Habari za asubuhi wanajamvi
Siandiki waraka huu kuharibu Biashara ya mtu au kwa chuki ila kwa nia njema kuepusha wanajamvi wenzangu kutokewa na yaliyonitokea.Na hata kama itatafsirika vibaya ila wameyataka wenyewe kwa kuharibu siku za watu.
Hawa vijana kwa wasiowafahamu ni wapiga picha za Video na Mnato hasa kwenye sherehe mbalimbali na Maharusi,Wanatumia Media sana kujitangaza sana kuwa ni wabunifu na wameweza kufanya lobying na kuchukua tuzo mbalimbali kitu ambacho kimewajengea kuaminika na kufuatwa na watu wengi sana.
Ila niwatahadharishe wanajamvi na Wengine wenye nia njema msije mkaingia kwenye mkumbo wa hawa wahuni na vijana wa mjini mkaharibiwa shughuli zenu msiamini kabisa kwamba kuna wanadamu wana roho za ajabu na kushindwa kuwa na utu kiasi hicho.
Ninaongea kwa yaliyonikuta mimi binafsi baada ya ukaidi,Niweke wazi nilitahadharishwa lakini nikajenga imani kwa kuangalia namna wanavyojitangaza na kupewa tuzo nikajua ndivyo walivyo,nikawapa siku yangu muhimu kabisa maishani ya kufunga ndoa yangu wanifanyie kazi ya Still picture na Video.
Aisee hawa vijana ni wahuni walichukua hela zangu wakaniharibia siku yangu walivuruga kazi zote pamoja na gharama kubwa walizochaji karibu vitu vingi wanavyoweka kwenye vipeperushi vyao ni utapeli havifanyiki na hivyo vichache wanavyoamua kuvifanya wao kwa matakwa yao huvipati utafuatilia miaka mimi nimeamua kuwaachia lakini nikiwa nimeumia sana.
Changamoto niliyoipata mimi sikuingia nao Mkataba nilikuwa nafanya malipo tu wananipa virisiti vyao vya Vitabu kwasababu ni wakwepa kodi pia nikashindwa hata kuwashtaki ila kwa jinsi walivyoniharibia shughuli yangu ningewapeleka mahakamani kama ningekuwa na Mkataba,Niwashauri wenye shughuli zenu ingieni tu Mkataba wa kisheria na Mavendors.
Kilichoniuma nilikuta watu wengi sana pale Ofisini kwao kila nikienda wanalalamika kufanyiwa vitu tofauti na makubaliano,kushindwa kupatiwa kazi zao,kuharibiwa shughuli zao nk niliumia sana kwasababu na mimi niliambiwa na dada mmoja nje wakati naenda kuwa ni wasumbufu nikakaidi baada ya kuwasikiliza manake wana sound balaa ikala kwangu.
Narudia nimeandika kwa nia njema ya kuzuia wengine wasitapeliwe au yasiwakute yaliyonikuta mimi,sherehe yangu ya harusi ambayo niliipanga kwa gharama kubwa sana na ndiyo siku yangu ya kipekee baada ya hapo ni kifo iliharibiwa na hawa wahuni,na kumbukumbu sina hadi leo kama mnavyojua picha ndiyo kumbukumbu zinazobakia.
Kwa jinsi nilivyoumia sipendi mtu mwingine aumie kama mimi au afanyiwe nilivyofanyiwa nimeona nina wajibu wa kutoka kushare na wenzangu.
Naruhusu povu kwa wenye upeo mdogo na watu wa kuchukulia mambo negative nimeshawasamehe ila wenye kuniona positive hii post itawasaidia.
So namfahamu NICK, aliwahi kufanya Wedding ya Rafiki yangu mwaka huu hapo Dar es Salaam. ALIFANYA KAZI HIYO KWA UBORA NA UAMINIFU
Nilipoona hii post niliamua kumtafuta sikumpata, lakini rafiki yangu ambaye alifanya naye kazi alimpata na kumuuliza kuhusu Uzi huu ulioweka.
Ndugu, uzi wako una kasoro na viashiria kwamba UNATAKA TU KUMCHAFUA NICK KWA SABABU ZAKO. Kasoro hizo ni;
1. Huelezi Nick kakukosea nini haswa. Uko too general husemi ulichofanywa.
2. Umetanguliza kujihami kwingi kwamba huandiki kwa nia mbaya, ilinipa hofu kuona kwamba unaweza kuwa na nia mbaya. Umemaliza pia kwa kusema utaletewa povu, why uletewe povu kweny jambo hilo?
Nicki amejieleza na kuomba wanajamvi wapime mambo yafuatayo:
1. Yeye sio biashara ya mtandaoni ambayo mtu anaweza kupata tabu kuifahamu. YEYE NI KAMPUNI, INA OFISI ZAKE ZIKO SINZA. Hivyo kama kweli una malalamiko kwake, ni rahisi kabisa kumkamata na kufungua kesi. So fara Ofisni kwake hakuna malalamiko ya hivyo unavyosema kwamba eti unashindwa kumpeleka mahakamani.
2. Nicki anahusisaha suala hili na vita za kibiashara kwa sababu YEYE ANAJITANGAZA SANA NA KUTOA HUDUMA KWA BEI NAFUU jambo ambalo washindani wake kwenye biashara linawakera sana. Mnaungana kumpiga vita.
3. Nicki amehusisha hili na TUZO, mnajua wenyewe mambo yenu ya tuzo ambazo mwaka jana Nicki alishinda. Mwaka huu tena yuko Nominated, hivyo kuelekea tuzo hizo mmeanza kuwekeana fitna.
MSICHAFUANE, MWENYE MALALAMIKO YA KWELI TUAMBIE ULIFANYWA NINI, NICKI YUPO OFISNI KWAKE TUELEZE KWA NINI HUJAMKAMATA?
Uzi wako una dalili zote za chuki za kibiashara, umekosa mashiko na ukweli wa hoja. ACHA.