wenye kuniona positive hii post itawasaidia.