Mnaotaka kufanya kazi na wanaojiita Nickshine Media Production kuweni makini sana

Mnaotaka kufanya kazi na wanaojiita Nickshine Media Production kuweni makini sana

Naona wote huko juu mna andika taarabu tu na hamsemi ni kipi mlicho fanyiwa tujue.Mki ulizwa mlifanyiwa nini mna jibu ujinga tu...kuna mdau hapo juu kauliza swali la msingi [emoji116]

Umelipa hujapewa picha? Picha zmepigwa vibaya? Baadhi ya vitu kama Tv Screens setups hazikuwepo ukumbini?

Lakini still mna lalamika bila reasonable point semeni hayo matatizo[emoji35]
Ukiona hujaelewa basi ujuwe kinachojadiliwa hapa hakikuhusu.

Watu wa society na mambo ya social tumemuelewa vizuri.

Hawa watu ni kimeo mimi wedding yangu mpaka leo Flash sikupewa wakati package ni Dvd na flash na imagine huyo mtu namjuwa fika, je kwa watu baki atawafanyia uhuni gani?
 
Poleni sana jamani
weakness kubwa kwetu ilikua kuignore mkataba, ingawa ata tungefanya enforcement yoyote bado kwetu pasingekua na msaada kwasbb demage iliyokwishafanyika haiwezi kuwa recovered, emagine video ya harusi lakini matukio na wahusika wanaoonekana ni bw na bi harusi tu( camera zilikua attentive kwao tu audience kwa ujumla na matukio muhimu mengine hamna
 
Hii imewahi nikuta nilikubaliana na mtu kuhusu kunipiga picha na video futi, kilichonikuta na kosa nililofanya nikuwapa hela yote, kanitolea picha mbaya, photo album hajaleta mpaka leo, Hawa vijana wapiga picha ni wajinga they don't think about future wao wakilipwa wanajiona wamefika na wanao waharibia ni hao wateja wao.
Ndio ile nilikuona sehemu umevaa shera jeupe ?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Na nyinyi si mnapenda Title zao , na wao wanawaumiza hapo hapo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Sio title mtu unaye muamini tena kijana mwenzako una mpa deal Sasa utendaji kazi wao sio wakiuaminifu. Nikiwa na shughuli nitakuwa naalika wa mkoani wanaoendaga Hadi Kenya camera zao quality na hutumia Hadi drones na zile light tofauti na huku Dar Hawa vijana wa kiswahili hawana business mind hawafikirii kesho
 
Na nyinyi si mnapenda Title zao , na wao wanawaumiza hapo hapo

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Wabongo wengi ni wababaishaji tu kwenye issue nyingi,sio hizo tu nyingi tu,mtu akipewa kazi anafanya ovyo ovyo yaani hatuna uaminifu kabisa na kauli mbaya mbaya na anaona sawa tu.

Na ndio maana raia wengi wa kigeni na wahindi wanapenda kuwatumia ndugu zetu toka nchi jirani hata kwa kazi za kawaida kabisa.
 
Nachokiona kama point ni ufike shekilango toka ubungo mataa ila umezungukia ubungo>mwenge>bamaga>sinza>shekilango!

Umezunguka sana yani make your point clear...

Umelipa hujapewa picha? Picha zmepigwa vibaya? Baadhi ya vitu kama Tv Screens setups hazikuwepo ukumbini?
Dont beat around the bush...nimecheka sanaa, maana pia nimesoma maelezo meengiii...point ni moja tu.hahahah
 
Hii imewahi nikuta nilikubaliana na mtu kuhusu kunipiga picha na video futi, kilichonikuta na kosa nililofanya nikuwapa hela yote, kanitolea picha mbaya, photo album hajaleta mpaka leo, Hawa vijana wapiga picha ni wajinga they don't think about future wao wakilipwa wanajiona wamefika na wanao waharibia ni hao wateja wao.
Na ndio maana wakawa wapiga picha,hazinaga heshima hizo kazi maana zimejaa wahuni tu.
 
Na ndio maana wakawa wapiga picha,hazinaga heshima hizo kazi maana zimejaa wahuni tu.
Ni kweli hizo kazi ni za vijana waliofeli na wahuni wao wanaharibu kazi bila kufikiria kesho Yao wangekuwa na akili haya yasingetokea. Saa nyingine Bora kuajiri wakemya au nchi nyingine ila sio Watanzania wamejaa utapeli sana
 
Mi wapiga picha wengi ninaowajua wote walifeli shule,wengine walikosa Cha kufanya mtaani wakaona wajishikize huko kwny kupiga picha.Kifupi hawa Ni wahuni Kama mafundi nguo tu.
 
Mi wapiga picha wengi ninaowajua wote walifeli shule,wengine walikosa Cha kufanya mtaani wakaona wajishikize huko kwny kupiga picha.Kifupi hawa Ni wahuni Kama mafundi nguo tu.
Na hawana akili kweli hawa viumbe imagine unatoa kazi mbaya kwa wateja wakati ungekuwa unafanya vizuri hao wateja ndio wangekutangaza vyema. Nadhani wapiga picha ni wale failures wanaosema shule si muhimu ila Matokeo wanafanya ujinga kwenye kazi
 
Kama wewe upo famous sana kwenye jamii, watumie vendors wenye majina kwasababu wataogopa kukuharibia na watatumia event yako kujitangaza, watakupa best services.

Ila kama wewe ni ngumbaru kama mimi, fanya kazi na ngumbaru wenzako unaowamudu kuwakoromea wakikuharibia kazi. Na wao watahakikisha wanapambana wakupe huduma bora ili uwarecommend wengine waende kwao.

Nimeshakutana na watu wengi wanawapapatikia vendors wenye majina waliangukia pua vibaya sana.

Ni list ndefu sana.
 
Habari za asubuhi wanajamvi

Siandiki waraka huu kuharibu Biashara ya mtu au kwa chuki ila kwa nia njema kuepusha wanajamvi wenzangu kutokewa na yaliyonitokea.Na hata kama itatafsirika vibaya ila wameyataka wenyewe kwa kuharibu siku za watu.

Hawa vijana kwa wasiowafahamu ni wapiga picha za Video na Mnato hasa kwenye sherehe mbalimbali na Maharusi,Wanatumia Media sana kujitangaza sana kuwa ni wabunifu na wameweza kufanya lobying na kuchukua tuzo mbalimbali kitu ambacho kimewajengea kuaminika na kufuatwa na watu wengi sana.

Ila niwatahadharishe wanajamvi na Wengine wenye nia njema msije mkaingia kwenye mkumbo wa hawa wahuni na vijana wa mjini mkaharibiwa shughuli zenu msiamini kabisa kwamba kuna wanadamu wana roho za ajabu na kushindwa kuwa na utu kiasi hicho.

Ninaongea kwa yaliyonikuta mimi binafsi baada ya ukaidi,Niweke wazi nilitahadharishwa lakini nikajenga imani kwa kuangalia namna wanavyojitangaza na kupewa tuzo nikajua ndivyo walivyo,nikawapa siku yangu muhimu kabisa maishani ya kufunga ndoa yangu wanifanyie kazi ya Still picture na Video.

Aisee hawa vijana ni wahuni walichukua hela zangu wakaniharibia siku yangu walivuruga kazi zote pamoja na gharama kubwa walizochaji karibu vitu vingi wanavyoweka kwenye vipeperushi vyao ni utapeli havifanyiki na hivyo vichache wanavyoamua kuvifanya wao kwa matakwa yao huvipati utafuatilia miaka mimi nimeamua kuwaachia lakini nikiwa nimeumia sana.

Changamoto niliyoipata mimi sikuingia nao Mkataba nilikuwa nafanya malipo tu wananipa virisiti vyao vya Vitabu kwasababu ni wakwepa kodi pia nikashindwa hata kuwashtaki ila kwa jinsi walivyoniharibia shughuli yangu ningewapeleka mahakamani kama ningekuwa na Mkataba,Niwashauri wenye shughuli zenu ingieni tu Mkataba wa kisheria na Mavendors.

Kilichoniuma nilikuta watu wengi sana pale Ofisini kwao kila nikienda wanalalamika kufanyiwa vitu tofauti na makubaliano,kushindwa kupatiwa kazi zao,kuharibiwa shughuli zao nk niliumia sana kwasababu na mimi niliambiwa na dada mmoja nje wakati naenda kuwa ni wasumbufu nikakaidi baada ya kuwasikiliza manake wana sound balaa ikala kwangu.

Narudia nimeandika kwa nia njema ya kuzuia wengine wasitapeliwe au yasiwakute yaliyonikuta mimi,sherehe yangu ya harusi ambayo niliipanga kwa gharama kubwa sana na ndiyo siku yangu ya kipekee baada ya hapo ni kifo iliharibiwa na hawa wahuni,na kumbukumbu sina hadi leo kama mnavyojua picha ndiyo kumbukumbu zinazobakia.

Kwa jinsi nilivyoumia sipendi mtu mwingine aumie kama mimi au afanyiwe nilivyofanyiwa nimeona nina wajibu wa kutoka kushare na wenzangu.

Naruhusu povu kwa wenye upeo mdogo na watu wa kuchukulia mambo negative nimeshawasamehe ila wenye kuniona positive hii post itawasaidia.
So namfahamu NICK, aliwahi kufanya Wedding ya Rafiki yangu mwaka huu hapo Dar es Salaam. ALIFANYA KAZI HIYO KWA UBORA NA UAMINIFU
Nilipoona hii post niliamua kumtafuta sikumpata, lakini rafiki yangu ambaye alifanya naye kazi alimpata na kumuuliza kuhusu Uzi huu ulioweka.

Ndugu, uzi wako una kasoro na viashiria kwamba UNATAKA TU KUMCHAFUA NICK KWA SABABU ZAKO. Kasoro hizo ni;

1. Huelezi Nick kakukosea nini haswa. Uko too general husemi ulichofanywa.

2. Umetanguliza kujihami kwingi kwamba huandiki kwa nia mbaya, ilinipa hofu kuona kwamba unaweza kuwa na nia mbaya. Umemaliza pia kwa kusema utaletewa povu, why uletewe povu kweny jambo hilo?

Nicki amejieleza na kuomba wanajamvi wapime mambo yafuatayo:

1. Yeye sio biashara ya mtandaoni ambayo mtu anaweza kupata tabu kuifahamu. YEYE NI KAMPUNI, INA OFISI ZAKE ZIKO SINZA. Hivyo kama kweli una malalamiko kwake, ni rahisi kabisa kumkamata na kufungua kesi. So fara Ofisni kwake hakuna malalamiko ya hivyo unavyosema kwamba eti unashindwa kumpeleka mahakamani.

2. Nicki anahusisaha suala hili na vita za kibiashara kwa sababu YEYE ANAJITANGAZA SANA NA KUTOA HUDUMA KWA BEI NAFUU jambo ambalo washindani wake kwenye biashara linawakera sana. Mnaungana kumpiga vita.

3. Nicki amehusisha hili na TUZO, mnajua wenyewe mambo yenu ya tuzo ambazo mwaka jana Nicki alishinda. Mwaka huu tena yuko Nominated, hivyo kuelekea tuzo hizo mmeanza kuwekeana fitna.

MSICHAFUANE, MWENYE MALALAMIKO YA KWELI TUAMBIE ULIFANYWA NINI, NICKI YUPO OFISNI KWAKE TUELEZE KWA NINI HUJAMKAMATA?

Uzi wako una dalili zote za chuki za kibiashara, umekosa mashiko na ukweli wa hoja. ACHA.
Habari za asubuhi wanajamvi

Siandiki waraka huu kuharibu Biashara ya mtu au kwa chuki ila kwa nia njema kuepusha wanajamvi wenzangu kutokewa na yaliyonitokea.Na hata kama itatafsirika vibaya ila wameyataka wenyewe kwa kuharibu siku za watu.

Hawa vijana kwa wasiowafahamu ni wapiga picha za Video na Mnato hasa kwenye sherehe mbalimbali na Maharusi,Wanatumia Media sana kujitangaza sana kuwa ni wabunifu na wameweza kufanya lobying na kuchukua tuzo mbalimbali kitu ambacho kimewajengea kuaminika na kufuatwa na watu wengi sana.

Ila niwatahadharishe wanajamvi na Wengine wenye nia njema msije mkaingia kwenye mkumbo wa hawa wahuni na vijana wa mjini mkaharibiwa shughuli zenu msiamini kabisa kwamba kuna wanadamu wana roho za ajabu na kushindwa kuwa na utu kiasi hicho.

Ninaongea kwa yaliyonikuta mimi binafsi baada ya ukaidi,Niweke wazi nilitahadharishwa lakini nikajenga imani kwa kuangalia namna wanavyojitangaza na kupewa tuzo nikajua ndivyo walivyo,nikawapa siku yangu muhimu kabisa maishani ya kufunga ndoa yangu wanifanyie kazi ya Still picture na Video.

Aisee hawa vijana ni wahuni walichukua hela zangu wakaniharibia siku yangu walivuruga kazi zote pamoja na gharama kubwa walizochaji karibu vitu vingi wanavyoweka kwenye vipeperushi vyao ni utapeli havifanyiki na hivyo vichache wanavyoamua kuvifanya wao kwa matakwa yao huvipati utafuatilia miaka mimi nimeamua kuwaachia lakini nikiwa nimeumia sana.

Changamoto niliyoipata mimi sikuingia nao Mkataba nilikuwa nafanya malipo tu wananipa virisiti vyao vya Vitabu kwasababu ni wakwepa kodi pia nikashindwa hata kuwashtaki ila kwa jinsi walivyoniharibia shughuli yangu ningewapeleka mahakamani kama ningekuwa na Mkataba,Niwashauri wenye shughuli zenu ingieni tu Mkataba wa kisheria na Mavendors.

Kilichoniuma nilikuta watu wengi sana pale Ofisini kwao kila nikienda wanalalamika kufanyiwa vitu tofauti na makubaliano,kushindwa kupatiwa kazi zao,kuharibiwa shughuli zao nk niliumia sana kwasababu na mimi niliambiwa na dada mmoja nje wakati naenda kuwa ni wasumbufu nikakaidi baada ya kuwasikiliza manake wana sound balaa ikala kwangu.

Narudia nimeandika kwa nia njema ya kuzuia wengine wasitapeliwe au yasiwakute yaliyonikuta mimi,sherehe yangu ya harusi ambayo niliipanga kwa gharama kubwa sana na ndiyo siku yangu ya kipekee baada ya hapo ni kifo iliharibiwa na hawa wahuni,na kumbukumbu sina hadi leo kama mnavyojua picha ndiyo kumbukumbu zinazobakia.

Kwa jinsi nilivyoumia sipendi mtu mwingine aumie kama mimi au afanyiwe nilivyofanyiwa nimeona nina wajibu wa kutoka kushare na wenzangu.

Naruhusu povu kwa wenye upeo mdogo na watu wa kuchukulia mambo negative nimeshawasamehe ila wenye kuniona positive hii post itawasaidia.
 
Pole Sana Mkuu

Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni

Umetoa Angalizo Kesho Mwingine Atakwenda Huko Huko
 
Hadi ikukute ndio utaelewa kaka, yani kwanza kama hawa vendor tuliotumia sisi walisisitiza tuwalipe malipo yote ndio mkataba unasema ivyo( ingawa hatukuusain alituambia atatutumia kwa email tusain kutokana na wingi wa mambo zile siku za mwisho tukasahau kusain ingawa oia hakuutuma na tuliona tunadeal na watu professionals wenye ethics za kazi kumbe ni sifuri) na tulikua recommended kwao na mtu credible ambaye wamefanya nae kazi, kitu nilichogundua ni hwa watu wenye majina huwa wanajali zaidi macelebrities ili wawa tangazie kuliko sisi tusio na majina ambapo sasa, sisi tusio na majina ndio sehemu kubwa ya wateja wao na wao bila kujua wanapoteza wateja kwa kutumisstreat sisi
Unamaanisha nini kuwaita vendors.

Pia nahisi kama vile una kitu unakifahamu na sasa unadivert thread.

Nakusoma kwa makini ndugu
 
Back
Top Bottom